Benki za Marekani kufeli ni ishara ya nini?

Okay, so kwa ushauri wako tu.. mtu afanyeje?
1. Tununue dollars?
2. Na hela zilizopo banks je zitakua salama bila kupoteza thamani kwa sie ambao zipo kwenye tzs?
3. Na kwa wale wenye hela zao kwenye government bonds wafanyaje?
Hakuna hela itakayokuwa salama ndani ya mfumo wa kifedha, endapo litatokea anguko au mdororo wa kiuchumi duniani. Hili naomba ulifahamu mapema kabisa. Kuhusu kunuanua US Dollars, ukweli ni kwamba hazitakuwa na thamani wakati wa mdororo wa kiuchumi kwasababu Fiat Currencies zote huathirika na mfumuko wa bei, Inflation. Ukiwa na uwezo mkubwa toa hela zako mapema leo, nunua vito vya thamani, Precious Metals, kama Gold-Coins and Gold-Bars.

Wale ambao mna, Sovereign Bonds mambo yanaweza kuwa mabaya endapo benki kuu itapandisha riba ili kudhibiti mfumuko wa bei. Bonds zitashuka thamani. Hali inaweza kuwa mbaya zaidi pale ambapo serikali itaamua kuingiza kufanya, Quantitative Easing. Serikali itaanza kununua Bonds zote ili kuongeza pesa mzunguko wa pesa kiuchumi. Sasa kama uliwekeza milioni moja na unasubiri kupata milioni mbili, AFTER BOND MATURITY, unaweza kupewa nusu ya hiyo hela ambayo unategemea. Hivyo ni hasara.

Serikali ya Tanzania inaweza kujipanga vizuri ili kudhibiti mfumuko wa bei na kuwasaidia watu wa kipato cha kawaida. Serikali inaweza kufanya, WAGE & PRICE FREEZE na mfumuko ukaisha ndani ya wiki. Serikali haitakiwi itegemee kupandisha riba peke yake kama mbinu ya kudhibiti mfumuko wa bei. Hili ndilo linaigharimu Marekani mpaka leo. Richard Nixon mwaka 1971 baada ya majanga kama haya kutokea, alitangaza, WAGE & PRICE FREEZE na ndani ya mwezi mmoja wakadhibiti mfumuko wa bei bila kuathiri wamarekani wa kawaida na mabenki.
 
Yale mabenki yalikuwa hayana mtaji wa kutosha kuweza kujiendesha, yalikuwa yanategemea watu waweke fedha ndiyo yaanze kuzifanyia kazi, hii ni kinyume na sheria. Kiutaratibu, kila benki inavyoanza lazima iwe na kiwango maalumu ambacho kiko, BOT na kile ambacho inaruhusiwa kuanza kufanyia kazi. Kile kiwango cha, BOT kinaweza kuja kutolewa endapo benki itakuwa na uhitaji mkubwa au imekumbwa na janga. Hili ndilo linaitwa, Fractional Reserve Banking.
 
Anayefuata ni credit Suisse ,Leo Yuko kwenye hali mbaya mno ,thamani ya hisa imeporomoka kupita maelezo , customer trust is at all time low ,hii benki inaenda kucollpase ,the madness goes on .
Hii financial collapse haitamwacha mtu salama ,mchina naye yuko kwenye hali mbaya na madeni yake ,benki zake za ndani nazo zinastruggle vibaya , soon naye ataanza kukipata cha moto ,ile Bailout waliyompa real estate giant "Evergrande" mwaka jana ili asicollapse sidhani kama ita workout this time , global finance iko kwenye hali mbaya
 
Zitaendelea kuporomoka. Mfumo wa uchumi wa kisasa umejengwa juu ya uongo.
 
First Republic Bank imefilisika ,hahaaa mpaka mabenki binafsi mengine yameingilia kati kuikopesha benki hii iliyofilisika ili isicollapse lazima maana wanajua ikicollapse lazima na wao waende na maji ,so wanachofanya sasa hivi ni kudanganya depositors Kwa kucreate maigizo ili depositors waamini kwamba mfumo wa kibenki uko sawa kumbe usanii mtupu .
 
Benki ya tano hiyo(Ya nne ndani ya USA). Na jamaa walisema pesa za bima za kuwafidia wateja zipo chini sana. Baada ya kuwalipa wateja wa Silicon valley bank na Silvrgate, wanaweza wasiweze kulipa wengine. Zikiendelea kuanguka itabidi tu wazifanyie bailout kwa pesa za umma.
 
Aiseeh umeandika vyema Sana...
 
Ukinunua dhahabu ukiuza sibei itapungua?
 
Nashukuru kwa maelezo
 
Uchumi wa Marekani ukitetereka na uchumi wa dunia unazubaa vilevile. Great economic depression ilitokea miaka ya 1920, mdororo wa uchumi 2008 ulianzia kule. Ingetokea COVID-19 ikaanzia Marekani uchumi wa dunia ungeyumba zaidi.
Ndio maana RUSSIA CHINA nawengine BRICS wanataka waondokane na huo utoto

Anguko la US liwe lakwake mwenyewe na shost zake wa EU sio wa DUNIA nzima

Multipolar ndio tiba sahihi na dedolarization ndio tiba sahihi zaidi

Hatujafika bado ila tunaelekea kwakasi
 
Haya ni maneno ya media za magharibi, ukitaka kusikia ukweli tazama RT ya Russia au CGTN ya china. Marekani uchumi wake upo matatani kila mtu mwenye ufahamu na uelewa mzuri wa mifumo ya kiuchumi hili atakuwa ameshaliona.
Kabisaa Us anapitia kipindi kigumu ila wacha tuone mwisho

Kama ndio anguko la dola ama nn
 
Mambo ya ugonjwa wa kovidi yalikuwa na ajenda nyingi za ufisadi wa kiuchumi dhidi ya nchi nyingine hivyo ukiwa na akili ndogo unaweza kudhani walikuwa wanatenda wema kumbe walikuwa wana sukuma kete ngumu kwa mtu wa kawaida kuweza kutambua ni mchezo gani wana cheza .
 
Sasa wewe umeeleweka vyema. Sio yule aliyesema ubongo mdogo wa kuelewa.
 
US Na Uswis Banks Zao Kudorora Maana Yake Nasi Tutaguswa Tu Kwa Njia Yoyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…