Bei ya vifurushi vya Internet leo trh 11/02/2018

Bei ya vifurushi vya Internet leo trh 11/02/2018

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,706
Reaction score
21,857
Hii ni bei ya vifurushi vya internet kwa mitandao ya simu ya Vodacom, TIGO, Halotel na AIRTEL kwa gharama ya shilingi 500 kwa siku ya leo trh 11/02/2020.
Kwa shilingi 500 utapata
MB150 (AIRTEL)
MB70 (TIGO)
MB70 (vodacom)
MB 100 (Halotel).
Maoni yangu.
Haya makampuni ya simu yanatengeneza faida kubwa sana kwenye miamala ya simu,yana uwezo mkubwa sana wa kujiendesha kwa faida kwa biashara moja tu ya huduma ya kifedha achilia mbali faida inayotengeneza kwa huduma nyingine kama voice.
Kwa wastani mtanzania ananunua data MB 90 kwa shilingi 500.
MB 90 ni kiasi kidogo sana ambacho hutakiwi hata kwa bahati mbaya ukafungua GIF au kupita YouTube kwa bahati mbaya.
Kampuni za simu acheni tamaa ya kutengeneza faida kubwa,tunajua mnaweza kutupa bure hizo data,sisi hatutaki bure tunataka kununua angalau MB 500 kwa jero.
 
Labda kama sijaelewa mada, ila mbona zinapatikana MB1000 kwa sh 1000, Airtel na Voda, Tigo kuna cha video/youtube only MB1000 kwa buku.
 
Labda kama sijaelewa mada, ila mbona zinapatikana MB1000 kwa sh 1000, Airtel na Voda, Tigo kuna cha video/youtube only MB1000 kwa buku.
Mkuu, labda unazungumzia vifurushi vya wanachuo cz nje ya hapo ni majanga. Tunaibiwa sana watanzania. Ila kwa kuwa tumezoea kukaa kimya, wacha waendelee kutupiga mpka siku tutakapoamua kusema inatosha.
 
Anzisheni kampeni siku moja watanzania wote msinunue data kuwashinikiza kubadili hivyo vifurushi.

makampuni hayo huwa yanasikiliza kama wote mtaongea kwa kauli moja.

Hakuna taasisi shirika wala kampuni inayoweza kushinda mbele ya nguvu ya wengi yenye kauli moja
 
Mleta mada ingependa ufahamu kuwa kwa sasa
Voice Call haina dili tena kama INTERNET
Na bado siku zijazo INTERNET BUNDLE itazidi kupanda saaana
Leo kujiunga VOICE CALL ya 500 unapata dakika zaidi ya 50
Lkn bando mia5 Mb 90
Kwanza hapa Kwetu TZ ni bei rahisi saaana jaribu kuulizia kwa majirani zetu Uganda huko bando hazishikiki Uganda sh1000 unapata MB20
Tukienda Nchi za MIDDLE East ndio balaa DIRHAM 100 unapata 1GB
Dirham 100 ni sawa na 50.000 Tshs, ndio maana huko makwao wanatumia INTERNET KWA KUPITIA WIFI TU
Ukiwa sehem hakuna WIFE Free hapo haupo ONLINE ktk Maswala ya INTERNET

Ningeshauri tu watanzania wenzangu tuacheni tabia za kujilizaliza hovyo pasipo na sababu za msingi[emoji1321]

Wahenga walishamaliza kwa kusema
“UKIMWONA ALIE JUU YAKO UTAKUFURU KWA MUNGU,NA UKIMWONA ALIEKUWA CHINI YAKO UTASHUKURU KWA MUNGU”[emoji1321]
 
Mitandao yote Tanzania ni wezi tu sema watumia mitandao hatuna namna!
Unaposema wezi basi tambua umeisema na serikali yako! haya makampuni yanasimamiwa na serikali kupitia Tcra,hivyo serikali pia itakuwa imebaliki wizi huo unaousema nje na hapo lbd serikali imewapa mamlaka makampuni kujipangia kiasi cha huduma husika.
tunatakiwa tulalamikie Tcra.
 
Back
Top Bottom