Benki Kuu ya Tanzania (BOT) yaifutia leseni benki ya FBME

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) yaifutia leseni benki ya FBME

Duh! Kweli Marekani taifa kubwa; lililofungwa Marekani limefungwa duniani pote na lililofunguliwa Marekani hakika na duniani limefunguliwa. FBME haiwezi tena kufikia mitandao ya Marekani ili kufanya miamala and therefore haiwezi kuifikia mitando ya duniani kuanzia NK, China, Russia, Iran, Syria, Europe, Afrika, Australia, na kwingineko.
 
Uuwwiii nina hela nyingi humo sijui itakuweje muniombee watanzania wenzangu
Ila nazani nitazipata si ndio eeh
 
Badala ya kuiliquidate hiyo bank, serikali ingetafuta mnunuzi mpya anunue rasilimali za benki hiyo ikiwa ni pamoja na madeni ya benk hiyo ili iendelee kutoa huduma chini ya mnunuzi mpya...
Utanunua na jina ama.. Mana kampuni imezuiwa kufanya kazi huko mbele sasa ww utaendeleaje kufanya kazi kwa kutumia jina lao..
 
Benki Kuu ya Tanzania imeifutia leseni ya kufanya biashara ya kibenki, benki ya FBME.

Suala la benki ya FBME na utakatishaji wa fedha limekuwepo muda mrefu baada ya serikali ya Marekani kuituhumu benki hii kuhusika na utakatishaji wa pesa kwa kiasi kikubwa nchini Cyprus. Wakati benkii hii imesajiliwa Tanzania, transactions nyingi na kubwa zilikuwa zikifanyika nje ya nchi. Wahusika hasa wa money laundering ni makampuni/nchi na hata waliopigwa marufuku kufanya biashara zao kupitia benki za kawaida. Hili swala la Cyprus ni maarufu sana duniani maana kuna tuhuma pia Russians Oligarchy pia waliikuwa wakitumia benki za nchi hiyo na kusababisha mtikisiko nchini huko kiasi kwamba cha mabenki kuweka kiwango maallum cha pesa zinazotelewa

Hapa kuna mafundisho na maswali kadhaa;

  • Hii tuhuma ya benki kusajiliwa Tanzania na kufanya biashara kwa asilimia kubwa nje ya nchi na katika nchi ambazo regulatory scrutiny zipo kidogo ni lazima zitazamwe kwa makini.
  • Hivi benki kuu haina uwezekano wa kufuatilia vyombo hivi mpaka viwe flagged na mamlaka za nchi za wenzetu?
  • Ni kwanini FBME iliamua kuweka makao makuu Tanzania na sio mahali pengine?
  • Hakuna uhalifu wowote unaohusu serikali ulifanywa na chombo hiki?
 
Back
Top Bottom