Bei ya unga wa Sembe yapanda, Serikali iingilie kati

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,597
141,413
pic+unga.jpg

Natoa tu angalizo kwa katibu wa idara ya uchumi ya chama changu CCM, huku mtaani bei ya Unga wa Ugali ( Sembe na Dona) ni kati ya sh 1500 hadi 1700 kwa kilo.

Ikumbukwe kuwa mahindi yamevunwa juzikati tu sasa ikifika February 2020 sijui hali itakuwaje?

Serikali itoe ruzuku kwa wakulima wa mahindi ili kuwasaidia na kumpa nafuu mwananchi wa kawaida.

Watanzania Ugali ndio mkate wetu wa kila siku

Maendeleo hayana vyama!
 
Labda mimi ndio sielewi..hivi katibu wa idara ya uchumi wa CCM anahusikaje na bei za mahindi..mbona kila mtu hii awamu anajiona ana mamlaka jamani
 
Inasemwa kuwa socialist economy is a shortage economy. CCM ni chama cha kisocalist. Kwenye mambo wanaoweza kupiga mpunga kama afya na elimu wameruhusu ebepari lakini kilimo wameendelea kukiendesha kijamaa.
As long as kilimo chetu tunaendesha kijamaa basi njaa, bei kubwa na ukosefu wa chakula vinatuhusu siku zote.
 
Wadau,

Huku kwetu nilikuwa ninanunua unga kiroba cha kilo 5 kwa Tsh. 5,000.

Jana nimeenda kununua sehemu ileile, kiroba kinauzwa Tsh. 8,000.

Hivi bei ya unga imepanda huku kwangu tu au nchi nzima? Si tumeambiwa kuwa tunayo mahindi ya kutosha hadi tunataka kuuza nje? Tunaelekea wapi katika hali ya maisha haya magumu, halafu unga, chakula pekee cha kukimbilia masikini kinapanda hivi?

Inabidi nifanye utafiti, maduka yote hapa mtaani bei imepanda.

Kilo moja ilikuwa inauzwa 1,000 sasa wanauza 1,800, bei sawa na mchele.
 
Hujasema upo wapi, ila unga umepanda. Mbeya nilikuwa nanunua kwa 5000 kilo tano ila saiv ni elfu 7.
 
Nilikuwa nanunua 25kg kwa 19,000/= ila wiki iliyopita nimenunua kwa 33,000/= Dsm.
 
Wakati mahindi yameshuka bei wakulima wanalia na Kula hasara hatukuona watu wanalia kwa ajili yao Leo acha wapate faida Mungu wao kawasikia mara hii.KUIMBA KUPOKEZANA.
 
Kama mahindi yalipatikana kwa wingi msimu uliopita na wakulima wana ziada, mwelekeo ni kuuza nje ya nchi kwa bei ya juu zaidi ya ile ya ndani!.

Wakulima wamechagua kuuza nje ya nchi na hivyo kunufaika kimapato, kama utapenda kununua mahindi ya mkulima ni lazima uyanunue kwa bei ya nje ya nchi.

Suruhisho ni kununua mazao mbadala kama mchele viazi na mtama, Au kuwazuia wakulima wasiuze mahindi nje ya nchi.
 
Yapande Zaid ili mkulima anufaike naye ...mbna mbolea ikipanda hamuanzishi nyuzi za kulalamika humu msengerema ww
 
Kama mahindi yalipatikana kwa wingi msimu uliopita na wakulima wana ziada, mwelekeo ni kuuza nje ya nchi kwa bei ya juu zaidi ya ile ya ndani!.

Wakulima wamechagua kuuza nje ya nchi na hivyo kunufaika kimapato, kama utapenda kununua mahindi ya mkulima ni lazima uyanunue kwa bei ya nje ya nchi.

Suruhisho ni kununua mazao mbadala kama mchele viazi na mtama, Au kuwazuia wakulima wasiuze mahindi nje ya nchi.
Anaeuza mahindi nje ya nchi sio mkulima!!
 
Back
Top Bottom