Hello Wana JF wenye uchungu.
Naomba niweke wazi kwanza sipingani na hoja zenu.Ila najaribu kusema nachojua.
Wakati Barrick wanaanzisha mgodi wao wa Kahama waliipa tanzani asilimia 15 ya hisa za company(mgodi) tena bure(free).Mwaka 2005 tanzania yenyewe ikawa zirudisha asilimia hizo kwenye mgodi.
Just imagine..ila kama unakumbukua vyema tanzania ilisha sema yenyewe haifanyo biashara..na dhahabu ni biashara vile tena soko lao liko New york Stock Exchange.Yenyewe inasema inakusanya kodi tu.
Sasa kama 15% walizirudisha hamsini wangeweza ku manage kweli?
Asilimia 50 mwanzijua....pesa mingi sana sio kwamba ni kitu lele mama tu.Kama wananunua Track za kuja kubebe mchanga kwa milioni 500 moja unajua tanzania inatakiwa kuchangia ngapi hapo kwa track hilo?Sio mwekezaji tu atakuwa analeta hayo magari sie tumelala tu.
Kuwa share holder si mchezo....lazima kuwe na pesa....kama viwanda vya nguo tumeshidwa kuendesha itawezekana mgodi?Mashimo yanayo chimbwa kwa ajiri tu ya utafiti,shimo moja linaweza cost badget ya wizara moja selikarini.Na uliza mashimo mangapi yanachibwa...kwa mwaka ni mashimo zaidi ya 600(200M)deep.
Wanajui Biashara na hisa pamoja na kuwa shareholder wanaweza eleza vyema.
Wizarani kwenyewe tukizungumzia katibu mkuu wa wizara ya madini...hajui hata site(mgodi)unajengwaje...upeo mdogo wa kuelewa.Unazungumza na katibu mkuu,au mkaguzi wa madini..unaona kabisa hajui kitu kama vile anafanya Homework.
Kinacho toke serikarini ni kuwa most of information zinakuwa ni siri kubwa migodi inalipa kodi zote ikiwa ni pamoja na Mrahaba(Royality),PAYE(Pay as you Earn),Na zile milioni 250 za kila wilaya...nani anajua haya?Vimefichwa ili wasije ulizwa baadae hizi kodi zinakwenda wapi?
Asubuhi njema.