Bei ya Soda!

Ernie

JF-Expert Member
Aug 3, 2010
217
23
Jamani hebu tukumbushane! Mnakumbuka Soda bei ya chini kabisa mlinunua bei gani? ukweli ni kwamba mimi nilinunua kwa shillingi taslimu ya Kitanzania 7 mwaka 1986, Kinondoni kwa Sheikh Hassan ndio duka pekee lilikuwa karibu na Home
 
Nyie wote bado madogo sana mimi nilinunua soda kwa senti 70 mwaka gani sijui nishasahau.
 
Nyie wote bado madogo sana mimi nilinunua soda kwa senti 70 mwaka gani sijui nishasahau.

Teh teh teh teh

Japo sio ya kucheka imenilazimu kucheka.

Nakumbuka wakati nasoma Primary, Ada ya mwaka mzima ilikuwa Sh. 100. Lakini cha ajabu kuna mwaka eti nilirudishwa nyumbani sijalipa ada, Sh. 100? nikikumbuka ninachofanyia Sh. 100 sasa hivi na nilivyorudishwa nyumbani kwa kukosa mia hiyo hiyo enzi nasoma, nasikitika sana jinsi maisha yalivyopanda.
 
Wewe kumbe mdogo du!! hiyo miaka ya 80 sasa mimi baba yangu alinipa Tshs moja kulipia karo ya shule kipindi kile kwa wazungu maana mshahara alikuwa anapata Tshs 130 alikuwa boss hapo na nilirudishwa kwa hiyo shilingi moja soda zilikuwa zinauzwa sent 5.bye chagua Dr. Slaa sasa uone mabadiliko kipindi kle uchumi ulikuwa juu sema wasomi hamna sasa soda inauzwa bei ya sawa na dola moja? haaaaaaa!!! CHADEMA NDIO JIBU SAHIHI LA UKOMBOZI WA INJI HII
 
Teh teh teh teh

Japo sio ya kucheka imenilazimu kucheka.

Nakumbuka wakati nasoma Primary, Ada ya mwaka mzima ilikuwa Sh. 100. Lakini cha ajabu kuna mwaka eti nilirudishwa nyumbani sijalipa ada, Sh. 100? nikikumbuka ninachofanyia Sh. 100 sasa hivi na nilivyorudishwa nyumbani kwa kukosa mia hiyo hiyo enzi nasoma, nasikitika sana jinsi maisha yalivyopanda.
Shs 100 ya siku hizi imechakachuliwa sana. ya wakati ule kwanza ilikuwa ni noti. tena hapo unahesabu noti za sh. kumi kumi zikifika kumi moja unakunjia
 
Nakumbuka enzi izo unanunua muhogo wa kukaanga aka chips dume kwa tsh moja.
Nenda leo uone mziki wake
 
Kwa mwendo huu wa shillingi kuporomoka na huyu mkwere asiendua hata uchumi, tutaanza kwenda dukani kununu unga na mafuta ya taa na briefcase :A S angry:
 
shilingi yetu tano miaka hiyo ilikuwa sawa na $1 (ndiyo likazaliwa jina la dala dala maana nauli ilikuwa ni shilingi tano) Shilingi 20 yetu ilikuwa ni sawa na pound 1 ya UK ndiyo likazaliwa jina la pound kwa shilingi 20.
 
Wakati nasoma UDSM miaka ya mwanzo ya 80 soda ilikuwa sh. 1, kama nakumbuka vizuri. Wakati huo USD ilikuwa ni sh. tano za Kitanzania, na mabasi ya binafsi yaliporuhusiwa kubeba abiria Dar, yalikuwa yanatoza sh. tano na ndio neno dala dala likatokea hapo maana wapiga debe walikuwa wanasema 'panda hapa, dala dala tu'!
 
Hela imeshuka thamani sana mjombangu aliniambia mwaka 71 alinunua Toyota pickup mpya kwa 15,000/- mwaka 86 alinunua nyingine kwa 750,000/- nenda sasa ushangae bei yake.
 
Wakati nasoma UDSM miaka ya mwanzo ya 80 soda ilikuwa sh. 1, kama nakumbuka vizuri. Wakati huo USD ilikuwa ni sh. tano za Kitanzania, na mabasi ya binafsi yaliporuhusiwa kubeba abiria Dar, yalikuwa yanatoza sh. tano na ndio neno dala dala likatokea hapo maana wapiga debe walikuwa wanasema 'panda hapa, dala dala tu'!

duh, basi maisha yalikuwa magumu sana. hapo kwenye red ina maana nauli ya daladala ilikuwa dola moja kwa safari moja? basi kama ni kweli, usafiri jijini dar ulikuwa ghali pengine kuliko popote duniani!!

sasa nitakosea nikisema kuwa kwa kulipa daldala sh. 300/- sawa na senti 20 (1/5 ya dola) maisha sasa ni nafuu zaidi (ceteris paribus) nitakuwa nimekosea??
 
Back
Top Bottom