Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 91
Mkapa ni Mwandishi wa Habari anajua kuwa akianza kujibu mapigo ndio utakuwa mwisho wake. Lakini anajua kuwa yeye ndiye aliyemsaidia Jk kuingia madarkani. Labda sisi wanaJf tusubiri kipindi cha Kampeni atapewa jukumu la kuendesha Kampeni ili Jk awe rais. Mimi nawambieni Ipo siku Hapa tanzania atakuja kiongozi na yeye atakuwa Chizi atawafunga wote hata huyu Jk kwa kufanya mambo kinyume cha Sheria za Nchi. Mbona Zambia na Malawi yanatokea mambo haya?? Ipo Siku inakujaShuhuda zipo mimi naona Mkapa alijitahidi sana kuiwekea nchi heshima ya juu haswa katika kukuza pato la taifa na kuzima mfumuko wa bei,maisha ya mtanzania ni ya kawaida sana kwa hiyo raisi anapoweza kumuwezesha kila mtanzania angalau kula mlo mmoja bila maumivu makubwa tunasema aliweza.
Aliikuta nchi iko pabaya sana alikuwa na ziada yakutufanyia watanzania tuwe na mwelekeo wa kiuchumi ili kuwa kazi ya taabu sana kwa hiyo panapostahili tumpe sifa.
Jk makundi yanamchanganya sana anapigana vita tatu wanompinga serikalini,wanompinga katika chama chake,na wananchi na wapinzani wote wamemkalia koo,yeye mwenyewe alikosea sana kuingia kwa njia ya mtandao na kutumia vyombo vya habari kumkandia,ndio maana yamemrudia na anapoteza umaarufu kwa haraka sana
Pamoja na matatizo yote ya Mkapa, kuna mtu anaweza kutupa walau mambo 10 tu ambayo rais wetu mpendwa JK amelifanyia taifa hili tunapoelekea kufikisha mwaka wa tano?
Binafsi nasema JK is a failure compared to Mkapa. Hata kina Mpendazoe ambao Phillemon Mikael anawakandia wanatumiwa na JK kumwandama Mkapa ili kuficha mapungufu ya JK.
Nipende au nichukie lakini binafsi sifurahishwi na utendaji wa serikali ya JK ambayo ilikuwa inatafuta namna zote za kumpunguza Magufuli lakini Mungu wa Israel na Mungu wa Yakobo bado anamsimamia mtumishi wake Pombe Magufuli.
Yapo mazuri katenda na yapo mabaya katenda. Mzani unaangukia wapi?
Mimi sikatai wala sikubali kuwa BWM ana tuhuma za kujibu. Sikatai kwa kuwa nasikia kwenye mawimbi tu kuhusu tuhuma hizo.Mahakama Huru na za kutafiti kujua kuwa kama kweli ana makosa au Kamati ya Bunge, Bunge Letu hawawezi kusafisha madudu haya wala nini. Lipo upande wa Mkapa kwa kazi yake nzuri katika Taifa lakini ukweli ni kwamba ana tuhuma za kujibu kwa Watanzania hivyo ni yeye mwenyewe ndio wa kusema.
Mimi nakubaliana na wewe kabisa, maana kama kweli huyu jamaa ana tuhuma lakini amefanya mambo mengi sana katika Taifa letu kwa ujumla hata kufikia kuona na kuona mambo mengi sana tumeweza kwasababu yake. hivyo watu wajitokeze kwa ajili ya kumpeleka mahakamani. siyo kinga yake au Katiba, Ni katiba ya Tanzania yenye matatizoMimi sikatai wala sikubali kuwa BWM ana tuhuma za kujibu. Sikatai kwa kuwa nasikia kwenye mawimbi tu kuhusu tuhuma hizo.
Haya sasa, wenye tuhuma kwanini hawachukui hatua ya kwanza ili haki itendeke? Ni nani anaetuhumu? Je, ni nani asietenda sahihi kwa taifa, mwenye tuhuma au mjua tuhuma na kukaa nazo bila kuchukua hatua na kubaki kupika majungu?
Mtu hatahukumiwa kwa yale aliyoyafanya tu, bali pia kwa aliyoacha kuyafanya, hasa akijua kuwa kuyatekeleza ni kutimiza haki. Kama BWM ni mkosefu, wale wote wanaomtuhumu mitaani wana hatia pia kwa kutochukua hatua stahili, hasa wakizijua hatua za kuchukua ili haki itendeke.
Miaka 10 kama kiongozi wa Taifa masikini kama hili lenye matatizo chungu mzima, kila hatua ya kutatua matatizo hayo ni lazima iwe na risk ya lawama. Kama binadamu ni lazima alikosea na wakati mwingine atakuwa alikosea sana. Ila alitimiza wajibu wake na akalifikisha Taifa alipoliachia likiwa na heri kuliko awali. Hata kama angekuwa hajafanya yote yanayosemwa kayafanya, bado matatizo yangetafutwa ili alaumiwe.
Mbona sasa Taifa linatikisika na hakuna anaetaka waliopo madarakani washitakiwe? Au halijatikisika na kuliwa vya kutosha?
Mimi nakubaliana na wewe kabisa, maana kama kweli huyu jamaa ana tuhuma lakini amefanya mambo mengi sana katika Taifa letu kwa ujumla hata kufikia kuona na kuona mambo mengi sana tumeweza kwasababu yake. hivyo watu wajitokeze kwa ajili ya kumpeleka mahakamani. siyo kinga yake au Katiba, Ni katiba ya Tanzania yenye matatizo
JF nini kumetokea??
takribani Miaka 2 iliyopita nilimtetea sana Mkapa ,humu ndani waumini wengi walinishambulia sana ati sikitakii kizazi cha watanzania yaliyo mema kwa kumtetea fisadi na tena hadi wakuu wakafikia kufananisha jina hili langu na la mkapa .
Sasa leo nauliza nini kinatokea? Siamini kuona watetezi wameongezeka kiasi hiki.
awajibishwe.