Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

Jamani kila nyakati na mambo yake,mamboleo haya tunayotumia ndiyo yanayotufanya kuhisi/kuona kwamba hali ni ngumu lakini kumbe dunia ni ile ile na mambo ni yale yale hata aje nani.

Kwa mtizamo wangu wa kulaumiwa si wale wenye madaraka bali ni mfumo mzima wa dunia ya leo ya utandawazi ambao mwasisi wake kwa upande karibu wate wa maziwa makuu ni Rais mtaafu Benjamini William Mkapa ambaye nae pia kwa wakati ule hakuwa ya namna ya kuukwepa.

Vivyo hivyo hata wale watakaokuja lazima tu watakutana na changamoto za utandawazi uliokomaa,maana kizazi cha wakati huo kitakuwa tofauti na sasa.Ndio maana leo hii wapo waliopinga sera za Awamu ya kwanza,pili na tatu na wapo ambao wanazi-support sera hizo kitu ambacho si dhambi.

Cha msingi tu ndugu zangu hapa hakuna wa kulaumiwa huu ni wakati wa kuchangamkia fursa zilizopo.
 

shida uwezo mdogo!
 
Matatizo ya sasa ambayo Jk anaonekana ndo tatizo..chanzo ni mkapa..


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mkapa alikuwa jembe!Aliwapa dozi yao waandishi wa habari ambao asilimia kubwa wana uelewa mdogo sana!ingawa wana platform za kusemea na kuambukiza watu masikini wa nchi hii ujinga ili matajiri na wenye mamlaka watawale milele wakikandamiza wanyonge!Alikuwa shujaa wa uchumi na thabiti katika kauli zake.Hakuwa muongo bali aliusema hata ukweli mchungu!Sikumwamini,nikamwamini na ninamheshimu sana kwa kuwa sipendi kudanganywa!
 
Benjamin Mkapa alikuwa ni Reformer,alijitahidi kufanya reforms nyingi sana alipoingia madarakani,na moja ya hizo ni local government reforms,ni maoni yangu kama Serikali ya awamu ya 4 ingeendeleza pale alipoishia sasa hivi tungekuwa tunaongelea mambo mengine,alikuwa na mapungufu yake pia lakini alijitahidi sana.He is a reformer na ana sifa za kuwa reformer,hataki mchezo,na Rais ajae wa Tanzania itambidi afanye radical Economic and Political reforms kwa kweli kututoa hapa tulipo..
 
Mkapa ana mabaya yake ila alikuwa Raisi mwenye mamlaka tofauti na huyu Msanii wa sasa. Raisi wa wapi anahutubia jambo muhimu kwa nchi huku anajchekesha hata kama siio jambo la kuchekesha.
 

nakuunga mkono mkuu.
 
Binadam tuna mapungufu mengi, lakin tuangalie mazuru pia halafu tuweke kwenye mizani, BIG UP Ben Mkapa alifanya mengi mazuri, Wana mtandao walijaribu kumchafua lakin maneno yao hayawaingii waTz. Hakika tutamkumbuka!!!
 

Umeongea ukweli mtupu. Tatizo la wachangiji wa mada hii naona kama vile hawana info na kumbukumbu za serikali ya mkapa au wanaukwepa ukweli ya mambo makusudi. Watz wengi hatutafiti mambo kupata uharisia wake badala yake uongozwa na ushabiki, itikadi za vyama, dini na ukanda. Jeuri na matumizi ya hovyo ya mali za umma, ufisadi na uzalilishaji wa viongozi wa vyama vya upinzania vilishamili sana ktk utawala wa Ben Mkapa. Watu waongelea kukua kwa uchumi wakati wa Ben lkn wanasahau miundombinu ya reli zetu zimekufa mikononi mwake! Jeuri ya viongozi wa serikali kujimilikisha mali za umma kama magari na nk kwa majina yao binafsi! Viongozi kujiuzia nyumba za umma ktk maeneo nyeti ktk miji mbalimbali nchi hasa DSM. Ufisadi wote mkubwa unaoliteza taifa kwa kiasi kikubwa ulipaliliwa na serikali ya Ben na CCM yake.
 
despite his wiknesses, he tried to maintain economic status ya nchi. Imagne he went to power frm mzee ruska where in the hazina ya nch was empty, alot of debts, inflation juu mbaya! He managed to kip da nation back into shape co mchezo. Mkapa m2 wa kaz alyetambua nfs yake! Hata ww ungepata nafas kma yake pengne na ww ungtaka uwe na financial security in future c maintain da status. Mkapa jembe, m2 wa kaz na hana porojo porojo. Unajua afrika bila rais dictactor ngumu mambo kwnda! Lazma 2buruzwe mambo yaende by puttng pple into dere places!
 
Umemaliza mkuu !!
Tatizo letu Watanzani ni wavivu kufikiri na wepesi kusahau, Ben huwezi kumsafisha hata kwa jiki akatakata ktk utawala wake asilimia kubwa ya mikataba yote mibovu yeye ndio kaibariki leo eti tunamsafisha duuu aisee sisi kweli mazezeta.
 

tafadhali sana watke radhi watanzania,mh.mkapa hatakiwi kukumbukwa kwa lolote zaidi ya kupewa lawama za kufilisi rasilimali za nchi hii
 
hivi mnataka kusema wakati wa Mkapa hakukua na Rushwa?
 
tutamkumbuka sana mzee mkapa kwa kweli amefanya mengi mema pamoja na kuwa kila kiongozi anamapungufu yake lakini ss watu wa NKNK pamoja na wilaya yetu tutamkumbuka kwa kuruhusu kilimo cha kujikimu angalia alivyoondoka watu wamekufa na njaa na watoto nao kwa utapiamlo wakati tumezungukwa na utajiri wa kutisha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…