Benjamin William Mkapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benjamin William Mkapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CHUAKACHARA, Mar 20, 2012.

 1. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Naona sasa ameibukia Bima ya Afya. Bado tunalia na wewe. Mwalimu alikukabidhi nchi uitunze, ukaihujumu kwa kutuibia. Umeuza nchi, hatuna nchi, wala lolote. Mwalimu anakusubiri akuulize!!!!
   
 2. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Chuakachara wewe si mkweli na si mjuzi wa mambo. BWM ndiye aliyesimamisha imara uchumi huu ambao nyinyi nyote including CDM na awamu CCM ya 4 manafaidi. Azimio la Arusha kwenye awamu ya 1 liliua uchumi katika utaifishaji wa mtaji binafsi, soko huria lililofuata wakati wa awamu ya pili liliua kabisa uchumi. Leo hii makampuni yanayoongoza katika kulipa kodi na kuajiri waTanzania wengi ni yale yaliyouzwa wakati wa BWM. Big respect to Ben
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  We wasema!! Mkapa yupo kwenye list of SHAME!!! Uchumi sawa uliimarika but at the expense of kuuza nchi kwa wageni!! Wapi benki zetu, NBC ilikuwa na tatizo gani etc. Wapi Kiwira, wapi nyumba za serikali etc. We wasema!!!!!!!!!!!!!
   
 4. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  NBC ya sasa ni bora kuliko ile ya miaka ya 1967- 1997 kwa kuwa sasa mwananchi yeyote mwenye proposal yake nzuri na asset ya ku morgage anaweza kupata mkopo ndani ya siku 5. Ile ya zamani walikuwa ni wanasiasa wachache na wafanyabiashara maarufu kama kina R Mengi na Iddi Simba ndiyo walikuwa wanaaxcess mikopo na wakawa hawarudishi. NBC ya sasa inalipa kodi kila mwaka kuchangia pato la Taifa wakati ile ya mwaka 1997 ilikuwa inapewa ruzuku kila mwaka na hazina. NBC ya sasa inatoa ajira kwa transparency na ina zidi kufungua matawi mpaka mitaani mwetu.
  Chuakachara musipende kushabikia mambo tu ali mradi mmesikia wanasiasa wanaropoko majukwaani, fanyeni na nyinyi utafiti kidogo. Mwalimu JKN alitaifisha njia kuu za uchumi na kuziweka mikononi mwa umma ". Lakini viongozi wa mashirika yetu au kwa kukosa elimu au kwa makusudi waliua yale mashirika. Iko wapi AISCO, BIT, HOSCO, RTC, GAPEX , Meya Textile Mwatex, Musomatex?

  Nimekutajia mashirika yale tu ambayo yalishakufa kabla hata BWM hajaingia madarakani
   
 5. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Uchumi kauuwa Nyerere pale azimio lake la Arusha. Mkapa kiuchumi kafanya vizuri kuiko raisi yeyote aliyewahi kutawala Tanzania. Nyerer alikuwa anti west and anti-semites, hizo sifa raiasi akiwa nazo hawezi kabisaa kujenga uchumi. Kenyatta alikuwa pro west west na Frend of Israel, ona alivyowajengea maisha bora wakenya.

  Komeni kabisaa kumtwika makosa ya nyerer mkapa ili hali mkiogopa kumsema vibaya nyerere ingawa naye kafanya mauzi kupita kiasi. wewe kuwanyang'anya hati miliki wanamuziki wa kitanzania wakati wanamuziki hao walijiajiali wenyewe kwa vipaji vyao, ni kitendo kizuri hicho alichokifanya nyerere? mbona nalo hilo jhamsemsemi ila kila kukicha mkapa eti kauza nchi.

  Kuonesha jinsi gani alivyowapenda wananchi wake, katujengea uwanja bora wa soka ukiwa ni mmoja mzuri sana barani africa mpaka DR Congo wametuiga kujenga uwanja kam wetu huko kwao. Benja, katuletea TRA,UDOM yenye kumeza 35,000 students, kajenga secondari nyingi sana, huyo nyerere kafanya nini si kama si kusimika azimio la arusha tuu. Hongera sana Benja, mungu akubaliki na akulinde leo kesho na keshokutwa. amina.
   
 6. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Nilidhani UDOM imeletwa na Kikwete!
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Makampuni unayomaanisha ni ya vilevi, mlewe ili wenzenu watimke na dhahabu, pombe ikiisha kichwani tayari mshaambukizwa vvu. na mnakuta mitoto yenu kumbe haikufundishwa skuli kwa maana hiyo mbumbumbu mzungu wa reli. nimekuchukia kama ninavyomchuki bwm
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  kauli yako ina reflect ukatili wa mkapa aliomfanyia nyerere, wewe jitu gani linaandika barua kuomba kujiunga na ukoo usio wake? kama si kujipanga kuzima tuhuma za kumrestisha in peace mzee wa watu ni nini? tena ukome kama net group solution!!!!!
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  wewe ulifaulu kusoma na kuandika tu. kibaraka la makaburu lione!!!!
   
 10. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Sishabikii mambo, UADILIFU umma ulioutegemea toka kwa Mkapa sio aliouonyesha!! Labda kwa vilke alizungukwa na wapenda hela wa kichaga wakamgilibu akapoteza mwelekeo. Mme mwenzake Mramba ameliibia taifa sana na ni kwa kulindwa na Mkapa. Msimteteee, hukumu inamgoja kama Mungu yupo. Wakatoliki wanamkumbatias, lakini Mungu si Athumani
   
 11. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nadhani Mkapa usiogope jitokeze uombe msamaha na uache siasa chafu kwani zimefifisha nyota yako
   
 12. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, ukweli ni kwamba tukubali alifanya mengi ya kuimarisha uchumi wetu. Kwa hilo umpe pongezi, na yale mabaya yake lazima tuyasemee. Hivi jaribu kufikiria kama NBC ingekuwa inaendeshwa na serikali kwa kutegemea ruzuku, hali ya ukata wa sasa hivi ingekuwaje?. Mimi ninaamini kuwa yeye alianzisha, hivyo serikali iliyofuata ilitakiwa kurekebisha sehemu alizokosea. Mfano masuala ya mikataba ya madini imerekebishwa, sasa ilitakiwa wajitahidi kuweka miundombinu ya kuchekechea huo udongo wa madini ili kila kitu kifanyike hapa au kudhibiti uchimbwaji wake. Lakini ukifuatilia kwa undani utakuta viongozi walio madarakani wana hisa zao katika hayo makampuni. Wakati wake kulikuwa na mpango wa kujenga nyumba za watumishi wilaya zote za tz, ulikuwa mpango mzuri kama ungeendelezwa. Magufuli alianza kufanya hivyo lakini awamu ya 4 hawakuendeleza.
   
 13. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kila binadamu ana mapungugu na BWM naye anayo alakini mazuri ya Ben ni mengi mno kwa kipindi chake alichotawala. Leo hii I swear wangesema tufanye uchaguzi na BWM awepo pamoja na akina JK, Slaa, EL, Lipumba na wengine wote hata akina Zitto na akina Migiro, nakuhakikishia BWM atashinda kwa kishindo. Hata tukiambiwa tutumie mtindo wa kusimama nyuma ya mgombea yaani kura ya wazi jamaa BWM ata emerge very high. You my hero Ben
   
 14. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Hizi sifa hizi, Hivi naota au? Mkapa ndio kajenga UDOM eeh, Mkapa ndio kajenga secondari nyingi eeh. Kumbe Mkapa aliendelea kuwa Rais mpaka baada ya 2005. Naota nini.

  Kwa kifupi Rais hachaguliwi kufanya mabaya, akifanya mazuri ni wajibu wake.
   
 15. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  huna lolote wewe kumsifia huyu jamaa fisadi
   
 16. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ufanisi wa hiyo NBC na mashirika yaliyobinafsishwa na Ben kwa MUONo wa juu juu haina MASHAKA BUT mnamshambulia chuakachara kwa aidha kugubikwa na wingu la ufisadi wa AMA kuhusika moja kwa moja AMA kuwa na mahusiano ya karibu na waasisi wa ufisadi inji hii ambao ni chama tawala.
  mnajua Ben aliuza kwa sh.ngapi NBC? Vp migodi huko Kama Barick na mingineyo? Zile airport zinafanya nini huko migodini? Je, ni kiasi gani cha kodi kinapotea kwa Kile kinachoitwa 5years tax holiday? Enzi za Ben kulikuwana Wizara maalum inayohusika na Ubinafsishaji......unajua hali za walohusika na wizara hiyo Leo? Ni kwa nini? Haya Makagoda na Meremeta mnajua yameibukia wapi?
  Hebu acheni kuchefua watu......Binafsi naona ni aibu kukaa na kuanza kumshabikia Huyu mzee....mnakera
   
 17. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  uwezo wako wa kumchambua Mkapa ndio umeishia hapo? au ulitaka kuanzisha thread tu
   
 18. A

  Adaha Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tukumbuke. Nyerere alisomesha watu bure toka shule ya msingi hadi PHD. Watu walitibiwa bure hadi hospiatali za rufaa bila ubaguzi. Kila kijana aliyemaliza shule hata yule wa darasa la saba alipata ajira. Bidhaa zilikuwa bei chini sana kwa mfano mwaka 1985 unga wa mahindi uliuzwa shilingi 1.5 kwa kilo. Nyerere alipigana vita ya Uganda na kupata ushindi mkubwa bila msaada wa inchi yeyote. Nyerere alipigania uhuru wa INCHI nyingi za Africa. Nyerere hakujilimbikizia mali.
  Hakika hakuna kama Nyerere na itachukua miaka mingi kumpata. Viongozi wetu baada ya mwalimu, raslimali nyingi za inchi zimehamishwa kuwasaidia wageni na wao wenyewe wakati wanainchi wengi wakikosa matumaini. Wakati wa`Nyerere hata ungezaliwa maskini lakini ukawa na akili nzuri bado ungeweza kusoma mpaka kiwango unachotaka bure. Sasa hivi shule za kata hazina waalimu kwa hivyo brain nyingi inafia vijijini na tunabaki na watoto wa wakubwa ndiyo wanasoma na kupata kazi nzuri lakini kuendesha inchi ovyo. Leo hii mhitimu wa chuo kikuu hana ajira je tunakwenda wapi na tunatetea nini.
   
 19. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mkapa ndiyo zaidi ya wote mpende msipende na bila yeye uchumi wenu ungekuwa mbuzi
   
 20. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Tunacholia ni jinsi ubinafsishwaji wa NBC ulivyofanywa kifisadi kwa bei ya kutupwa. NBC haikuwa na shida yoyote ilikuwa ni suala la utendaji tu. MBona CRDB ipo mpaka leo? mbona yenyewe haikuuzwa kwa makaburu? alipatikana mtanzania mwenye maono, serikali ikakaribisha wabia wazawa na mpaka leo inatoa ushindani wa kutosha. Postal Bank bado ipo. MKAPA NI FISADI WA KUTUPA NA SASA TUMEAMBIWA SIRI NYINGINE JUU YA KIFO CHA MWALIMU. hAKIKA SIKU INAKUJA TU NA HANA PA KUKWEPEA YEYE NA WENZAKE AKINA JK.
   
Loading...