Bei ya mafuta katika soko la Dunia imeshuka, Ewura shusheni bei | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei ya mafuta katika soko la Dunia imeshuka, Ewura shusheni bei

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MPadmire, Mar 20, 2011.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Ukisoma katika CNN utaona kuwa bei ya mafuta katika soko la Dunia imeshuka tangu ijumaa.

  SOMA HAPA - SOURCE

  Sasa EWURA ifanye kazi kwa haki, bei imeshuka katika soko la Dunia na sasa ishuke hapa Tanzania.

  Tunajua vibosile wenye biashara za mafuta ni wazito serikalini na wabunge. Tafadhali Serikali na wabunge wa CHAMA TWAWALA, punguzeni kuwanyonya wananchi.

  Kuna mgeni mmoja kutoka South America Chile alisema wananchi wa kule ni masikini kama Tanzania na matajiri kule ni wachache ila akasema hali ni tofauti na Tanzania.

  Alisema kule Chile Matajiri wa kule wanafanya biashara na wanasaidia masikini kwa maana hata hivyo nchi yao haina rasilimali.

  Ila akasema hapa Tanzania nchi ina rasilimali nyingi ila wananchi ni masikini, pia akasema matajiri wa Tanzania wanawanyonya au kuwaibia (ufisadi) wananchi masikini.

  Akasema hii inashangaza sana na wala haingii akilini, ni akili ya kawaida au ni nini.

  Mie nilikubali maneno aliyosema ila nilisikitika na kuona aibu

  Sasa why bei ya mafuta ikipanda wenye biashara za mafuta wanapandisha chap chap hata kama walikuwa na stock while ikishuka wanachelewa kushusha?
   
Loading...