Jamani wanaJF ni vyema tukajadili kwa hoja na wala siyo jazba. Kuna mtu anasema anamfahamu huyu mama ya kuwa ni mchapakazi hodari kwa hiyo anastahili tuzo na kuna wengine wanasema hastahili ila hawatoi hoja wanasema ni kada wa CCM. Hapa weredi uko wapi? Hatupingani kwa hoja ila kwa hisia kwa kuwa tu huyu mama amepinga elimu ya bure kama ilivyopendekezwa na CHADEMA? Tujuilize ili tuweze kujadili kwa uungwanga: NANI ANATEUA MFANYAKAZI BORA? Kama ni CCM basi huyu mama atakuwa nalipwa fadhila lakini kama si CCM ni kwa nini tusikubali kuwa ni mfanyakazi hodari na wafanyakazi wenzake (ambao baadhi yao ni wa CHADEMA: Huenda ni wengi kwa kuwa Moshi ni ngome ya CHADEMA) wameona hivyo na kuamua kumpa ufanyakazi hodari? JAZIBA NA KUKOSA UEREDI KUTAINYAKUA HESHIMA YA JAMII FORUM
Hakuna jazba hapa mkuu kwani tunaongea na data ambazo ni reliable na Valid. Elewa huyu mama ni mwajiriwa wa TAMISENI na inawezekana amependekezwa huko huko TAMISENI na inawezekana TAMISENI wamempa zawadi kwa jinsi anavyo battle na CHADEMA hapo Manispaa ya Moshi.
.. Alijitahidi sana kuhakikisha CDM aishindi Moshi lakn nguvu ya umma tu ilimshinda.. na sasa anajitahidi kwa hali na mali kulinda mali za CCM Moshi ambazo ilipora toka kwa wananchi hazirudi tena kwa wananchi!! MFANYAKAZI BORA KATIKA KULINDA MASLAHI YA CCM.!
Mkuu mimi ningefurahi sana kama ningejua huo ufanyakazi wake hodari umepatikanaje. Hii ni kwa sababu nimesikiliza wakati zawadi zinatolewa kwa wafanyakazi hodari nami nikasikia anatoka Halmashauri ya Moshi Mjini sikusikia kama ametoka TAMISEMI. Sasa nashindwa kujua amependekezwaje na TAMISEMI wakati hawakusema ni mfanyakazi bora wa TAMISEMI? kwa uelewa wangu kuna taratibu za kuchagua wafanyakazi hodari na taratibu hizi husimamiwa na vyama vya wafanyakazi. Kama kuna mwanaJF anajua mchakato wa kumpata mfanyakazi hodari wa Halmashauri ya Moshi anisaidie ili nami niridhike kuwa amepata ufanyakazi hodari kwa njia ambazo si sahihi. Vinginevyo kama amechaguliwa na wafanyakazi wenzake hapo Halmashauri nitashindwa kuamini kuwa hasitahili kuwa mfanyakazi hodari nitaendelea kuamini kuwa hatumkubali kwa kuwa amepinga elimu bure huko Moshi kama CHADEMA walivyotaka. Mimi siungi mkono CCM wala CHADEMA ila naogopa majungu na kuwa biased
JF: Where we Dare To Talk Openly
Na wewe ulijiunga baada ya nini?
Heshimu mawazo/michango ya wenzio mkuu,Umeleta Thread acha members waichangie,na si kila mchango lazima ulenge unachokitaka wewe....
Haya mambo ya kuanza kuangalia mchangiaji kajiunga lini hayaijengi JF hata kidogo
Tunaongea kwa sababu tunamfahamu ila be it amechaguliwa na TAMISENI au Manispaa ya Moshi kwa mchakato wowote najua hawezi kuwa the best. Mimi nimefanya kazi na halmashauri za moshi vijijini, Moshi mjini na Arumeru namjua huyu mama kwani ana tabia za kulazimisha na she is very hard woman. Na kumbuka ni mmojawapo wa wakurugenzi ambao wamefanya hii kazi kwa miaka mingi mno. Simwonei ila najua kuna waliostahili kuliko yeye.
tatizo kuna wafanyakazi wa msekwa, ila ni kweli tuwe makini
Lini hii ilitokea?? (kwenye bold)ni yule aliyezuia chadema-moshi kulipia watoto wa shule ada kwa madai kuwa wazazi watakosa uchungu wa elimu kwa watoto wao.
eti na yeye (kinabo) ni mfanyakazi hodari.
...inawezekana TAMISENI wamempa zawadi kwa jinsi anavyo battle na CHADEMA hapo Manispaa ya Moshi.
Mkuu una maana kabla ya CCM kujivua gamba na kusema kuwa JF ni hatari kwake kulikuwa hakuna wana CCM humu? Nadhani hii ni forum ya watu wote na jambo kuu ni hoja. Kama mtu ana hoja mujarabu iwe ya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, TANDU, JAHAZI ASILIA, n.k aiweke tu na kuitetea. Tupingane kwa hoja na si kuwa huyu mfanyakazi wa fulani. Tufungue mioyo na macho yetu kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu. Mategemeo yangu ni kwamba wana JF wanaweka maslahi ya nchi mbele kuliko magenge yao wanayoyaita vyama
...inawezekana TAMISENI wamempa zawadi kwa jinsi anavyo battle na CHADEMA hapo Manispaa ya Moshi.
Lini hii ilitokea??
hatua zozote zilichukuliwa?
Alikuwa ktk position gani?
........................ kumpa ufanyakazi hodari? JAZIBA NA KUKOSA UEREDI KUTAINYAKUA HESHIMA YA JAMII FORUM
Nachukia huu UPUZIIII ulioanza siku hizi hapa JF kuwa mtu asipo kubaliana kitu kidogo tu au akicoment kinyume na matakwa ya wengine, Basi eti HESHIMA ya JF INAVUNJIKA. Nani kawadanganya JF ipo,Ilikuwepo na Itaendelea kuwepo nyinyi na UPUUUZII wenu mtaondoka na wengine watakuja!
Jamani wanaJF ni vyema tukajadili kwa hoja na wala siyo jazba. Kuna mtu anasema anamfahamu huyu mama ya kuwa ni mchapakazi hodari kwa hiyo anastahili tuzo na kuna wengine wanasema hastahili ila hawatoi hoja wanasema ni kada wa CCM. Hapa weredi uko wapi? Hatupingani kwa hoja ila kwa hisia kwa kuwa tu huyu mama amepinga elimu ya bure kama ilivyopendekezwa na CHADEMA? Tujuilize ili tuweze kujadili kwa uungwanga: NANI ANATEUA MFANYAKAZI BORA? Kama ni CCM basi huyu mama atakuwa nalipwa fadhila lakini kama si CCM ni kwa nini tusikubali kuwa ni mfanyakazi hodari na wafanyakazi wenzake (ambao baadhi yao ni wa CHADEMA: Huenda ni wengi kwa kuwa Moshi ni ngome ya CHADEMA) wameona hivyo na kuamua kumpa ufanyakazi hodari? JAZIBA NA KUKOSA UEREDI KUTAINYAKUA HESHIMA YA JAMII FORUM
Mchakato mzima wa kuwapata hao wafanyakazi bora hauna uwazi hata kidogo kwahiyo watarajie watu kutoridhishwa na mshindi..