Benki Kuu ya Tanzania(BoT) yahamisha Mali na Madeni ya Bank M kwenda Azania Bank Ltd

Hiyo ni merger by operation of law? embu wataalamu watuambie, watupe na wanahisa wa hiyo Azania na watujuze maamuzi ya kwenda Azania na si benki nyingine yalifanywa kwa misingi ipi? MAJIBU TAFADHALI
 
Kwanini wanahangaika?! Wafunge bank zote tuweke pesa majumbani. Waliifungua yao (TPB) lakini wananchi sijui hawaielewi naona kama haina wateja vile. Nadhani sasa tutalipuwa mishahara BOT moja kwa moja.

Hiyo bank iko vizuri sana kwenye group lending.
 
Hahaha huwa nawaonea huruma waandishi wa habari yani hata konda akuitisha mkutano nao wanatumwa kuhudhuria.
Huyo gavana aandike tu anachosema atume kwa whatsap kila mtu mwenye simu atapata ujumbe. Unaweza kuta anaongea hata yasiyotusaidia.
Niliona juzi juzi TRA wanaongea na wanaongea na kutuma taarifa za makusanyo ya miezi sita. Hivi taarifa kama hiyo mimi inanisaidia nini?!
 
Hiyo bank iko vizuri sana kwenye group lending.
Hahaha ujinga huo, kulazimishana vitu visivyo work. Eti mjiunfe kikundi mkope, wakati kikundi hakiwezi kufanya kazi pamoja. Kila mtu akopeshwe kivyake akushindwa kulipa afe na msala wake.
 
Huyu n/gavana kakimbia swali...walitumia vigezo gani kuamishia madeni Azania?
Halafu mbona swali LA hawa wa DW hajajibu kapiga poroje....hii inaashilia nn kwa benki tatu kufungwa kiuchumi

Kwa kifupi benki nyingi ndogo nchini zina hali mbaya sana. Wanacheza na vitabu...
 
Wewe Roving Journalist, ask those guys the fate of FBME depositors.

FBME had different case to Bank Ms case. FBME was condemned to be facilitating Money Laundering activities, but it was financially sound.

Bank M has liquidity issues, for almost 2 years back it has failed to honour it's obligations on time. So expect most of depositors to lose.
 
Benki Kuu ni benki ya Serikali,wajibu wake ni regulate uchumi wa nchi ndio ina issue notes and coins,ndio in control all commercial banks kwa kuhakikisha liquidity ratios za benki za biashara haziteremuki chini ya kiwango kilichowekwa na central bank,benki ikiwa na deposits kidogo kuzidiwa na madeni chechefu benki kuu itafilisi..Hari ya sasa benki zetu ziko hoi nyingi zinapungukiwa na deposits wananchi wamerudi nyuma kuweka fedha zao benki .Hii inaashiria benki nyingi kukosa fedha za kukopesha wafanyabiashara,wakulima wajasiliamali nk.uchumi wetu waweza kuzorota ingawa unaonyesha dalili wa kupanda.
 
Jamaa kagongwa swali kaona ni gumu kahamia kwa mwenzie na kumnong'oneza....

"AISEE HILO SWALI GUMU SANA HEBU NIPE MATERIAL YAKO NIDESE... HAHAHAHAHA"

I smell something fish on this

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndo merger and acquisition?

kutoka mjati wa 1 trilion mpaka uwe chini ya bil 15 na madeni kibao?
 
Hahaha ujinga huo, kulazimishana vitu visivyo work. Eti mjiunfe kikundi mkope, wakati kikundi hakiwezi kufanya kazi pamoja. Kila mtu akopeshwe kivyake akushindwa kulipa afe na msala wake.

Lengo la group lending ni zuri tu, kuna wakulima wafugaji na vijana hawana dhamana na hawakopesheki, hivyo wanabidi waunde kikundi wajidhamini wao kwa wao (group guarantorship) na wanapata mikopo mizuri tu.

Kama una sifa za kukopesheka stand alone man mabank yako mengi yanakufata, ila kwenye group loans Tpb wako vizuri hawana muda mrefu toka waanze kukopesha vikundi ila wanaperform vizuri.
 
Hahaha binafsi sionagi faida ya vikundi, labda wenzangu mliowahi mimi nainaga matatizo tupu kwenye tuvikundi. Saccos hazikui kila kukicha malumbano na majungu tupu.
Hongera zao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom