BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Tanzania imengia mkataba na Barrick ili kuiruhusu kampuni hiyo kuchimba dhahabu. Barrick imeingia mkataba huo kwa niaba ya shareholders wake wakiwemo watu binafsi na makampuni mbali mbali ulimwenguni. Wakati bei ya dhayabu 'inandelea kupaa' katika soko la dunia jana ilifikia $900 kwa ounce moja na kuongeza profit ya kampuni hiyo ambayo pia inawatajirisha shareholders wa kampuni hiyo, Tanzania hainufaiki na chochote kutokana na ongezeko hilo la bei ya dhahabu katika soko la dunia. Na hadi hii leo baadhi ya mikataba hiyo iliyosainiwa awamu ya fisadi Mkapa bado ni siri kubwa. Wakati tunasaini mkataba na Barrick bei ya dhahabu iliyowekwa inasemekana ilikuwa $238 ambayo sasa hivi imeshaongezeka mara tatu zaidi.
Thanks kwa Watanzania wenye uchungu wa nchi yao walioamua kuvujisha mkataba wa Buzwagi au vinginevyo na mkataba huo ungekuwa bado ni siri kali. Katika recommendations zitakazotolewa na kamati ya madini inabidi hii ya Tanzania kupewa 5% au zaidi ya ownership ya Barrick iwe moja ya recommendations hizo na kuongeza royalties kutoka 3% tunayopata sasa pamoja na kulipa kodi ili tuwe tunanufaika kila wakati bei ya dhahabu inapoongezeka.
Kuna wanauchumi wanadai kwamba kama uchumi wa Marekani ukiendelea kusuasua na currency yao kuendelea kuwa dhaifu kwa muda mrefu basi bei ya dhahabu inaweza kufikia hata $2,000 per ounce. Wakati ni huu tusikubali rasilimali zetu ziendelee kuwatajirisha wageni.