Bei ya vifaa vya ujenzi inapaa kila kukicha

wiseman734

Senior Member
Apr 29, 2018
137
210
Serikali itusaidie sisi wananchi wa kipato cha chini tunapoelekea tunashindwa hata kujenga, bei za vifaa vya ujenzi inapaa kila uchao, yaani leo hii bei ya mfuko wa cement ni elfu 17 hapa kibaha mjini, nondo mm 12 zinauzwa sh 21000/=
Je ni hawa wenye maduka wamejipangia bei!? Mh raisi tunaomba utupie macho huku maana sisi wananchi wako tunashindwa kumudu
 
Bei ya vitu sio kwamba inapangwa na wenye maduka au mh raisi....ni uchumi mbovu hera haina dhamani na uzalishaji uko chini na ghari, kwahiyo usitegemee raisi kupanga bei ya vifaa, ya sukali elimshinda tena vibaya sembuse hiyo ya vifaa vya ujenzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Komaeni nazo tuuuu mbona Pande za Kigoma, Musoma, Sumbawanga, Mpanda hizo bei za cement elfu 20 zishazoeleka na watu wanajenga.
 
Inategemea na maeneo ndugu yangu bei ya cement

Kwa mfano mim jana nimetoka kununua cement kwa elf 14500 ila chaa ajabu Duka la mtaa huo huo wanauza cement 15000 mpaka 16000 elf

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sarakasi Zimeanza Watu Wanahamisha Magoli
Kama Wakati Wa Sukari Na Mafuta Ya Kula
Honourable Minister Mwijage Upo Wapi Sasa
😂🤣😃
Tupe Swager Za Hadidu Za Rejea
 
Kama bei inafaa tumia fursa. Fungua duka la vifaa vya ujenzi na wewe
 
Serikali itusaidie sisi wananchi wa kipato cha chini tunapoelekea tunashindwa hata kujenga, bei za vifaa vya ujenzi inapaa kila uchao, yaani leo hii bei ya mfuko wa cement ni elfu 17 hapa kibaha mjini, nondo mm 12 zinauzwa sh 21000/=
Je ni hawa wenye maduka wamejipangia bei!? Mh raisi tunaomba utupie macho huku maana sisi wananchi wako tunashindwa kumudu
Ni matokeo ya uchumi kukua kwa kasi.
 
Bei ya vifaa vya ujenzi ipo juu sasa
Hasahasa nondo,saruji na gpsam kwamtindo huu watu wataishia nyumba za kupanga kila siku bei inaongezeka
 
Back
Top Bottom