Akumbukwe kwa nini naye huyo? Kuna tofauti gani ya maisha baina ya utawala wake na ule wa Mwinyi na Kikwete? Rumba bado ni kali tu na Tanzania hatujawahi kuwa na ahueni ya maisha hata siku moja. Na hapo wala sijagusia mambo mengine .
Dhambi zinatofautiana mkubwa ndio maana yesu alisema anayesamehewa sana hupenda sana na anayesamehewa kidogo hupenda kidogo wakati wa yule CD.
Kikwete katika awamu yake ya kwanza aliinjinia kutolewa kwa kashfa dhidi ya BWM na hapo kwenye red, ni kweli jamaa hakushitaki bali aliamua kukaa pembeni na hata wakati wa kampeni zilizomfanya JMK kurudi madarakani jamaa alikaa pembeni kabisa na ilibidi watumwe wazee kwenda kumwomba ashiriki kampeni (mmoja wa wazee ni kingunge) kwani upepo haukuwa upande wao.Mwanzoni kabisa mwa utawala wa Kikwete(nasita kuweka neno Rais), vyombo vya habari vilimuandama sana kuandika kila kukicha maovu aliyoyafanya ikiwemo kashfa ya Kiwila, kila kukicha utasikia hili na lile kuhusiana na udhaifu wa utawala wa wake, ninaamini mengi yaliyokuwa yakisemwa dhidi yake yalikuwa ya kweli kwasababu hakuwahi kushtaki kwamba anasingiziwa na kushushiwa heshma yake bure, sana sana nakumbuka alisema "Watanzania mtanikumbuka"
Ilikua rahisi kwa Raisi wa tatu kutabiri kinachokuja kwani alimfahamu ajaye nyuma yake(raisi wa nne) anauwezo gani kiutendaji kwani aliufahamu utendaji wake kwa miaka kumi aliyofanya kazi chini yake kama waziri wa mambo ya nchi za nje. Kama asingelazimishwa na nguvu ya 'Mtandao' iliyokuwepo kuna kila dalili ya kuamini kwamba 'kijiti' kingekwenda kwa mtu mwingine kabisa.