#COVID19 Benki ya Dunia: COVID-19 imewarudisha Watanzania takriban 600,000 chini ya mstari wa umasikini

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,013


Leo Tarehe 29 Julai, 2021 Benki ya Dunia inazindua Toleo la 16 la Ripoti ya Hali ya Kiuchumi ya Tanzania, yaani "16th Tanzania Economic Update"

Toleo la Hali ya Kiuchumi Tanzania huchapishwa mara mbili kwa mwaka na Benki ya Dunia, likiwa na lengo la kutoa mtazamo wa uchumi wa ndani wakati pia likiangazia suala muhimu la kimkakati ambalo linalenga kukuza mjadala mzuri wa sera kati ya wadau na watunga sera.

Toleo la leo linaangazia Sekta ya Utalii, lengo likiwa ni kuangalia namna ya kubadilisha Utalii ili Kuelekea Sekta Endelevu, Thabiti na Jumuishi

Uchambuzi unajadili masuala ya muda mrefu yanayokabili utalii nchini Tanzania pamoja na changamoto mpya zilizoletwa na janga la COVID-19.

UPDATES:

Albert Zeufack -- Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia kwa Afrika


Kama ilivyooneshwa katika matoleo 2 yaliyopita ya Ripoti ya Hali ya Kiuchumi ya Tanzania, Tanzania imekamata fursa ya kutumia Teknolojia za Kidijitali inayoweza kusaidia kuongeza Ukuaji jumuishi na pia ni kipengele muhimu ktk kukabili athari za COVID19 Nchini

Ktk Biashara, Usafirishaji wa bidhaa za Tanzania kwenda nchi za EAC uliongezeka kwa 22% mnamo 2020. Hii ilikuwa chini kwa takribani 10%, lakini ni ishara nzuri

Ni muhimu kuipongeza Serikali kwa kufungua biashara na mianya zaidi ndani ya EAC

Tanzania bara, Benki zinakadiria ukuaji ulipungua hadi 2.0% mnamo 2020 kutoka 5.8% ya 2019 kutokana kwa athari katika sekta zinazouza nje kama Utalii, Uzalishaji Viwandani

Zanzibar Uchumi umepungua hadi wastani wa 1.3% kutoka 7.0% 2019

Athari ktk ustawi zimekuwa kubwa ambapo zaidi ya Watanzania 500,000 wanakadiriwa kuwa chini ya mstari wa Umaskini wa kitaifa Mwaka 2020 kutokana na Janga la COVID19

Janga hili linaendelea kuelemea sana Ajira na Vipato

Kuimarika kwa Uchumi wa Tanzania kunaweza kuwa kwa polepole lakini ishara ni nzuri kwa nusu ya pili ya 2021

Ukuaji wa Mikopo, Usafirishaji na shughuli za Mawasiliano ya Simu zinapanuka ktk viwango vya kabla ya COVID19, hali inayotia Moyo

Utawala mpya wa Tanzania uko katika kipindi tete cha Majukumu makuu mawili ikiwemo kushughulikia janga hili kwa muda mfupi na kuweka msingi wa kufufua sekta binafsi kwa muda wa kati hadi mrefu - ukianza na sekta ya Utalii

Ripoti ya Tanzania Economic Update tunayoizindua leo inaangalia sekta ya Utalii ambayo huchangia sehemu kubwa ya Uchumi wa Nchi na imekuwa sekta iliyoathiriwa zaidi kutokana na janga la COVID19 na huwa ishara kubwa ya kupona kwa sekta binafsi

Rasilimali za Kiuchumi na Kitamaduni za Tanzania hufanya Utalii kuwa fursa nzuri ya Kiuchumi

Utalii huongeza maendeleo kwa kutengeneza Ajira, kuongeza mapato ya Fedha za kigeni, kusaidia kuhifadhi Urithi wa Kitamaduni, na kupanua wigo wa kodi

Kati ya 2019 na 2020, Tanzania ilishuhudia kushuka kwa mapato ya Utalii kwa 72%. Athari kwa Wafanyakazi na Biashara ndogo zinaendelea kuonekana, na tunatarajia zitakuwa kubwa

Lakini, kuna fursa hapa ya kutafakari upya namna sekta ya Utalii inavyofanya kazi

Mfano ni kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Watendaji wa Sekta ya Utalii, kuhakikisha ufadhili sahihi ktk kusaidia biashara kuhimili hali hii ya mshtuko ambao haujawahi kutokea, na kuleta zaidi uwekezaji ili kusaidia usimamizi wa mandhari ya Bahari na Nchi kavu

Hii ni fursa ya kutumia uwezo usiotumika kwenye Utalii wa Tanzania ili kusaidia Ukuaji endelevu na thabiti, ongezeko la utengenezaji wa ajira jumuishi na kuchangia zaidi kwenye matarajio ya Nchi za Uchumi wa Kati


Wanajopo | Panelists
  • Prof. Wineaster Anderson -- Professor of Marketing, UDSM
  • Kennedy Edward -- Hotel Association of Tanzania
  • Sirili Akko – CEO, Tanzania Association of Tour Operators (TATO)

Prof. Wineaster : Tunapozungumzia Utalii, tunamaanisha Ajira na Uwekezaji, lakini huenda mbali zaidi kwasababu inaunganisha minyororo yote ya thamani ktk utalii. Hivyo, unapambana na Umasikini.

Hivyo, Utalii ktk Nchi zinazoendelea kama zetu ni sekta inayohitajika kuondoa Umasikini

Kennedy Edward: Fursa kubwa ktk Utalii ambayo iko wazi ni Ajira na inaweza kupatikana kwa kufanya mabadiliko ya Kisekta.

- Utalii upo chini tangu Uhuru. Hivyo, Wadau wa Sekta lazima tukae na Serikali na kujadili changamoto tulizonazo na tunaendelezaje sekta hii

Sirili Akko: Kwa sasa, Utalii ni sekta iliyopigwa zaidi na kuna haja ya kulizingatia jambo hili pekee

- Angalau kwa sasa kabla hatujafikiria kupiga hatua tunapaswa kuhakikisha tunastahimili vishindo

Prof. Wineaster: Tunahitaji kukuza uwezo wa kiujuzi kwa Watu wetu. Zaidi ya 90% ya Watanzania ni Vijana Huu ni mtaji katika kuongeza nguvu kazi kwenye sekta ya Utalii na huduma zake. Kwa hiyo tujikite katika kukuza nguvu kazi hii

Kennedy Edward: Sekta ya Utoaji Huduma inakabiliwa na Changamoto nyingi za ufanyaji Biashara kutokana na msururu wa Kodi, Ada na vigezo Hizi zimefanya Utalii wa Tanzania kuwa wa gharama sana ikilinganisha na washindani wetu Afrika Mashariki na Kusini

Sirili Akko: Tunapitia shida ambayo naweza kuiita "athari za Kimisionari ", kwasababu Wamisionari wametufundisha kuamini kwamba kuna Jamii tajiri mahali Fulani ambayo iko tayari kumwaga pesa nzuri na kutuunga mkono

- Tunahitaji kufanyia kazi Mitazamo hii, ambayo kwa namna fulani inaathiri Sera zetu, na mwisho wa siku huathiri Biashara Pia, inaakisi kukosekana kwa msimamo na kupelekea kupoteza Wawekezaji makini

Prof. Wineaster: Ushirikiano wa Sekta ya Umma na Sekta binafsi ni muhimu sana katika kurejesha Sekta ya Utalii Katika hili, tunahitaji mijadala yenye tija juu ya kila kitu kilichopangwa katika kufufua Sekta ya Utalii

Kuna mateso mengi sana ktk utendaji na Watunga Sheria wanapaswa kuangalia utoaji wa mikopo rahisi, jinsi ya kutoa vifurushi vya hamasa pamoja na kusaidia Biashara hizi kufunguliwa tena

Prof. Wineaster: Tanzania ndiyo Nchi pekee ambayo tumehifadhi zaidi ya 25% ya Ardhi yetu - kwa maana ya Misitu, Mbuga za Wanyama Tuna Mbuga kubwa za kitaifa na zaidi ya vivutio 120 vya Kitamaduni na Kiakiolojia. Hivyo, tuna Mali kubwa. Kinachohitajika ni Uendelevu na Uvumbuzi

Kennedy Edward: Kwa sasa, Wafanyabiashara wote wanazungumza juu ya namna ya kuishi Hakuna anayezungumza juu ya kukuza au kupanua Biashara. Sote tunazungumza namna ya kustahimili katika kipindi hiki kigumu

- Tunapendekeza Serikali itoe motisha kwa Wafanyabiashara ikiwemo Msamaha wa Kodi au kipindi cha Neema ili kuvuka kipindi hiki kigumu Baadaye wakati mambo yote yakiwa sawa, tunaweza kuzungumza juu ya changamoto za ushuru, sera na mfumo wa udhibiti

- Tunapozungumza juu ya kuboresha Mazingira ya Biashara, tunahitaji kuelewa jukumu la kila mmoja Serikali ni mtunga Sera na Mdhibiti, sisi ndio Wafanyabiashara tunaohusika na miamala na kodi

- Kwa hivyo, kabla ya Maboresho au Mabadiliko ziangaliwe Kanuni, Sheria na Sera ambazo baadaye zitaathiri Wafanyabiashara Kuna haja ya kuwa na ushirikishwaji wa kila mara ili kuhakikisha mawazo yetu yako katika mstari mmoja

- Tunahitaji kuwa na udhibiti mzuri wa Maliasili za Tanzania Kuwe na Mfumo wa kuhakikisha Maliasili za Wanyamapori zinabaki kwa Wanyama na Maliasili za Binadamu zitumiwe na Binadamu
 
Mwaka jana tulikuwa uchumi wa katii (matatizo kede kede - ajira, COVID-19, etc)

Mwaka huu tutakuwa tumesogea uchumi wa juu kidogoo ama tumedorora?
 
Niko hapa nasikiliza ripoti ya benki ya dunia, kilichonigusa ni watanzania ambao walishatoka kwenye mstari wa umaskini na Covid19 imeamua kuwarudisha, imani yangu sehemu kubwa ya kundi hili inatoka kwenye sekta ya utalii na nyinginezo zilizofungamana na uchumi wa kimataifa. Hapo bado walioyumba lakini hawajagusa mstari wa umaskini.

Positive, Anguko la Tanzania lina ahueni kulinganisha na nchi zilizotuzungua(Labda policy ya kutojifungia ilitusaidia) though uchumi umeshuka

Hivi Serikali ilishafanya mpango wowote kuwakwamua? Hawa jamaa zetu walishayapatia maisha
 
Bahati mbaya mwafrika hata akifanya jambo la kushangaza dunia hutasikia negative impact kwenye dunia ya white people.
 
Jiulize wewe utaifanyia nini Tanzania na siyo Tz itakufanyia nini. (Nimetohoa kutoka kwa J.F. Kennedy)

Mkuu, Marekani yenyewe ilipokumbwa na Economic Crisis 2008 Serikali yao ilijitokeza kuyainua makampuni na watu waliorudishwa na janga lile(Japokuwa lilikuwa Human Made). Lazima atokee coordinator wa kuwaunganisha juhudi zao na kuwatoa kwenye mstari wa umasikini..
 
Mkuu, Marekani yenyewe ilipokumbwa na Economic Crisis 2008 Serikali yao ilijitokeza kuyainua makampuni na watu waliorudishwa na janga lile(Japokuwa lilikuwa Human Made). Lazima atokee coordinator wa kuwaunganisha juhudi zao na kuwatoa kwenye mstari wa umasikini..
poverty alleviation strategies should focus on individuals. Mbinu za kuongeza kipato
 
Daah yaani Covid-19 ni janga haswa imagine watu 500,000 wameingia kwenye umasikini, hapo bado watu ambao walikuwa kwenye umasikini na wakabaki huko huko
 
Nilikuwa Arusha siku chache zilizopita. Hali ya Uchumi kwa upande wa Utalii kwakweli inasikitisha. Lakini inajenga fursa kuona mbadala wa mazoea ya awali na kutengeneza akili mbadala za kukabiliana na majanga kama haya siku za usoni
 
Daah yaani Covid-19 ni janga haswa imagine watu 500,000 wameingia kwenye umasikini, hapo bado watu ambao walikuwa kwenye umasikini na wakabaki huko huko
Hiyo 500,000 izidishe mara (X) 5 Wastani wa Watu Tegemezi ndani ya hizi Familia zetu hivyo utagundua kuwa huenda 'Figure' ikawa ni Kubwa kuliko hii yao (yako) tajwa hapa.
 
Corona imepiga uchumi wa dunia. Mitaji, biashara zimeyumba, ajira katika utalii, biashara za Kimataifa zimetikiswa. Global political economy kwa sasa ni namna gani ya kurescue sekta ili kupunguza umasikini, kuimarisha sekta binafsi na umma, kutengeneza fursa za ajira, kutafuta na kutumia resources za kunusuru hali.

Hiki nilitegemea kukiona kwa vyama hadi vya upinzani nchini. Badala yake CHADEMA wanakuja na hoja ya Katiba mpya ambayo si ajenda inayoweza kujadili mipango ya dharura kusaidia kampuni za utalii kule Arusha, Kilimanjaro, kusaidia wakulima waweze kurejesha mzunguuko wa biashara, sekta binafsi iamke. Ni muhimu sana wanasiasa wetu wajue ajenda na mahitaji ya watu kwa wakati. #Uchumi kwanza.
 
Nilikuwa Arusha siku chache zilizopita. Hali ya Uchumi kwa upande wa Utalii kwakweli inasikitisha. Lakini inajenga fursa kuona mbadala wa mazoea ya awali na kutengeneza akili mbadala za kukabiliana na majanga kama haya siku za usoni
Sure ndugu kwenye jambo hili linatupa akili ya kujiongeza kuona njia nyingine za kutoboa kiuchumi maana kwa majanga kama haya tukitegemea sekta ya utalii pekee tutaaibika siku za usoni.
 
Back
Top Bottom