TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 13,749
- 21,202
Siwezi kusema kauli ya Father of The Nation Mwl. JKN kuwa mpinzani wa kweli atatoka ndani ya CCM, maana hata wakati wa Edo kauli hii ilitamkwa sana na kuaminisha umma kuwa sasa siasa ya Tanzania imepata uhalisia.
CCM ni chama chenye mizizi iliyosambaa sana kiasi ukichimba juu juu huwezi kuiona na unaweza kusema huu mti utakufa mbona unaishi pasipo mbolea hahahaaaa.
Hapana/Ndiyo kwa mtizamo unaoweza kuwa nao, hapa tunakutana na safari nyingine ya kisiasa ambayo kila uchaguzi mkuu unapokaribia visa vya aina hii huwa haviishi kabisa toka jemedari JKM alipokuwepo ukikumbuka wakati wa kambona mpaka yule jamaa aliyetaka kuanzisha jeshi la msituni ili kumng'oa Julius.
Leo tunaye (kitengo mbobezi au lijendari) Bernard Camilius Membe, jamaa anaonyesha nia adhimu ambayo naweza kusema inaleta chachu kuufikia uchaguzi wa mwaka huu kupitia (chama babu) CCM ambapo kwa uharisia hawezi kupenya kwa vyovyote na njia yoyote.
Hapa anakwambia "Unaweza kwenda Dar es Salaam kwa basi, kama basi limekuacha chukua pikipiki utafika"
Lakini anakwambia, "ningekupa majina yote sita ya vigogo wanaoniunga mkono"
Hebu mfuatilie kwenye mahojiano hayo nimekuwekea hapo.