Ben Saanane anastahili Tuzo CHADEMA

Ben Saanane anastahili Tuzo CHADEMA

Ni takribani miezi miwili tangu mwanachama wa Chadema Ben Saanane aibuke katika vyombo vya habari hususan mitandao mbalimbali ya kijamii na kile kinachoitwa kundi la Masalia ndani ya Chadema ambalo lilikuwa linatumiwa na CCM kuhujumu chama na ambalo lilikuwa pia na malengo ya kutukana na kukashifu viongozi wakuu wa chama kupitia mitandao ya kijamii.

Kati ya waliotajwa kuasisi na kuunda kundi hilo ni Mtela Mwampamba aliyegombea ubunge jimbo la Mbozi na Juliana Shonza
aliyekuwa Makamu Mwenyekiti BAVICHA.Ben alitoa ushahidi mbalimbali ambao kwa kiasi kikubwa ulisaidia BAVICHA kuwafukuza uanachama Mtela Mwampamba na Juliana Shonza.

Hata hivyo wako watu wachache waliolaumu na kupinga uamuzi huo na kusema vijana hao wameonewa.Hata hivyo leo yametimia baada ya vijana hao kurudi CCM na kuporomosha kila aina ya kashfa kwa chama cha Chadema na viongozi wake.

Ni ukweli ulio wazi kwamba aliyosema Ben Saanane leo yametimia pale aliposema vijana hao walikuwa wamepanga kuleta madhara makubwa ndani ya chama na hatimaye kutimkia CCM.Kutokana na ushirikiano wa Ben Saanane hatimaye vijana hawa walifukuzwa kwa hiyo hawakukamilisha mpango waliopanga kuhujumu chama.

Kuna wengine walipinga kitendo cha Ben Saanane kumhusisha Zitto Kabwe na vijana hawa mapandikizi hata hivyo vyovyote iwavyo Zitto Kabwe amebadilika sana tokea tuhuma dhidi yake zitolewe na yuko pamoja na chama katika shughuli za kukijenga tofauti na siku za nyuma.Ilikuwa ni nadra sana Zitto kushiriki maandamano ya Chadema kama alivyoungana na viongozi wenzie Jumapili ya kumlaani Spika wa bunge Zitto alishangiliwa sana Temeke Mwisho Jumapili pale alipomkaribisha Dr Slaa na kusema’’ huyu ni Rais wa watu ambaye hakutangazwa mshindi’’ Ni wazi mwenendo wa Zitto umebadilishwa na ujasiri wa Ben Saanane.

Bila unafiki wala upendeleo Chadema wanapaswa kumpongeza Ben Saanane kwa kazi kubwa aliyofanya kuwatifua Mapandikizi ya CCM na kuleta umoja na mshikamano ndani ya Chadema.

Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja kuwa Saa nane apongezwe na ikiwezekana apewe kitengo kabisa na aongezewe nguvu kazi kwani kazi aliyoifanya ni kubwa sana japo haijakamilika kwa sababu ya uoga wa chama kutochukua hatua kwa ZZK

Kuhusu ZZK kujirudi na kuonekana kwenye maandamano ya CDM juzi sio kweli kama amejirudi ila ni NJAA zilizompelekea kuinga kwenye maanda mano ya juzi nitafafanua.

Kuvunjwa kwa kamati ya bunge ya kudumu ya Kusimamia Mashirika ya UMMA (POAC) Ndilo jambo pekee lililomfanya ZZK aweppo kwenye maandamano yale na hakuna neno lingine lolote aliloliongee zaidi ya kuvunjwa kwa hiyo Kamati na utendaji wa Spika,NJAA ni kali tuhuma nyingi kwa ZZK ni kutokana na kamati aliyopewa hii ilimpelekea hata kutetea mitambo ya DOWANS kwa sababu ya NJAA.

Ukiangalia Picha zote ZZK akiwa kwenye maandamano ya juzi utausoma USO wake ni wa aibu na mara nyingi ameinamisha kichwa chini bado anajuta na anajua kilichomuweka kwenye maandamano yale ambayo yeye binafsi hayaamini ni NJAA yake kwa kufutiliwa mbali POAC

HII NI HATARI KWA CHAMA MAKINI.
 
Ni afadhali ya ulinzi kuliko kuishi mjini kwa kujipendekeza kwa mwanaume mwenzio ili akulee

Chama
Gongo la mboto DSM

Kwa hyo cku hzi umeamua kuwa mlinzi? Umeacha kuambatana na Nape kwenye mikutano? Endelea kujipendekeza ili akulee.
 
Kwa hyo cku hzi umeamua kuwa mlinzi? Umeacha kuambatana na Nape kwenye mikutano? Endelea kujipendekeza ili akulee.

Nape namsoma kwenye magazeti; nina elimu ya kutosha sana kujilea; nipo viwanja Nape nitaambatana naye wapi? Mkuu endelea na kutapika pumba

Chama
Gongo la mboto DSM
 
sera zenu ni zipi?

Sera zipo nyingi tu labda uweke wazi ni katika nyanja zipi elimu; afya; usafirishaji na nyanja nyinginezo sera ni wigo mkubwa natumai hilo unalijua kabla hujauliza

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hakika tunao vijana makini na BEN SAANANE ni mmoja wao na lazima tukubali kuwa cdm sasa kiko makini na mapandikizi, lazima yote yang olewe
 
Ninacho weza kusema nikuwa INTELEJENSIA ndani ya CDM imepevuka sana!! Amini nawaambia mengi yataibuka lakini mwisho wa siku wote tutafurahi pamoja baada ya ushindi 2015 . Masalia wataitwa mashujaa nawatapewa zawadi ya ushindi. Sababu tunacheza ngoma moja kwa staili tofauti. I love CDM 4REVER.!
 
Nimekuwa nasema mara kwa mara kwamba huyu anayeitwa Ben Saanane ni mtu wa kuchunga sana na hasa hawa viongozi wa chadema!,nasema hivyo kwa ababu kama ni kweli kwamba alikuwa amewekwa kwa ajili ya kazi maalum ya kuwafuatilia wenzake ama kuwategeshea hayo yaliyojitokeza kama ambavyo amejipambanua na kupambanuliwa huko nyuma,bsi huyu ni tatizo!:Ni mtu hatari na lazima waliomtuma kufanya hivyo atakuja kuwageuzia kibao siku za usoni ama atatumiwa na chama kingine kuwamaliza viongozi hao kama ambavyo alitumiwa na kuwamaliza wenzake.

Nasema hivyo kwa sababu kiongozi ama mtu mwenye busara ambaye an nia njema ya kujenga hawezi kukubali ushauri wa kuwamaliza wenzake anaokula nao,anaotembea nao,anaoshinda nao na kupangiana mikakati mbalimbali!,ukimweleza jambo kama hilo lazima atabaini kwamba kuna hatari inakuja mbele ya safari na lazima atawaa-Lert wenzake.Ben Atambue kwamba wenzake wametangulia kutokana na mikono yake yeye,na yeye atafuata kwa mikono yake mwenyewe na wao wenyewe.

Haa haa haaaa.....watu wanapenda sana kuwa manabii! Mtazamo wangu ni tofauti, inawezekana huyo wajina wa Mkapa alisikiliza akili za kuambiwa akafuata mkumbo, sasa alipochanganya na za kwake akajiona yuko nje ya maadili mema, akaamua kurudi kundini! Anastahili pongezi kwa hili.
 
Sera zipo nyingi tu labda uweke wazi ni katika nyanja zipi elimu; afya; usafirishaji na nyanja nyinginezo sera ni wigo mkubwa natumai hilo unalijua kabla hujauliza

Chama
Gongo la mboto DSM
kilimo.....
 
Ninacho weza kusema nikuwa INTELEJENSIA ndani ya CDM imepevuka sana!! Amini nawaambia mengi yataibuka lakini mwisho wa siku wote tutafurahi pamoja baada ya ushindi 2015 . Masalia wataitwa mashujaa nawatapewa zawadi ya ushindi. Sababu tunacheza ngoma moja kwa staili tofauti. I love CDM 4REVER.!
Na wewe acha kuwa na akili kama ubongo wa kuku, ni nani mwenye muda wa kupandikiza watu CCM? kuna Mtanzania gani asiyejuwa kwamba CCM ni genge la wezi tu na waliingia madarakani kwa wizi wa kura? Think big. Masalia wote they are dead & buried.
 
Na karibuni Ben Saanane atahamia CCM. Mtakuja kujadili humuhumu.weka hii katika kumbukumbu zako.

Mkuu,hapa Ben anapongezwa kwa kuwafichua mamluki wa ccm waliojificha ndani ya CDM ili kufanya uhaini,suala la kwamba atahamia ccm halina mashiko ilimradi kazi aliyoacha ameifanya inadumu.Mwl.Nyerere yuko wapi? lakini angalia mawazo na kazi alizozifanya bado zinaishi ndani ya mioyo ya watu.
Ben,ongera kwa kazi nzuri ya kuwatimua waroho wa madaraka ili tubaki na makamanda ambao wanachapa kazi na siyo wapenda madaraka.
Sonza na mwenzako mmerudi mahali sahihi pa kutafuta madaraka hata kwa mtutu wa bunduki(Basho na hKingalingwali)
 
Na karibuni Ben Saanane atahamia CCM. Mtakuja kujadili humuhumu.weka hii katika kumbukumbu zako.

Ben Saanane anastahili pongezi kubwa sana lakini sio kutoka CDM, ila ni kutoka CCM. Kazi anazofanya Ben ni kubwa sana. Ukifuatilia sinema zake na jinsi alivyokuwa akitengeneza scenes zake na wahusika..huwezi kupata tabu kuwa anamtumikia nani.

Mengi ameyaeleza mwenyewe akiwa anajibu mapigo ya wanaoitwa Masalia...kundi aliloshiriki kuliandaa kwa maelekezo wa anaowatumikia. Unachotakiwa kufanya na kuthink critically the whole saga na kisha utapata khabari yake.

Kikwebo.
 
Kwa hiyo hayo mapandikizi yenu yaliyohamia kwenu jana tusemeje?
 
Nilisoma na kufatilia taarifa hiyo pamoja na wachangiaji katika post ya Ndugu Ben Saanane, na hakika hitimisho lake dhahiri lilibeba uzito na taarifa ambazo hata waliowatuma hao mamluki walipatwa na kibaridi baada ya mkakati huo kuvuja. Napendekeza Press Conference fupi kumpongeza Kamanda na Mwanaharakati Ben Saanane.
 
Na karibuni Ben Saanane atahamia CCM. Mtakuja kujadili humuhumu.weka hii katika kumbukumbu zako.

Hata kama atahamia ccm ni haki yake kisheria ila la msingi amekisaidia cdm kutambua waliotumwa na ccm/Cuf kukiharibu cdm. matokeo yake azimio lao halikufanikiwa
 
Historia ya nchi hii itakuwa very kind kwa Bena Saanane. Amefanya kazi kubwa kuepusha Tanzania kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Kitendo cha CCM kutumia vijana wasio na mwelekeo kuharibu cha kikuu cha upinzani, kilitaka kuuwa kabisa uwepo wa siasa za vyama vingi.

It is such a shame kwamba CCM hawaonekani kujikitita kwenye hoja/sera badala yake wanapandikiza mamaluki kwenye vyama vya upinzani. Hivi hawajifunzi huko wanakuzunguka kila siku? Hawaoni wenzao wakikesha kuchambua sera za wapinzani wao badala ya kutumia mamaluki? Siasa za aibu kweli hizi!
 
mafisadi PAPA ya CCM Yanalia kilio cha kusaga meno!!!!..yamebaki njia panda baada ya kuwafichua mapandikizi yao.Hapa imejionyesha ni namna gani usivyo cheap kuongeka...hapa nakupa saluti
 
Historia ya nchi hii itakuwa very kind kwa Bena Saanane. Amefanya kazi kubwa kuepusha Tanzania kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Kitendo cha CCM kutumia vijana wasio na mwelekeo kuharibu cha kikuu cha upinzani, kilitaka kuuwa kabisa uwepo wa siasa za vyama vingi.

It is such a shame kwamba CCM hawaonekani kujikitita kwenye hoja/sera badala yake wanapandikiza mamaluki kwenye vyama vya upinzani. Hivi hawajifunzi huko wanakuzunguka kila siku? Hawaoni wenzao wakikesha kuchambua sera za wapinzani wao badala ya kutumia mamaluki? Siasa za aibu kweli hizi!

Umeandika kwa hisia kubwa mkuu
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom