benki gani nzuri kwa online services? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

benki gani nzuri kwa online services?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Uswe, Dec 26, 2010.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  nimekua nikitumia crdb kulipia vitu online, lakini nimepata matatizo mara kadhaa, kila inapotokea shida na pesa kurudihwa basi ujue hiyo ndo imekula kwako, mfano ukinunua kitu ebay, badae seller anasema hatoship tanzanzania na anaamua kurefund pesa yote, ujue hiyo pesa ndo imepotea, ukicheck statement ya, say paypal, amabyo mi natumia unaona kweli pesa imerudishwa lakini hiyo pesa hautaina kamwe kwenye account yako

  sasa, ni benki gani nzuri (ambayo mdau ametumia services zake na anarecomend) kwa kushop online?
   
 2. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana USWE habari za mchana .

  Natanguliza salaam zangu sijui kama wewwe ni Dada au Kaka. Mimi ukiniita kaka au mdogo wako wa kiume siyo mbaya.

  Narudi kwenye swali lako la Benki nzuri. Majibu niliyoyapata

  Ili hali ilivyo huko Tanzani ukweli mambo ya online banking ni hakuna kabisa. Niautoa Mfano wa benki maarufu ya Standard Chartered, Bclays za pale Arusha. Siku hiyo nikaona kulikoni kusafirisha fedha kupitia Western union basi nikaongee nao ili wanishauri uzuri wa online money transfer wakanieleza huwa system haijaanza na hawajui watanza lini kwani mtiririko wa wateja ndo utakaoamua uwesheshaji wa huduma hiyo kwa sababu haina maana kuanzisha huduma ambayo wataingia gharama kubwa ili hali wateja wa aina hiyo ni chini ya kiwango chao; mfano kama wana wateja mia wanoleta fedha online bila kupitia bank swift code kwa mwaka basi haina haja wao wapate hasara kwa ajili hiyo. Kwa hiyo system is not yet on the banking progress.

  CRDB yawezekana kama ulivyosema ukweli nao hawategemei financial export kama zilivyo benki nyingi pia huko TZ.
   
 3. n

  njemba fulani Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hao crdb ni wazushi,full kujitangaza alaf huduma hamna mi mwenyewe nshakata tamaa na hao jamaa kwenye online services
   
 4. U

  Uswe JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  nashukuru kwa majibu, ila mi nahitaji vitu viwili tu
  1, nikinunua kitu online niweze kukilipia.
  2. inapotokea matatizo/sababu yeyote seller/service provider akashindwa kudeliver na kuamua kunirudishia pesa basi pesa irudishwe kwenye account yangu, i understand kutakua na tofauti kidogo because of difference in exchange rate, but at least wairudishe, sasa hawa jamaa wa crdb hawana kitu kinaitwa refund, hela ikirudi huipati kabisa
   
 5. mapango

  mapango Member

  #5
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa hili ndugu yangu Ubwe usiwalaumu CRDB, ni bank zote hata za ulaya, ukinunua kitu ebay, unatumia paypal kufanya malipo, paypal ndio wanaochukua hela yako kutoka bank yako, hivyo inapotokea bidhaa imefeli na upate refund, seller atarejesha hela yako katika account yako ya paypal, kama unataka hela irudi kwenye account yako ya bank hiyo sasa ni juu yako, na sio ebay wala seller, unaweza kurejesha hela yako katika bank account, nenda katika paypal account, halafu nenda withdrawal.
   
 6. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kama nimemwelewa vzuri nikwamba hzo pesa hata kwenye paypal ac inakuwa akuna
   
 7. mapango

  mapango Member

  #7
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa ufupi Uswe haijala kwake, kwani pesa yake anasema ipo katika paypal account, cha kufanya ni kui-withdraw tu, au kufanya manunuzi mengine.
   
 8. U

  Uswe JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  paypal wamerudisha besa crdb, imetokea several times, nimeandika barua crdb, na nimeattach statement yangu ya paypal, crdb wanasema wanachunguza lakini hakuna hata trn moja walorudisha hadi hii leo na moja kati ya hizo ni ya ya muda mrefu sana, zaidi ya miezi kumi!

  hata leo nimemlipa mtu via paypal, inatoka kwenye account ya benki kwa sababu paypal wamerudisha pesa crdb
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  we malyamungu mbona una mbwembwe hivyo!!
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwa Tz sidhani kama paypal inalink na local account..i think it connects only to your credit card. Nadhani hapo ndipo kimbembe kilipo in case unataka refund au kuwa seller(kwa maana ya kupokea hela)..cha kufanya next time ukinunua kitu online usikimbilie kubonyeza button ya kulipa..m-contact seller kwanza kujua kama wana ship tz.
   
 11. mapango

  mapango Member

  #11
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ushauri mwengine, unaporejeshewa hela yako, wacha ibakie katika paypal account yako, unaweza kuitumia tena wakati wowote kwa vile kuna tatizo la kutofika katika bank account yako.
   
 12. Avocado

  Avocado Member

  #12
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli CRDB katika kutransfer fedha nje ni wa babaishaji sana hilo ni kati ya mambo ambayo yanawasumbua sana,ukifanya deal halafu ukatuma pesa nje kwa CRDB nakushauri utume mwezi mmoja kabla,vinginevyo utaonekana TP !
   
 13. mzozaji

  mzozaji JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2010
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wewe ungaeacha tuu hela ikae kwenye Paypal account yako, hakuna haja ya kutaka irudi kwenye account yako ya CRDB. Pesa iwe Paypal au iwe CRDB ni ya kwako hakuna ulazima irudi CRDB. Kwanza ikiwa kwenye Paypal inakurahisishia kununua wakati ujao. Ninachokushauri waambie Paypal wawe wanabakisha kwenye account yako any refunds. CRDB ni wazuri kwa online Banking kwa maoni yangu, ila inawezekana hapo wana mapungufu au kuna wafanyakazi wasio waaminifu wanacheza na pesa za namna hiyo kwani wanajua si rahisi watu kufuatilia au wao kugundulika. Pia haya mambo huwa yanafanywa na kundi la wafanyakazi kuanzia huyo unayempelekea malalamiko mpaka anayetoa hizo pesa.
   
Loading...