Behind the curtain: September 11

S

shiite

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Messages
270
Points
250
S

shiite

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2016
270 250
kila neno ninalofikiri kulitoa naona halifai. Labda niseme tu, Shikamoo The Bold!! Fikiria kuandika vitabu, uweke kama riwaya ili kuepusha wafitini na wenye roho mbaya wa nchi hii kukudisturbalize. Jazakharah khair!!
 
Slowly

Slowly

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Messages
2,372
Points
2,000
Slowly

Slowly

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2016
2,372 2,000
Hili swala la september 11 lina wajuaji wengi sana...hasa wenye ngozi nyeusi hujifanya wanalijua sana....mtu anakrupuka tu anacopy copy na kupaste vitu toka mtandaoni...haya mambo nenda VATICAN ndo utayaelewa...maskini Osama aliwekwa chambo bila kujua effect yake...kumbe watu wana mipango yao
 
Habibu B. Anga

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined
May 7, 2013
Messages
6,433
Points
2,000
Habibu B. Anga

Habibu B. Anga

Verified Member
Joined May 7, 2013
6,433 2,000
kila neno ninalofikiri kulitoa naona halifai. Labda niseme tu, Shikamoo The Bold!! Fikiria kuandika vitabu, uweke kama riwaya ili kuepusha wafitini na wenye roho mbaya wa nchi hii kukudisturbalize. Jazakharah khair!!
Shukrani sana mkuu!

Tuko pamoja sana..
 
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
38,063
Points
2,000
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
38,063 2,000
Hii story umemiss kitu kikubwa mno

nimeshangaa jinsi ambavyo umekikosa hiko kitu

hebu tafuta links wikispooks na site zingine

uhusika wa israel kwenye tukio hili hujaugusa kabisa

hebu google dancing arabs on 9/11...

halafu kamisheni yote ya kuchunguza matukio ya september 11 iliundwa
na jews watupu wengine wakimiliki uraia wa Israel na USA..

na kuhusu jews waliokufa WTC ..walikufa wachache mno

wale ambao hawajui kiyahudi...kuna app ya kiyahudi iliyo warn wasiende

hadi mbunge mmoja black nae alionywa asiende new york na rafiki zake wayahudi..'
 
N

nsekwa

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2015
Messages
910
Points
1,000
N

nsekwa

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2015
910 1,000
Mkuu The bold naomba kujua kuhusu huyu Afisa aliyezama na MV Bukoba Bwana kama alikuwa na comnection yeyote na shambulizi hili. Na kazi zake huyu jamaa zilikuwa nini?

Abu Ubaidah al-Banshiri
 
Kibwebwe

Kibwebwe

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2012
Messages
809
Points
225
Kibwebwe

Kibwebwe

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2012
809 225
BEHIND THE CURTAIN: SEPTEMBER 11

View attachment 471418


Siku ya Jumanne, tare 11 mwezi September mwaka 2001 majira ya saa 2 na dakika 46 asubuhi mpaka saa 4 na dakika 28 asubuhi lilifanyika shambulio kubwa na baya zaidi kuwahi kutokea na kufanywa na adui katika ardhi ya nchi ya Marekani.

Majira ya saa 2 na dakika 46, ndege aina ya Boeing 767-223ER (A.A. Flight 11) iliyosajiliwa kwa namba N334AA, mali ya shirika la American Airlines ambayo iliruka kutoka Boston katika uwanja wa ndege wa Logan International Airport ikitegemewa kutua katika uwanja wa ndege wa Los Angels International Airport ambamo ndani yake kulikuwa na abiria 81 na wafanyakazi 11 ilijibamiza na kulipua jijini New York kwenye jengo la Kaskazini (North Tower) la kituo cha kibiashara cha kimataifa (World Trade Center) jengo ambalo lilikuwa na ghorofa 110.

Dakika chache baadae, ndege nyingine aina ya Boeing 767-222 (U.A Flight 175) iliyosajiliwa kwa namba N6126UA inayomilikiwa na shirika la United Airlines ambayo pia iliruka kutoka Boston katika uwanja wa ndege wa Logan International Airport na ikitegemewa pia ikatue katika uwanja wa ndege wa Los Angeles International Airport ambamo ndani yake ilikuwa na abiria 56 na wafanyakazi 9 ilinibamiza na kujilipua pia jijini New York kwenye jengo la kusini (South Tower) la kituo hicho hicho cha biashara cha kimataifa. Jengo hili pia lilikuwa na ghorofa 110.

Kujibamiza kwa kwa ndege hizi na kulipua majengo haya kulisababisha maghorofa haya kudondoka kabisa (total collapse) na yalisababisasha kudondoka kwa majengo mengine kama vile ghorofa la 7 WTC Tower na maghorofa mengine kumi yaliyomo ndani ya kituo cha cha kimataifa (WTC Complex).

Wakati haya yakitokea jijini New York, ndege nyingine aina ya Boeing 757-223 (A.A. Flight 77) iliyosajiliwa kwa namba N644AA inayomilikiwa na shirika la American Airlines ambayo iliruka kutoka katika uwanja wa ndege wa Washington Dulles International Airport ikitegemewa ikatue kwenye uwanja wa Los Angels International Airport ambmo ndani yake ilikuwa na abiria 58 na wafanyakazi iligeuza njia na kurudi nyuma na kwenda kujibamiza na kulipua jengo la Pentagon, ambalo ndio Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani (US Department of Defense).

Muda huo huo pia, ndege nyingine aina ya Boeing 757-222 (U.A Flight 93) iliyosajiliwa kwa namba N591UA mali ya shirika la United Airlines ambayo iliruka kutoka Newark Intenational Airport ikiwa na abiria 37 na wafanyakazi 7 na ikitegemewa ikatue katika uwanja wa San Fransisco International Airport ilidondoka karibu na eneo la Shanksville, Pennsylvania na inasadikiwa ndege hii ilikuwa njiani kwenda kujibamiza katika Ikulu ya marekani.

Mfululizo wa mashambuluo haya ya siku hii yalikuwa ni tukio baya zaidi katika historia kwa Marekani kushambuliwa na adui katika ardhi yake mwenyewe.

Jumla ya watu 2997 walifariki na watu 6000 wengine walijerehiwa vibaya mno.
Hasara ya kudondoka kwa majengo yote haya na uharibifu wa miundombinu uliotokea thamani yake inafikia shilingi za Kitanzania Trilioni 20.
Lakini tukijumlisha na harasa za mifumo, rasilimali watu, majengo, miundombinu, na kitega uchumi chenyewe cha WTC, hasara hii inafikia jumla ya shilingi za kitanzania Quadrillion 6 (Trilioni elfu sita za kitanzania).Swali la kujiuliza iliwezekana vipi kutekeleza shambulio kubwa kiasi hiki tena kwa mfululizo kwenye nchi ambayo ndio kioo cha dunia kuhusu masuala ya usalama, ujasusi na intelijensi?? Ni nini hasa kilitokea??Ili kulielewa kwa uzuri zaidi suala hili, yatupasa tuangalie jinsi mioango ilivyoanza kupangwa kwa umakini na ustadi mkubwa kwa muda wa miaka mitano.
Yaani ndio kusema kwamba, mipango ya utekelezaji wa tukio hiliilianzawaka 1996.!

Lakini pia, kabla hatujaanza kuitazama jinsi mipango na mikakati ya tukio hili ilivyopangwa, ni vyema kuangalia chimbuko la "mbegu" iliyochochea kuwapa hamasa watu hao kutekeleza tukio hili.

MBEGU INAPANDWA: CIA, Operation Cyclone

Mwaka 1978 yalitokea maoinduzi nchini Afghanistan yaliyomuweka madarakani Rais Nur Mohammad Taraki.

Baada ya Rais Nur Taraki kuchukua madaraka alianzisha Urafiki na nchi ya Urusi ya kipindi hicho ambayo ilikuwa imepania kueneza Ukomunisti ulimwenguni.

Hii ilipelekea December 5, mwaka huo 1978 Rais Taraki kusaini makubaliano ya "Urafiki" wa miaka 25 kati ya Urusi na Afghanistan.

Hii ikipelekea Rais Taraki kuanzisha sera Kikomunisti ambazo zilikuwa hazikubaliki katika jamii ya Afghanistan.

Mfano, Taraki akaondoa sheria iliyokuwa inaruhusu wazazi kumchagulia mchumba binti yao pia akaaruhusu wanawake kushiriki siasa.

Pamoja na hili akaanzisha Mapinduzi ya Sera ya ardhi ambayo ilidhibiti kiasi cha ardhi kinachoweza kumilikiwa na familia moja.
Hii ilisababisha zaidi ya hekari milioni 1.6 kupokonywa kutoka kwa familia mbali mbali na kurudishwa serikali.

Pamoja na hilo Rais Taraki akaanzisha kampeni ya kuwafunga gerezani wapinzani wake wa kisiasa nje ya chama chake na hata ndani ya chama chake cha People's Democratic Party of Afghanistan.
Inakadiriwa kwamba zaidi ya wapinzani 27,000 waliuwawa kipindi cha utawala wa Rais Taraki.

Hii ikapelekea Rais Taraki kuchukiwa mno ndani ya Afghanistan na mwishoni akapinduliwa kutoka madarakani na rafiki yake aliyeitwa Hazifizullah Amin.

Baada ya Amin kuingia madarakani ilikurudisha imani ya wananchi akaanza kuondoa sera za ukomunisti akaanza kukata mawasiliano na Urusi.

Kutokana na mahusiano ya Afghanistan na Urusi kuzorota mno hii ikapelekea December 24, 1979 Majeshi ya Urusi yakaivamia Afghanistan na kumuua Rais Amin na kumuweka kibaraka wao aliteitwa Babrak Karmal.

Baada ya Karmal kuwa rais akaanza kurejesha tena sera za Ukomunisti na kujenga tena ukaribu na Urusi.
Hasira za wananchi zikawaka zaidi.

Kwanza walipinga uvamizi wa Urusi, lakini pia walipinga Sera za ukomunisti nchini mwao.

View attachment 471420
Majeshi ya Urusi yakiigia Afghanistan Desembe 24, 1979.

Ndipo hapa vikaanza kuibuka vikundi vya upiganaji vya Mujahedeen kila kona ya nchi.

Vikundi hivi viliungana mwaka 1981 na kuunda umoja uliojulikana kama Islamic Unity of Afghanistan Mujahedeen.
Vikundi hivi vilipambana kila kona ya nchi kupinga uwepo wa majeshi ya Urusi nchini Afghanistan na uwepo wa vibaraka wa Urusi serikalini.

Ikumbukwe kwamba kipindi hiki ndicho kipindi ambacho 'Vita Baridi' kati Urusi na Marekani ilikuwa imepamba moto.

Ndipo hapa ambapo Marekani kwa kushirikiana na nchi nyingine za Kiarabu wakaanzisha mkakati wa kuvisaidia vikundi hivi vya Mujahedeen kupambana na majeshi ya Urusi nchini Afghanistan.

Mkakati huu ulisimamiwa na Shirika la ujasusi la CIA, na mkakati huu ulijulikana rasmi kama OPERATION CYCLONE

Operation Cyclone ilikuwa na malengo makuu mawili;

Moja:- kuwapatia mafunzo waoiganaji wa Mujahedeen.
Mafunzo hawa yalikuwa yanafanyika nchini Pakistan kwa kushirikiana na jeshi la nchi hiyo na Idara yake ya Ujasusi (ISI - Inter Service Intelligence).
Jumla ya wapiganaji wa Mujahedeen 100,000 walipatiwa mafunzo ya kijeshi kuanzia mwaka 1978 mpaka 1992.

Mbili:- kutoa msaada wa kifedha kwa vikundi vya Mujahedeen.
Msaada huu ulikuwa katika mtindo wa fedha taslimu na silaha.
Pia msaada huu ulitolewa katika awamu mbili.
Miaka sita ya kwanza (1981-1987) marekani ilitoa jumla silaha na fedha taslimu zenye thamani ya Dola bilioni 3.2.

Katika awamu ya pili (1987-1993) Marekani waliwapa vikundi vya Mujahedeen jumla ya fedha silaha na fedha tasilimu vyenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 4.2

Nchi ya Saudi Arabia nayo ikaweka ahadi ya ya "kumatch a dollar for a dollar" yaani kama marekani akitoa dola moja nao wanatoa moja, wakitoa bilioni nao wanatoa bilioni.

Kwahiyo, Mujahedeen nchini Afghanistan walikuwa na rasilimaki fedha za kutosha, silaha za kutosha na mafunzo adhimu kabisa ya kijeshi. Hivyo vita ilikuwa kali kweli kweli.

View attachment 471421
Wapiganaji wa Mujahedeen nchini Afghanistani, 1981.

Wakati huo huo,

Nchini Suadi Arabia, kulikuwa na familia maarufu ya Bilionea ambaye ndiye alikuwa raia tajiri zaidi asiyekuwa mwanafamilia ya kifalme (wealthiest non-royal citizen)! Bilionea huyu aliitwa Mohammad bin Awad bin Laden na alikuwa ndiye mmiliki wa kampuni ya SAUDI BINLADEN GROUP, kampuni kubwa zaidi ya Ujenzi nchini Saudi Arabia.

Bilionea huyu aliuwa amezaa na mke wake wa kumi Hamida al-Attas, kijana aliyeitwa Usama bin Mohammad bin Awad bin Laden ambaye alizaliwa tarehw 10, March 1957.

Kijana huyu alisomea fani ya Uchumi na utawala wa biashara katika chuo kikuu cha King Abdulaziz University. (Japokuwa zipo taarifa zinazoonyesha kuwa huenda alisomea Uhandisi (civil engeneering)).

Wanafunzi wenzake wanaeleza kuwa alikuwa ni kijana mwenye bidii ya masomo na alikuwa muumini mtiifu wa Kiislamu dhehebu la Sunni.

Inaelezwa kuwa alitumia muda mwingi sana chuoni kujisomea Qur'an na kufanya kazi za kujitolea.
Pia inaelezwa kuwa alianza kuwa shabiki wa Klabu ya mpira ya Arsenal tangu akiwa hapa chuoni.
Pia alipendelea sana kutunga ushahiri na kusoma vitabu vya fasihi.

Kijana huyu alivutiwa na vugu vugu la Wapiganaji wa Mujahedeen lililokuwa linaendelea nchini Afghanistan.

Kijana huyu alishawishika mno na mahubiri ya mwanatheolojia wa kiislamu mwenye asili ya Plaestina aliyeitwa Abdullah Azzam ambaye mpaka sasa ndiye anafahamika kama "Baba Wa Jihad Duniani" (Father of Global Jihad).

Kijana huyu akawasiliana na Azzam, na Azzam akamshawishi na kumsaidia ajiunge na Mujahedin.

Hivyo baada ya kumaliza chuo (wengine wanasema aliondoka miezi michache kabla ya kuhitimu) alielekea moja kwa moja Afghanistan kujiunga na wapiganaji wa Mujahedeen kupinga uwepo wa majeshi ya Urusi kwenye Ardhi ya Afghanistan.

View attachment 471422
Osama bin Laden (aliyezungushiwa duara)na wanafamilia wenzake wa Bilionea Mohammad bin Awad walipotembelea London kwa mapumziko miaka ya 1970s

Akiwa nchini Afghanistan, yeye Osama pamoja na Azzam ambaye sasa alikuwa ndiye "mentor" wake wakaanzisha Muktab al-khidamat (MAK) au kwa jina lingine ilijulikana kama Afghan Services Bureau.

Kazi kuu ya MAK ilikuwa ni kueneza propaganda na kushawishi vijana kutoka nchi za Kiarabu wajiunge na Mujahedeen nchini Afghanistan kupigana na majeshi ya Urusi.
Si hivyo tu, bali pia MAK ilikuwa na jukumu la kukusanya michango kutoka kwa watu mbali mbali duniani waliokuwa wanaunga mkono harakati za Mujahedeen.

Osama akatumia kiasi kikubwa cha utajiri wake aliorithi kutoka kwa baba yake (bilionea Muhammad bin Awad bin Laden alifariki mwaka 1967 kwa ajali ya ndege), akatumia kiasi kikubwa cha fedha kuwalipia nauli, tiketi za ndege na malazi vijana wote waliokuwa wanatoka kila pembe ya dunia kujiunga na Mujahedeen.

Kujitoa kwake huku, pamoja na uwezo wake mkubwa wa kujieleza na ushawishi, kukamjengea heshima kubwa sana kwa wapiganaji wa vikundi vya Mujahedeen.

Vita ikaendelea kati ya Mujahedeen wakiungwa mkono na marekani dhidi ya majeshi ya uvamizi ya Urusi.


Baadae Urusi ikaja kuona kwamba vita hii ilikuwa na gharama kubwa kwao. Kwanza ilikuwa gharama ya kuharibu mahusiano yao ya Kidiplomasia duniani na pia vita iligharimu kiasi kikubwa cha rasilimali fedha na rasilimali watu.

Hivyo basi kiongozi wa Urusi wa kipindi hicho, Mikhail Gorbachev akaamuru majeshi kurejea nyumbani na kikosi cha mwisho cha Urusi kiliondoka Afghanistan tareahe 15, February 1989.


Baada ya majeshi ya Urusi kuondoka, vikundi vya Mujahedeen walibakiwa na wapiganaji wengi na silaha nyingi za kutosha lakini hawakuwa na adui wa kupigana naye.

Hivyo wakaanza "kutengeneza" maadui wapya.
Wakanzisha vugu vugu la kudai kukomeshwa kwa ukandamizaji wa Israel dhidi ya Palestina na kudai "Uhuru" wa eneo la Kashmir.
Pia wakaweka msimamo kuwa hawataki uwepo wa wanajeshi wa nchi za magharibi katika nchi yoyote ya Kiarabu.

Vugu vugu hili ndilo likasababisha kuanza uadui kati yao vikundi vya Mujahedeen na mshirika wao Marekani.

Ndipo hapa ambapo viongozi kadhaa wa vikundi vya Mujahedeen wakafanya kikao cha siri ili kupanga mikakati mipya, mbinu mpya na falsafa mpya ya kumkabili adui yao mpya, Marekani na nchi za magharibi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa mlinzi binafsi wa Osama Kikao hiki cha siri kubwa kilifanyika Tarehe 11 August 1988 na kiliudhuriwa na viongozi wakuu wa Mujahedeen akiwemo Ayman al-Zawahiri, Abdullah Azzam na Osama bin Laden.

Kupitia kikao hiki, kikundi kipya kikaundwa na Osama bin Laden akachaguliwa kuwa Amiri Mkuu wa kikundi (General Emir).

Ni siku hii ya kikao hiki cha tarehe 11 August 1988 ndipo ambapo kilizaliwa rasmi kikundi cha kigaidi cha AL QA'IDA, na ni ndipo hapa ambapo kizaza cha matukio ya kutisha kikaanza

Usikose SEHEMU YA PILI ambayo tutaona namna ambavyo Osama Bin Laden alitoa Fa’twa ya kwanza na Fa’twa ya pili (na impact zake).

Pia tutaangalia namna ambavyo mikakati ya tukio la September 11 ilipangwa kuanzia mwaka 1996.

BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA PILI


BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA TATU


BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA 4, 5 & 6

BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA 7 & 8

BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA 9

BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA 10

BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA 11


BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA 12


The Bold
 
Nyamai

Nyamai

Member
Joined
Jun 12, 2017
Messages
54
Points
125
Nyamai

Nyamai

Member
Joined Jun 12, 2017
54 125
The bold jaribu kuiacha akili yako ifanye kazi kwa uhuru zaidi.
Tukio la September eleven halikuasisiwa na alqaida km ulivyoaminisha na hao mabwenyenye.

Na ndo nyie hadi leo mnaamini ni kweli USA walikwenda mwezini, ni nyinyi hadi Leo ndio mnaamini kwamba USA walimuua Osama .

Tafuta ukweli ili uwe huru nasi kila kitu utakachoambiwa na wao moja kwa moja uamini.

Sent from my GT-I9152P using JamiiForums mobile app
 
D

Devon sawa

Senior Member
Joined
Apr 30, 2017
Messages
165
Points
225
D

Devon sawa

Senior Member
Joined Apr 30, 2017
165 225
Ntarudi

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
elmagnifico

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Messages
7,918
Points
2,000
elmagnifico

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2011
7,918 2,000
Mkuu The bold naomba kujua kuhusu huyu Afisa aliyezama na MV Bukoba Bwana kama alikuwa na comnection yeyote na shambulizi hili. Na kazi zake huyu jamaa zilikuwa nini?

Abu Ubaidah al-Banshiri
Duh mkuu Mv Bukoba imezama mwaka 1996 wakati tukio aliloongelea the bold la 2001
 

Forum statistics

Threads 1,336,221
Members 512,562
Posts 32,531,147
Top