Benadeta Kinabo apewa tuzo ya Milioni Moja Mei Mosi

Jamani wanaJF ni vyema tukajadili kwa hoja na wala siyo jazba. Kuna mtu anasema anamfahamu huyu mama ya kuwa ni mchapakazi hodari kwa hiyo anastahili tuzo na kuna wengine wanasema hastahili ila hawatoi hoja wanasema ni kada wa CCM. Hapa weredi uko wapi? Hatupingani kwa hoja ila kwa hisia kwa kuwa tu huyu mama amepinga elimu ya bure kama ilivyopendekezwa na CHADEMA? Tujuilize ili tuweze kujadili kwa uungwanga: NANI ANATEUA MFANYAKAZI BORA? Kama ni CCM basi huyu mama atakuwa nalipwa fadhila lakini kama si CCM ni kwa nini tusikubali kuwa ni mfanyakazi hodari na wafanyakazi wenzake (ambao baadhi yao ni wa CHADEMA: Huenda ni wengi kwa kuwa Moshi ni ngome ya CHADEMA) wameona hivyo na kuamua kumpa ufanyakazi hodari? JAZIBA NA KUKOSA UEREDI KUTAINYAKUA HESHIMA YA JAMII FORUM

Hakuna jazba hapa mkuu kwani tunaongea na data ambazo ni reliable na Valid. Elewa huyu mama ni mwajiriwa wa TAMISENI na inawezekana amependekezwa huko huko TAMISENI na inawezekana TAMISENI wamempa zawadi kwa jinsi anavyo battle na CHADEMA hapo Manispaa ya Moshi.
 
Bernadeta Kinabo! Mfanyakazi bora!
Mfanyakazi bora asingeshawishi kuuzwa kwa bustani yetu pale Moshi
Mfanyakazi bora angundua angalao kipato familia zimzungukazo ambazo madiwani wake wameliona na kuamua kuwalipia ada watoto wao.
Mfanyakazi bora kwa lipi?
Moto utakaomuwakia atajuta kuijua Moshi,,,,,,,,,,muda ndio ushahidi mzuri
 
Hakuna jazba hapa mkuu kwani tunaongea na data ambazo ni reliable na Valid. Elewa huyu mama ni mwajiriwa wa TAMISENI na inawezekana amependekezwa huko huko TAMISENI na inawezekana TAMISENI wamempa zawadi kwa jinsi anavyo battle na CHADEMA hapo Manispaa ya Moshi.

Mkuu mimi ningefurahi sana kama ningejua huo ufanyakazi wake hodari umepatikanaje. Hii ni kwa sababu nimesikiliza wakati zawadi zinatolewa kwa wafanyakazi hodari nami nikasikia anatoka Halmashauri ya Moshi Mjini sikusikia kama ametoka TAMISEMI. Sasa nashindwa kujua amependekezwaje na TAMISEMI wakati hawakusema ni mfanyakazi bora wa TAMISEMI? kwa uelewa wangu kuna taratibu za kuchagua wafanyakazi hodari na taratibu hizi husimamiwa na vyama vya wafanyakazi. Kama kuna mwanaJF anajua mchakato wa kumpata mfanyakazi hodari wa Halmashauri ya Moshi anisaidie ili nami niridhike kuwa amepata ufanyakazi hodari kwa njia ambazo si sahihi. Vinginevyo kama amechaguliwa na wafanyakazi wenzake hapo Halmashauri nitashindwa kuamini kuwa hasitahili kuwa mfanyakazi hodari nitaendelea kuamini kuwa hatumkubali kwa kuwa amepinga elimu bure huko Moshi kama CHADEMA walivyotaka. Mimi siungi mkono CCM wala CHADEMA ila naogopa majungu na kuwa biased
 
.. Alijitahidi sana kuhakikisha CDM aishindi Moshi lakn nguvu ya umma tu ilimshinda.. na sasa anajitahidi kwa hali na mali kulinda mali za CCM Moshi ambazo ilipora toka kwa wananchi hazirudi tena kwa wananchi!! MFANYAKAZI BORA KATIKA KULINDA MASLAHI YA CCM.!

naunga mkooo hoja!
 
Mkuu mimi ningefurahi sana kama ningejua huo ufanyakazi wake hodari umepatikanaje. Hii ni kwa sababu nimesikiliza wakati zawadi zinatolewa kwa wafanyakazi hodari nami nikasikia anatoka Halmashauri ya Moshi Mjini sikusikia kama ametoka TAMISEMI. Sasa nashindwa kujua amependekezwaje na TAMISEMI wakati hawakusema ni mfanyakazi bora wa TAMISEMI? kwa uelewa wangu kuna taratibu za kuchagua wafanyakazi hodari na taratibu hizi husimamiwa na vyama vya wafanyakazi. Kama kuna mwanaJF anajua mchakato wa kumpata mfanyakazi hodari wa Halmashauri ya Moshi anisaidie ili nami niridhike kuwa amepata ufanyakazi hodari kwa njia ambazo si sahihi. Vinginevyo kama amechaguliwa na wafanyakazi wenzake hapo Halmashauri nitashindwa kuamini kuwa hasitahili kuwa mfanyakazi hodari nitaendelea kuamini kuwa hatumkubali kwa kuwa amepinga elimu bure huko Moshi kama CHADEMA walivyotaka. Mimi siungi mkono CCM wala CHADEMA ila naogopa majungu na kuwa biased

Tunaongea kwa sababu tunamfahamu ila be it amechaguliwa na TAMISENI au Manispaa ya Moshi kwa mchakato wowote najua hawezi kuwa the best. Mimi nimefanya kazi na halmashauri za moshi vijijini, Moshi mjini na Arumeru namjua huyu mama kwani ana tabia za kulazimisha na she is very hard woman. Na kumbuka ni mmojawapo wa wakurugenzi ambao wamefanya hii kazi kwa miaka mingi mno. Simwonei ila najua kuna waliostahili kuliko yeye.
 
tatizo kuna wafanyakazi wa msekwa, ila ni kweli tuwe makini

JF: Where we Dare To Talk Openly

Na wewe ulijiunga baada ya nini?

Heshimu mawazo/michango ya wenzio mkuu,Umeleta Thread acha members waichangie,na si kila mchango lazima ulenge unachokitaka wewe....

Haya mambo ya kuanza kuangalia mchangiaji kajiunga lini hayaijengi JF hata kidogo
 
Tunaongea kwa sababu tunamfahamu ila be it amechaguliwa na TAMISENI au Manispaa ya Moshi kwa mchakato wowote najua hawezi kuwa the best. Mimi nimefanya kazi na halmashauri za moshi vijijini, Moshi mjini na Arumeru namjua huyu mama kwani ana tabia za kulazimisha na she is very hard woman. Na kumbuka ni mmojawapo wa wakurugenzi ambao wamefanya hii kazi kwa miaka mingi mno. Simwonei ila najua kuna waliostahili kuliko yeye.

Mkuu mimi bado shida yangu ni mchakato. Kama amechaguliwa na wafanyakazi wenzake kwa njia za kidemokrasia basi ni the best kwa mujibu wa waliomchagua naa kama ungekuwepo wewe usingemchagua ila waliokuwepo wamemuona anafaa na kumchagua. Wewe kama umefanya kazi huko basi naomba unisaidie kujua mchakato wa kumpata mfanyakazi hodari wa halmashauri unakuwaje ili nami nijiridhishe vinginevyo naona hii ni vita ya CCM na CHADEMA nami sitapenda kushiriki kwa kuwa sivipendi vyama hivi.
 
tatizo kuna wafanyakazi wa msekwa, ila ni kweli tuwe makini

Mkuu una maana kabla ya CCM kujivua gamba na kusema kuwa JF ni hatari kwake kulikuwa hakuna wana CCM humu? Nadhani hii ni forum ya watu wote na jambo kuu ni hoja. Kama mtu ana hoja mujarabu iwe ya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, TANDU, JAHAZI ASILIA, n.k aiweke tu na kuitetea. Tupingane kwa hoja na si kuwa huyu mfanyakazi wa fulani. Tufungue mioyo na macho yetu kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu. Mategemeo yangu ni kwamba wana JF wanaweka maslahi ya nchi mbele kuliko magenge yao wanayoyaita vyama
 
ni yule aliyezuia chadema-moshi kulipia watoto wa shule ada kwa madai kuwa wazazi watakosa uchungu wa elimu kwa watoto wao.

eti na yeye (kinabo) ni mfanyakazi hodari.
Lini hii ilitokea?? (kwenye bold)
hatua zozote zilichukuliwa?

Alikuwa ktk position gani?
 
Mkuu una maana kabla ya CCM kujivua gamba na kusema kuwa JF ni hatari kwake kulikuwa hakuna wana CCM humu? Nadhani hii ni forum ya watu wote na jambo kuu ni hoja. Kama mtu ana hoja mujarabu iwe ya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, TANDU, JAHAZI ASILIA, n.k aiweke tu na kuitetea. Tupingane kwa hoja na si kuwa huyu mfanyakazi wa fulani. Tufungue mioyo na macho yetu kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu. Mategemeo yangu ni kwamba wana JF wanaweka maslahi ya nchi mbele kuliko magenge yao wanayoyaita vyama

humu kuna wanachama na wafuasi wa vyama karibu vyote. Tatizo ni kwamba kuna "wafanyakazi" wa msekwa na tunawafahamu. Aliyesema alikuwa anajaribu kumtambua mchangiaji maana hao akina msekwa wengi walikuja humu jf baada ya 1st episode kwenye comedy ya kuvua magamba
 
Lini hii ilitokea??
hatua zozote zilichukuliwa?

Alikuwa ktk position gani?

ilitokea kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Moshi mjini wakiwa kwenye kikao cha kupitisha budget ya 2011/12. Alikuwa kama katibu wa kikao kwa nafasi yake ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo. Hadi sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa
 
Huyu mama Mbaya
Huyu mama Mzuri

Hebu andikeni kwa urefu. Hakuna haja ya mafumbo. Uwazi! yapi ni mabaya na yapi ni mazuri ya huyu mama?
 
Dhana ya mfanyakazi bora ilishapoteza maana siku nyingi siku hizi mtu uchaguliwa pasipo na vigezo kuzingatiwa
 
........................ kumpa ufanyakazi hodari? JAZIBA NA KUKOSA UEREDI KUTAINYAKUA HESHIMA YA JAMII FORUM

Nachukia huu UPUZIIII ulioanza siku hizi hapa JF kuwa mtu asipo kubaliana kitu kidogo tu au akicoment kinyume na matakwa ya wengine, Basi eti HESHIMA ya JF INAVUNJIKA. Nani kawadanganya JF ipo,Ilikuwepo na Itaendelea kuwepo nyinyi na UPUUUZII wenu mtaondoka na wengine watakuja!
 
Tatizo siyo kucoment kinyume na matakwa ya mtu, tatizo watu wanandika hisia badala ya hoja. humu kuna wanachama kibao kwa hiyo kutofautia ni lazima
 
Jamani wanaJF ni vyema tukajadili kwa hoja na wala siyo jazba. Kuna mtu anasema anamfahamu huyu mama ya kuwa ni mchapakazi hodari kwa hiyo anastahili tuzo na kuna wengine wanasema hastahili ila hawatoi hoja wanasema ni kada wa CCM. Hapa weredi uko wapi? Hatupingani kwa hoja ila kwa hisia kwa kuwa tu huyu mama amepinga elimu ya bure kama ilivyopendekezwa na CHADEMA? Tujuilize ili tuweze kujadili kwa uungwanga: NANI ANATEUA MFANYAKAZI BORA? Kama ni CCM basi huyu mama atakuwa nalipwa fadhila lakini kama si CCM ni kwa nini tusikubali kuwa ni mfanyakazi hodari na wafanyakazi wenzake (ambao baadhi yao ni wa CHADEMA: Huenda ni wengi kwa kuwa Moshi ni ngome ya CHADEMA) wameona hivyo na kuamua kumpa ufanyakazi hodari? JAZIBA NA KUKOSA UEREDI KUTAINYAKUA HESHIMA YA JAMII FORUM

Mchakato mzima wa kuwapata hao wafanyakazi bora hauna uwazi hata kidogo kwahiyo watarajie watu kutoridhishwa na mshindi..
 
Mkuu hapo kwenye mchakato ndipo penye hoja. Hata mimi najua michakato mingi ya nchi hii huwa haizalishi matunda yanayotarajiwa. Kuanzia uchaguzi mkuu kumbe hadi kuchagua wafanyakazi hodari, mwenyekiti wa kijiji, mwenyekiti wa kikao cha harusi, nk. Ni wakati muafaka sasa wa kuangalia michakato ambayo inatuletea visivyotarajiwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom