Benghazi yajitangazia utawala wake

Benghazi yajitangazia utawala wake

NICK2275

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
3,930
Reaction score
924
bengazi.jpg
Jeshi la Taifa la Cyrenaica, utawala mpya wa Benghazi nchini Libya

Viongozi wa wapiganaji na wa makabila katika mji wa Benghazi nchini Libya wamejitangazia utawala wao katika eneo la mashariki mwa nchi kama jimbo lenye uhuru.

Wanasema wanarejea makubaliano ya tangu miaka ya 1950 ya jimbo hilo, likijulikana kama Cyrenaica, lilivyoendeshwa kwa asilimia kubwa ya utawala.
Wengi wa watu wa Benghazi wamekuwa wakilalamika kuachwa nyuma na kubaguliwa kwa jimbo lao ambalo lina utajiri mkubwa wa mafuta Hatua hiyo inaleta wasiwasi kwa utawala wa muda mjini Tripoli.

Mwandshi wa BBC Gabriel Gatehouse aliyeko mjini Benghazi katika sherehe hizo amlisema mamia ya watu walikusanyika katika eneo la kuegeshea ndege katika kitongoji kimoja cha jiji la Benghazi.
Walicheza ngoma huku wakitoa kauli za kuunga mkono mfumo wa shirikisho.
Msemaji wa Baraza la wananchi wa Cyrenica aliiambia BBC kwamba makabila na wanajeshi wanaliunga mkono azimio linalohimiza eneo la Mashariki ya Libya lijitawale wenyewe.

Cyrenaica ina utajiri mkubwa wa mafuta na hatua hii itachochea taharuki ya ugomvi katika Tripoli na kwingineko kuwania udhibiti wa mali asili za Libya.
Lakini watu wake wanasema wanachokitaka ni kugawana sawasawa utajiri huo.
Azimio lao halina mashiko ya kisheria .

Kwa sasa Libya iko katika hali ya taharuki za kisiasa lakini baada ya miongo kadhaa ya kutengwa,hatua hii inaungwa mkono na wengi katika mji huu wa pili kwa ukubwa nchini Libya.

source:
BBC Swahili - Habari - Benghazi yajitangazia utawala wake
 
"Dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha. Na mimi naomba, na Mwenyezi Mungu anisamehe, iwamalize" Julius Nyerere (1995)

Wanabaguana ndani ya Kinchi cha watu 6 million
 
"Dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha. Na mimi naomba, na Mwenyezi Mungu anisamehe, iwamalize" Julius Nyerere (2005).

Wanabaguana ndani ya Kinchi cha watu 6 million
ngoja tuone watafikia wapi
 
Haya ndo yanatazamia wa kutokea siku soni ukivunjika muungano. Usishangae ukasikia Jamhuri ya Pemba, ohh Iamhuri ya Unguja, yetu macho kaza buti kijana Jusa
 
"Dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha. Na mimi naomba, na Mwenyezi Mungu anisamehe, iwamalize" Julius Nyerere (2005).

Wanabaguana ndani ya Kinchi cha watu 6 million

Nyerere yupi huyu aliyekuwa mbaguzi na mchoyo? (amekufa kabla hajaizamisha zanzibar kwa chuki zake)

Btw..Zanzibar watakuwa wamoja kuliko unavyofikiri wakashaacha kugawanywa na Tanganyika kutoka viako vya DODOMA na BUTIAMA lol

Labda utasikia majimbo Tanganyika kama cdm inavyonadi ..unajua kitakachofuata baada ya majimbo go forbid chadema wasishike Tanganyika lol
 
Hahahaaaa Topical nilikumbuka kwamba nimechemsha..........

Hayo ya Zanzibar na CDM tuyaache maana yataingilia mjadala husika
 
Libya haiwezi kukaa sawa tena,ardhi yao imejaa damu isiyo na hatia,
 
"Dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha. Na mimi naomba, na Mwenyezi Mungu anisamehe, iwamalize" Julius Nyerere (1995) Wanabaguana ndani ya Kinchi cha watu 6 million
"Miafrika ndivyo tulivyo" [Kwa hisani ya Nyani Ngabu]
Hapa mbaguzi ni nani, jimbo lenye utajiri linaloachwa
nyuma kimaendeleo au wananchi wanaodai haki yao?

Inatokea katika nchi nyingi ulimwenguni lakini Afrika imezidi.
ambako sehemu zote zilizo na utajiri ndizo zilizo masikini zaidi.
Angalia Equitorial Guinea, ambao ni wazalishaji wa pili wa mafuta
Afrika Kusini ya Jangwa la Sahara, watu wake wengi wanaishi
kwa chini ya dola moja kwa siku. DRC je na utajiri wa almasi?

Maneneo yenye madini Tanzani je? Binafsi ninaunga mkono
popote pale ambako rasilimali zinafurisha matumbo ya wana-
siasa na kuwaacha raia wakiponea hewa na maji. BTW, hata
hewa na maji wanayachafua.
 
Mtamkumbuka sana MUamar...R.I.P kamanda wangu we miss you..
 
Nyerere yupi huyu aliyekuwa mbaguzi na mchoyo? (amekufa kabla hajaizamisha zanzibar kwa chuki zake)

Btw..Zanzibar watakuwa wamoja kuliko unavyofikiri wakashaacha kugawanywa na Tanganyika kutoka viako vya DODOMA na BUTIAMA lol

Labda utasikia majimbo Tanganyika kama cdm inavyonadi ..unajua kitakachofuata baada ya majimbo go forbid chadema wasishike Tanganyika lol

acha we,nyerere angekua na nia ya kuibagua zanzibar asingeisaidia kakta mapinduz..coz haiifadshi bara chochote ..ila sishangai coz watu mlio na asili ya waarabu ndivo mlivo..
 
acha we,nyerere angekua na nia ya kuibagua zanzibar asingeisaidia kakta mapinduz..coz haiifadshi bara chochote ..ila sishangai coz watu mlio na asili ya waarabu ndivo mlivo..

You are very far from reality (go back to school)
 
Bengazi imepata ajali

Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom