Bernard Membe Kumburuza Kortini Hussein Bashe: AK-47 Vs Mawe!

Bernard Membe Kumburuza Kortini Hussein Bashe: AK-47 Vs Mawe!

vichwa vya samaki vyote hivyo...elephants killers:doh:
 
Kama mimi ningekuwa Membe nisingehangaika kihivyo na huyo Bashe, ni siasa hizo, la maana asubiri 2015 kwani JK atahakikisha hao wenye makundi hawataambulia kitu, kwake hatopoteza kitu hata akikorofishana nao kwani atakuwa keshamaliza urais, atarudi kijijini kwake Msoga kuendeleza shamba lake la mananasi. Hivyo wao wamalizane tu, lakini kama ilivyowahi kusemwa, jina tayari analo.
 
Hapa ni kelele tu Ngoja tusubiri hiyo j.tatu.

Mwandishi kaandika kishabiki kabisa na nikambi ya Membe!
 
Huyu mwenye id ya chikakatata ni rafiki mkubwa wa kigwangalla someni comment zake nyingi humu jamvini au inawezekana hii Id anaitumia kigwangalla mwenyewe
 
Last edited by a moderator:

MBONA wanatukana Watu wa CHADEMA matusi ya NGUONI lakini MAHAKAMA inakaa kimya? Ina Maana kwa WA CCM kutukanwa UNAPELEWA ISSUE MAHAKAMANI?

Kweli hapo ndio UNAJUA HAKUNA SHERIA NCHINI mpaka UWE na U-CCM NDANI YAKO!!!
 
NDUGU WANABODI,

Kuna taarifa kwamba Waziri wa Manbo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernard Membe ame-engage wanasheria wake dhidi ya Ndg. Hussein Bashe, Kada wa Chama Cha Mapinduzi asiye na wadhifa wowote ule, juu ya kumkashifu na kumuita na kumshambulia kwa maneno makali yasiyo saizi ya heshima aliyonayo Waziri membe. Mhe. Membe ameamua kumburuza kortini Ndg Bashe mnamo siku ya Jumatatu ijayo, kwa mujibu ya jopo la wanasheria wake watatu maarufu na mahiri. Ndg. Bashe, siku moja kabla ya Mkutano Mkuu wa Nane Dodoma alituita waandishi wa habari na kutueleza kuwa "...Membe hafai hata kupewa ubalozi wa nyumba kumi kwa kuwa ni muongo, mnafiki na amezoea kuishi kwa kubebwa..."

Itakumbukwa Mhe Membe alikuwa ni mgombea maarufu na mahsusi wa U-NEC wajumbe kumi na akina Bashe na Lowassa walikuwa kwenye jitihada za hali ya juu kuhonga pesa ili asipite katika kinyang'anyiro kile sambamba na uhamasishaji mkubwa waliokuwa wakiufanya pia kutaka Rais JK ambaye pia alikuwa ni mgombea wa Kiti Taifa cha CCM apate kura za Hapana ili kumuaibisha, ikiwa ni pamoja na hoja ya Hussein Bashe na kundi lake kutaka Uenyekiti wa CCM utenganishwe na U-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkutano huu baina ya waandishi wa habari na Ndg Bashe ulichukuliwa kama sehemu ya mkakati madhubuti wa kutaka kuhakikisha Membe anaaibika na anashindwa uchaguzi ule ili kumkatisha tamaa na kumshusha hadhi kama mgombea Urais haswa ukizingatia kuwa Mkutano Mkuu ule ndiyo utakaopitisha jina la mgombea wa Urais wa CCM 2015; kinyume na mipango na fitna zao, pamoja na hela walizohonga aliibuka kidedea akishika nafasi ya sita bila kutoa hongo wala kuzunguka mikoani kutafuta kura, jambo ambalo liliwashangaza sana wanaCCM na wanahabari wengi waliokuwepo Mkutanoni pale - hali ambayo ilidhihirisha kuwa Membe ana umaarufu wa kutosha kushinda URais huku akigombea kwa kufuata misingi yote ya uadilifu. Pia ikizingatiwa kuwa mshindani wake mkubwa Mhe Lowassa aliliogopa kundi la kifo la NEC na kwenda kugombea UNEC jimboni kwake Monduli.

Lengo la mkutano wa dodoma baada ya uchaguzi ilikuwa kuvunja makundi kingwa na bashe walipatanishwa na wengine wengi sasa hili la membe kumburuza mahakamani limetoka wapi?
 
Lengo la mkutano wa dodoma baada ya uchaguzi ilikuwa kuvunja makundi kingwa na bashe walipatanishwa na wengine wengi sasa hili la membe kumburuza mahakamani limetoka wapi?

Kuvunja makundi hakuna maana kuvunja kazi ya mahakama, Membe vs Bashe ni kesi inayowahusu wao wawili sio CCM Bashe anahaha kutaka aombe radhi kwa Membe ili yaishe na waliomtuma wameanza kumsusa. Nadhani Bashe atajifunza kwamba anayekununua pia ana uwezo wa kukuuza. Naam, Lowasa ananunua na kuuza, Shigela na Malisa nao wako sokoni kwa bei nafuu sana maana JK kawaambia hawafai, Mwigulu kapewa mtihani. In short Lowasa anauza wachezaji wake wote ili afanye usajili mpya. Unasahau kwamba Lowasa ana degree ya sanaa aka kiini macho.
 
Mwandishi gani wewe hujui hata ethics za kazi yako?
Habari kama ngonjera peleka hukohuko kwenu
NDUGU WANABODI,

Kuna taarifa kwamba Waziri wa Manbo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernard Membe ame-engage wanasheria wake dhidi ya Ndg. Hussein Bashe, Kada wa Chama Cha Mapinduzi asiye na wadhifa wowote ule, juu ya kumkashifu na kumuita na kumshambulia kwa maneno makali yasiyo saizi ya heshima aliyonayo Waziri membe. Mhe. Membe ameamua kumburuza kortini Ndg Bashe mnamo siku ya Jumatatu ijayo, kwa mujibu ya jopo la wanasheria wake watatu maarufu na mahiri. Ndg. Bashe, siku moja kabla ya Mkutano Mkuu wa Nane Dodoma alituita waandishi wa habari na kutueleza kuwa "...Membe hafai hata kupewa ubalozi wa nyumba kumi kwa kuwa ni muongo, mnafiki na amezoea kuishi kwa kubebwa..."

Itakumbukwa Mhe Membe alikuwa ni mgombea maarufu na mahsusi wa U-NEC wajumbe kumi na akina Bashe na Lowassa walikuwa kwenye jitihada za hali ya juu kuhonga pesa ili asipite katika kinyang'anyiro kile sambamba na uhamasishaji mkubwa waliokuwa wakiufanya pia kutaka Rais JK ambaye pia alikuwa ni mgombea wa Kiti Taifa cha CCM apate kura za Hapana ili kumuaibisha, ikiwa ni pamoja na hoja ya Hussein Bashe na kundi lake kutaka Uenyekiti wa CCM utenganishwe na U-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkutano huu baina ya waandishi wa habari na Ndg Bashe ulichukuliwa kama sehemu ya mkakati madhubuti wa kutaka kuhakikisha Membe anaaibika na anashindwa uchaguzi ule ili kumkatisha tamaa na kumshusha hadhi kama mgombea Urais haswa ukizingatia kuwa Mkutano Mkuu ule ndiyo utakaopitisha jina la mgombea wa Urais wa CCM 2015; kinyume na mipango na fitna zao, pamoja na hela walizohonga aliibuka kidedea akishika nafasi ya sita bila kutoa hongo wala kuzunguka mikoani kutafuta kura, jambo ambalo liliwashangaza sana wanaCCM na wanahabari wengi waliokuwepo Mkutanoni pale - hali ambayo ilidhihirisha kuwa Membe ana umaarufu wa kutosha kushinda URais huku akigombea kwa kufuata misingi yote ya uadilifu. Pia ikizingatiwa kuwa mshindani wake mkubwa Mhe Lowassa aliliogopa kundi la kifo la NEC na kwenda kugombea UNEC jimboni kwake Monduli.
 
Membe hana ubavu na hawezi fanya hivyo maana kupita kwake kumetokana na Kikwete kupiga mkwara na kubadilisha system ya uchanguzi nje ya hapo waliiba hata kura ilikuwapitisha waliokuwa wanawataka kwa kutumia usalama wa taifa. Na akifanya hivyo jua ccm inakufa kabla ya 2015.
 
Mtoa mada kashindwa kubalance hoja yake badala kaingiza
1. Mapenzi kwa membe. Freedom of action imekushinda.
2. Kujikweza kwa kusema Bashe alituita waandishi wa habari(Conflict of interest) katika hilo suala.
Kumfikisha mahakamani ni hoja ya msingi kwa vile mahakamani ni home of justice. Kuhusu kumkampenia membe u are wrong. Acha nature itaselect. Any one from either membe or lowasa even non of them can be a candidet 4 presidential post(ccm)
 
Kama habari hiyo ni ya kweli,Membe awashauri wanasheria wake kuahirisha mpango huo,maana Membe na huyo hasimu wake wote walikuwa mtandao mmoja,waliwafanyia fitina hizihizi wenzao kipindi hicho,leo dhambi imewaludia wanatafunana wao kwa wao.

haya ni malipo ya dhambi walizozifanya wakiwa pamoja,siku zote shetani huwa hana fadhira za milele ni MUNGU peke yake.Tafuteni uongozi kwa njia halali si rushwa na kupakana matope shetani atawadhalilisha
 
Naogopa kusema nisije na mimi nikaburuzwa mahakamani hiyo j3.
 
Kundi la LOWASA halifwatwi fwatwi,Usifwate nyayo za Simba kwa kutegemea Majungu na fitna,chezea LOWASA wewe uliza Mukama na Chiligati.
 
Kundi la LOWASA halifwatwi fwatwi,Usifwate nyayo za Simba kwa kutegemea Majungu na fitna,chezea ! LOWASA wewe uliza Mukama na Chiligati.
 
Kwa maonI yako kama kula za NEC ni kigezo then STEVEN MASATU WASIRA ndiye atakayepeperusha bendera ya CCM 2015
 
Achana kutuhangaisha na mambo yako ya kishambi,nenda huko na wewe ukawe mashahidi wa membe wako kwa vile ulikuwepo,akishida 2015 utakabiziwa wizari ya ushabiki. KISHAMBI, AKISHIDA, UTAKABIZIWA, WIZARI! kajifunze lugha kwanza!
 
Achana kutuhangaisha na mambo yako ya kishambi,nenda huko na wewe ukawe mashahidi wa membe wako kwa vile ulikuwepo,akishida 2015 utakabiziwa wizari ya ushabiki. KISHAMBI? AKISHIDA? UTAKABIZIWA? WIZARI? kajifunze lugha kwanza!
 
Unamaanisha Martin Shigella ? Unajua alitumia sh ngapi kuwa mjumbe ? hivi nyie watu wa ccm mkoje ? Unalinganishaje watoa rushwa na wasiotoa !

Mwambie ukweli huyo,

Siyo kwamba nashabikia ila nasema ukweli na ukweli huu unatoka moyoni kwamba pamoja na kumpiga vita Membe (kwa kufanya negative campaigns ili asipite), pamoja na wagombea waliokuwa wanaungwa mkono na kambi ya EL kuzunguka nchi nzima, na pia kuhonga zaidi ya milioni 850 ili wagombea wenu wapite bado ameshinda kwa kishindo tu. Tafsiri yangu ni kwamba EL hana nguvu kiasi hicho na anatakiwa kujifikiria mara mbili kama aendelee kuweka uadui na wenzake ama anyooke awe mstaarabu ili watakapochukua Urais wamhurumie kama mstaafu na wasimshughulikie, la sivyo akiendeleza uhasama na kuikwamisha serikali ambamo alikuwemo akatoka kwa tuhuma za ubadhirifu na utumiaji mbaya wa madaraka yake wakichukua nchi wanaweza kumshughulikia.

kibaya kilichotushangaza wengi tuliokuwepo pale ni kwamba jamaa walikuwa wanahangaika sana kupiga kampeni za kuwakwamisha wenzao badala za kujitafutia wao kura. Japokuwa nilifurahishwa na msimamo wa Mzee Makamba kwenye hotuba yake pale aliposoma mchezo na kuwakimbia kutoka kwenye hizo mbinu zao chafu na kusimama upande wa chama na mwenyekiti na kuanza kuwashambulia, japokuwa wengine walileta tafsiri tofauti kwamba Makamba ana kijana wake, tena ambaye ametazamwa na kupewa nafasi na mwenyekiti sasa hawezi kuacha kusimama na kundi la ushindi na lililo kwenye madaraka akabaki na mafisadi wasiotakiwa na chama na hata na nchi huku anataka wambebe mwanae
 
Back
Top Bottom