GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 5,070
- 6,774
Hata kama anauza dalali, bado bei ya ndani haina maslahi makubwa kwa mkulima.Anaeuza mahindi nje ya nchi sio mkulima!!
Hata kama anauza dalali, bado bei ya ndani haina maslahi makubwa kwa mkulima.Anaeuza mahindi nje ya nchi sio mkulima!!
Unajua bei ya sukari kwa sasa?
Ni Tsh 2,950.
Tatizo wabongo tumezoea lawama. Serikali ilipopiga marufuku mahindi kuuzwa nje ya nchi watu walilalamika.Natoa tu angalizo kwa katibu wa idara ya uchumi ya chama changu CCM, huku mtaani bei ya Unga wa Ugali ( Sembe na Dona) ni kati ya sh 1500 hadi 1700 kwa kilo.
Ikumbukwe kuwa mahindi yamevunwa juzikati tu sasa ikifika February 2020 sijui hali itakuwaje?
Serikali itoe ruzuku kwa wakulima wa mahindi ili kuwasaidia na kumpa nafuu mwananchi wa kawaida.
Watanzania Ugali ndio mkate wetu wa kila siku
Maendeleo hayana vyama!
Kama mahindi yalipatikana kwa wingi msimu uliopita na wakulima wana ziada, mwelekeo ni kuuza nje ya nchi kwa bei ya juu zaidi ya ile ya ndani!.
Wakulima wamechagua kuuza nje ya nchi na hivyo kunufaika kimapato, kama utapenda kununua mahindi ya mkulima ni lazima uyanunue kwa bei ya nje ya nchi.
Suruhisho ni kununua mazao mbadala kama mchele viazi na mtama, Au kuwazuia wakulima wasiuze mahindi nje ya nchi.
Arawaaa!... Soma kwa makini bandiko langu uone kama ulichoandika hapo juu kina tofauti na nilichoandika mimi, anzia mstari wa kwanza tu.... 😳 😳Uwazie kuuza nje ili wapate hasara?
Limeni nyinyi muuze bei rahisi.
Mimi nilidhani ni mtu mkubwa na cheo chake kwenye chama cha CCM kumbe ni mngangaa njaa tu. Hiyo ni pesa ndogo sana, tena napenda tununue unga wa sembe kilo moja 5,000 ili wakulima nao wafaidike. Kilimo ni kazi ngumu sana kwahiyo acha nao wapate faida.Kweli wewe huelewi!