NBC ya sasa ni bora kuliko ile ya miaka ya 1967- 1997 kwa kuwa sasa mwananchi yeyote mwenye proposal yake nzuri na asset ya ku morgage anaweza kupata mkopo ndani ya siku 5. Ile ya zamani walikuwa ni wanasiasa wachache na wafanyabiashara maarufu kama kina R Mengi na Iddi Simba ndiyo walikuwa wanaaxcess mikopo na wakawa hawarudishi. NBC ya sasa inalipa kodi kila mwaka kuchangia pato la Taifa wakati ile ya mwaka 1997 ilikuwa inapewa ruzuku kila mwaka na hazina. NBC ya sasa inatoa ajira kwa transparency na ina zidi kufungua matawi mpaka mitaani mwetu.
Chuakachara musipende kushabikia mambo tu ali mradi mmesikia wanasiasa wanaropoko majukwaani, fanyeni na nyinyi utafiti kidogo. Mwalimu JKN alitaifisha njia kuu za uchumi na kuziweka mikononi mwa umma ". Lakini viongozi wa mashirika yetu au kwa kukosa elimu au kwa makusudi waliua yale mashirika. Iko wapi AISCO, BIT, HOSCO, RTC, GAPEX , Meya Textile Mwatex, Musomatex?
Nimekutajia mashirika yale tu ambayo yalishakufa kabla hata BWM hajaingia madarakani