figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,493
- 54,900
Tangu mwanzo nasema, Siasa za Nchi hii zina wenyewe, haijalishi wapo nje ya nchi wala ndani ya Nchi. Kwa taarifa tu, wenye nchi hawaogopi Vitisho hata Uongee kwa kufoka hadi Mic ilowane, wenye nchi hawaogopi.
Siku moja kabla ya Manji Kukamatwa alisema "Huwezi kuniita kama Mbwa wewe njoo, wewe ni mtoto mdogo kwangu". Alisema mimi situmii madawa ya kulevya, Mahakama ndo itaamua hii kesi.
Baada ya Siku Benard Membe akataka kuongea na Waandishi wa habari akapigwa Stop kuzungumza.
Vikao vya CCM vilivyomteua Magufuli kupeperusha bendera ya CCM, walikamatwa watu na begi limejaa noti wakadai zimetoka kwa Manji.
Tangu siku hiyo Membe alikasirika sana kufikia hatua ya kuanza kukosoa uongozi wa Magufuli.
Baadhi ya kauli zilizonkera rais na kuwakera wanaccm wachumia tumbo ni ambayo Membe alisema Magufuli kateua baraza kubwa la Mawaziri kawaweka kwenye mafungu waonekane wachache ila huyu rais hana jipya.
Pia Membe alionya hata kama tajiri vipi huwezi sema hutasafiri, nawahakikishia Magufuli lazima ataenda nje ya nchi. If you isolate yourself, you will be isolated (ukijitenga, utatengwa).
Membe amkosoa Magufuli
Membe: Magufuli anawafukuza watumishi kiurahisi kwakuwa hakuwateua yeye
Kwanini wanasisitiza rais aende nje?
Pamoja na manji kubambikiwa kesi zisizo na dhamana na kushikiliwa bila dhamana Polisi, mwisho wa siku katoka.
Unajua kwanini Membe alikatazwa kuongea? Mkutano wa Membe na wanahabari waahirishwa
Watu wamepewa kichwa wakala na Masikio, hii nchi ina yenyewe. Cheka na watu uvae viatu.
Wale matomaso, Yusuf Manji awe case study kwenu. Kila nchi ina Wababe.
Matomaso wengine watumie case study ya Lissu. Lissu kapigwa risasi lakini bado watu hawaogopi kuikosoa Serikali tena ndo wameongezeka.
Roma anakwambia weka bunduki chini tubishane kwa hoja.