Behind the curtain: September 11

Bush did it.ile ilikua ni controlled demolition.

Kuna kipindi jeshi tena ili lipate sababu za kuivamia Cuba walitaka kuandaa shambulio ndani a marekani ili wawasingizie wa Cuba.JFK alikataa hii.Mwanzoni watu walisema ni conspiracy theory lakini badae through declassified intel ikajulikana ilikua kweli.
Yeah ,ni kama ile ya Amsterdam bombing ambayo walikuja kushikana uchawi wenyewe kwa wenyewe,ni false flag terror attack ikiwa imezungukwa na mysteries nyingi ambazo kwetu ni ngumu kidogo kung'amua ila wenyewe wanaopanga wanatulamba vichogo.
 
Mwanzo mwa post ya kwanza, Mkuu The Bold, umeeleza kuwa 11 September attack in US, lilikuwa shambulio kubwa kabisa kuwahi kufanywa nchini humo. Je. Lile shambulio la Pearl Harbour lilikuwa jepesi kiasi hicho?
 
Hizi ni akili za mbuzi sasa wee jamaa unataka mwenzako atembee kwenye mawazo yako wewe?

Lete yako kwa namna ujuavyo na si kutaka mwenzako alete unavyotaka wewe...simple
 
AL QAIDA WANAANZA "KUPASHA" MISULI KUJIANDAA NA 9/11

Asante sana Mkuu...kwa simuliza Mubashara kabisa!!!



Shambulizi katika Balozi za Marekani Afrika Mashariki

Siku chache baada ya kutoka kwa fa'twa ya Osama bin Laden, washirika wa All Qaida kutoka kikundi cha kigaidi cha Misri (Egyptian Islamic Jihad) kwa muongozo wa Osama bin Laden binafsi na Al Qaida wakaanza kupanga mkakati wa kuanza kuwaonyesha "advertise" ya uwezo wao wa kufanya mashanbulio na kuwalipiza kisasi.

Mwezi May 1988, Sheikh Ahmed Salim Swedan alipanga chumba katika Jengo la kipato cha kati jijini Nairobi.

Wakati huo huo, bwana mmoja anayejukiakana kama K.K Mohamed naye alipanga nyumba namba 213 iliyoko maeneo ya Ilala jijini Dar es Salaam, nyumba hii ikiwa takribani kilomita sita pekee kutoka Ubalozi wa Marekani.

Nyumba hizi mbili za Dar na Nairobi zilitumiaka kama vituo vya kutengenezea mabomu yatakayo tumika kulilipua balozi za Marekani.

Mabomu haya yaliutengenezwa chini ya uangalizi wa "mtaalamu" Mohammed Odeah.

Bomu la nairobi liliundwa katika mtindo ambao ulitumia zaidi TNT.

TNT (Trinitrotoluene) ni tumawe mawe fulani hivi twenye rangi ya manjano ambayo ni Chemical Compound - C6H2(NO2)3CH3.

TNT huwa inatumiaka kwenye "chemical synthesis" kama "reagent".

Pia hutumika kwenye process za kikemia kutengeneza "charge transfer salts"

Licha ya hivyo kampaundi hii unaewezo mkubwa wa kulipuka na hii ndio sababu hata hutumika kama kipimo cha kupimia uwezo wa vitu vingine kulipuka (standard measure of explosives)

Sasa jijini Nairobi, magaidi hawa wakatumia cylinder mia tano za TNT, pamoja na unga wa Aluminum kuunda mabomu yao ambayo waliyahifadhi katika masanduku ya mbao.

Jijini Dar es salaam Bomu lake lilikuwa tofauti kidogo.

Hili bomu la Dar lilitengenezwa kwa kutumia hiyo hiyo TNT, lakini cylinder zake ziliuungwa kwenye mitungi kumi na tano ya Oxygen na "gas canisters".

Pia kwenye steji ya mwisgo ya upakiaji kwenye gari waliweka na viroba vinne vya mbolea yenye kiwango kikubwa cha Ammonium Nitrate.


Baada ya mabomu kukamilika, magaidi wa Nairobi wakanunua gari aina ya Toyota Dyna na kupakia karibia maboksi 20 yenye milipuko.

Huku Dar, wao walinunua gari aina ya Toyota Atlas, yenye jokofu (refrigeration truck) na wakajaza milipuko waliyotengeneza kama wenzao wa Nairobi.

Siku ya August 7, 1998 siku ambayo ilikuwa ni maadhimisho ya miaka 8 tangu vikosi vya Marekani kuwasili nchini Saudi Arabia, magari haya yenye milipuko yakiendeshwa na kwenda kupaki kwenye balozi za Marekani jijini Nairobi na Dar es salaam.

Mnamo saa nne na nusu asubuhi, mabomu ya Nairobi yakalipuka.

Dakika kumi baadae, yaani saa nne na dakika arobaini asubuhi, bomu mabomu ya Dar es salaam nayo yakalipuka.

Mlipuko wa Nairobi ukisababisha vifo vya watu 213 na kujerehi wengine 4000, huku mlipuko wa Dar ukisababisha vifo vya watu 11 na kujeruhi watu 85 wengine.

Kicha ya vifo hivi vingi, lakini ni Wamarekani 12 pekee walio fariki kutokana na milipuko hii.
Kati ya hao wamarekani 12 waliofariki walikuwemo, makachero wawili wa CIA waliokuwepo Ubalozini Nairobi, kulikuwa na Sajenti mmoja wa US Marine, julikuwa na Marine mwingine aliyekuwa kama mlinzi ubalozini, pia kulikuwa na sajenti wa jeshi (US Army).


View attachment 473330
Eneo la tukio la mlipuko ubalozini.



Tukio hili ndilo kikifanya kwa mara ya kwanza FBI ikamuingiza Osama katika Orodha ya Most Wanted.

Likaanzushwa "vugu vugu" la kuwasaka waliohusika kutekeleza tukio hili la kulipua balozi.

Lakini bila kujua, wakati vyombo vyote vya usalama na ujasusi nchini Marekani vikihahah na kukuna kichwa kuwatafuta wahusika wa mashambulio haya kwenye balozi wao, ndipo kipindi hiki hiki nchini Afghanistan Osama bin Laden anapokea ugeni muhimj wa kikundi cha wanafunzi wa kiarabu wanaosoma nchini Ujerumani... Vijana ambao Osama alikuja baadae kuwatumia kuwapandikiza nchini Marekani na kutekeleza tukio la September 11.



View attachment 473329
Ahmed Ghailani kijana wa kitanzania aliyehusiuka katika shambulio la Balozi ya Marekani.




The Hamburg Cell

Katika jamii ya Ujasusi nchini kuna "kijiwe" cha ugaidi cha wanafunzi ambacho kilikuwa kwenye mitaa ya Hamburg nchini Ujerumani na wamekibati,a jina kama "The Hamburg Cell"

Wanachama muhimu zaidi katika kijiwe hiki walikuwa ni, *Mohamed Atta, Ramzi bin al-Shibh na Marwan al-Shehhi.* hawa watatu walikuwa na uhusika mkubwa katika tukio la September 11.

Lakini pia kijiwe hiki kilikuwa na wanachama wengine kama vile, Said Bahaji, Zakariya Essabar, Mounir el-Mossadeq na Abdelghani Mzoudi.

Kijiwe hiki kina historia ndefu mpaka kufikia kuwepo kwake.


Historia ya kijiwe hiki inaanzia kwa kufika kwa Mohamed Atta nchini Ujerumani.


Mohammed Atta; Kijana pekee wa kiume katika familia ya mwanasheria mahiri nchini Misri Bw. Mohamed el-Amir Awd el-Sayed Atta, alizaliwa September 1 mwaka 1968 katiaka eneo la Kafr el-Sheikh kwenye mkoa wa Delta ya Nile.

Mohamed Atta alikuwa na bahati, kwani alizaliwa kwenye familia yenye kipato kizuri kabisa baba yake akiwa ni mwanasheria mahiri, pia mama yake mzazi alikuwa anatokea kwenye familia ya kitajiri inayojihusisha na kilimo kikubwa.
Atta pia alikuwa na dada wawili wakubwa na wote walikuwa wasomi wa hali ya juu na wenye mafanikio. Dada yake mmoja alikuwa ni Daktari Bingwa na mwingine akiwa ni Profesa wa Chuo kikuu.

Baba yake Atta anajulikana kwa kuwa muisilamu mwenye kuifuata dini mpaka kipindi kingine anazidisha anafanya mambo ambayo labda yanaweza kuonekana sio ya lazima kidini. Hii ilipelekea hata familia yao isiwe karibu na upande wa ndugu wa Mama yake wakiokuwa nabutajiri mkubwa. Wengi wa ndugu hao hawakupendezwa na misimamo ya kidini ya baba yake Atta.

Akiwa na umri wa miaka 10 familia yao ilihamia jijini Cairo ambapo baba yake alimpiga marufuku kujichanganya na watoto wengine wa majirani.

Hivyo Atta alitumia muda wake mwingi wa utotoni akiwa mpweke amejifungia ndani akijisomea.
Lakini hii pia ilimpa faida kwani, alifanikiwa kufaulu vizuri masomo yake na kuchaguliwa kujiunga na Chuo kikuu cha Cairo mwaka 1985 akisomea Uhandisi.

Akiwa katika mwaka wake wa mwisho chuoni, kutokana na kuwa wanafunzi bora kabisa hapo chuo, akaingizwa kusoma programu adhimu kabisa chuoni hapo ya Architecture.
Mwaka 1990 akahitimu chuo.

Baada ya kuhitimi chuo akapata kazi kwa muda katika kituo cha Mipango Miji jijini Cairo (Cairo Urban Development Center) akifanta kazi ya 'Architectural Planning and Building Designing'.

Baadae mwaka 1991 akajiunga na Kituo cha Goethe Institute ili kujifunza kijerumani.

Mwaka 1992 akapata nafasi ya kusoma Shahada ya Uzamiri katika 'Urban Planning' kwenye chuo kikuu cha Hamburg.

Akiwa chuoni hapa kusomea shahada hiyo mwangalizi wake wa masomo (Supervisor) alikuwa anaitwa Dittmar Machule ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Idara.

Bw. Dmittar anamuelezea Atta kama mwanafunzi mwenye akiki sana lakini alikuwa na misimamo mikali ya kiitikadi.

Kwa mfano; anaeleza kuwa kwenye maongezi ya kawaida (mara chache sana, inaelezwa kuwa Atta hakuwa muongeaji, unaweza kuishi naye nyumba moja wiki nzima asikusemeshe hata neno wala, hata salamu.. Mwanzoni alipoingia Ujerumani aliwahi kufukuzwa kwenye nyumba ya wanandoa fulani waliokuwa walimu wa sekondari kutokana na tabia yake ya ukimya uliopitiliza mpaka kuudhi).. Sasa kwenye maongezi hayo ya bahati nasibh, inaelezwa kuwa Atta alikuwa nanipinga sana Sera ya Marekani kuhusu Mashariki ya Kati.

Si hivyo tu bali pia alipinga Utawala wa 'kifamilia' wa Hussein Mubarak nchini Misri na aliichukia serikali kutokana na kampeni yake ya kutokomeza kikundi cha kisiasa cha Muslim Brotherhood.

Atta alikuwa anapinga hata namna ambavyo miji katika nchi za kiarabu ilovyokuwa "inaharibiwa" kwa kujengwa kwenye mtindo wa kuiga umagharibi.

Bw. Dittmar anaeleza kwa mfano, Atta alichefukwa sana na namna ambavyo maghorofa yalikuwa yakijengwa kimagharibi jijini Cairo kila uchwao.

Hata katika 'thesis' yake, Atta alitafiti ujenzi wa zamani wa mji wa kihistoria wa Aleppo nchini Syria na akaonyesha namna ambavyo mji huo unaharibiwa kwa "usasa"



View attachment 473325
Mohammed Atta akiwa na wanafunzi wenzake wa Hamburg University katikasiku zake za kwanza mara baada ya kufika Ujerumani.


Akiwa bado mwanafunzi chuoni, baadae Mohamed Atta akaanza kuhudhuria Ibada katika Msikiti wa Kisunni wa Al-Quds.!

Msikiti huu unajulikana kwa kuwa na mahubiri yenye chuki na hasira dhidi ya mataifa ya magharibi.

Akiwa msikitini hapa ndipo akakutana na Ahmed Maklat, Muonir El Motassadeq na Ramzi bin al-Shibh.

Mwanzoni waliunda urafiki kwa kuunda "kikundi cha maombi" cha pamoja, lakini baadae umoja huu ndio ukaja kugeuka na kuwa kijiwe cha kigaidi maarufu cha "Hamburg Cell".


Mara kadhaa Atta ilimbidi kuhahirisha masomo kwa sababubz kiidini nyingine zikiwa zinaeleweka ila nyingine zilikuwa na mashaka makubwa.

Mfano tarhe 31 october 1995 Atta allihairisha masomo kwa muda na kwenda Hijja, Makka. Hii ilieleweka na ilikuwa na msingi.

Takribani miezi kumi na nane baadae, yaani June 1997 Atta akapotea tena chuoni.
Supervisor wake anaeleza kuwa hii ilisababisha kuwa nyuma ya muda wa kuwasilisha thesis yake (alifanikiwa kuwasilisha thesis mwanzoni mwa mwaka 1999 na kufanya utetezi mwezi August 1999) Dittmar aalipowasiliana nae ili kujua mahali alipo wasiliana nae ili kujua alipo alimueleza kuwa yuko safarini kwenda tena Hiija.

Hii ilitia mashaka kidogo ukizingatia ni miezi 18 tu nyuma alitoka kwenye Hijja.

Atta alikaa kwa muda mrefu huko alipoenda na kurejea mwaka 1998.

Aliporejea alikuwa amebadilika sana kiahiba! Kwanza alikuwa amevuga ndevu ndefu sana na alikuwa mtu 'serious' kuzidi mwanzo.
Pia akaeleza kuwa amepoteza passport yake hivyo hii imembidi kutafuta passport nyingine. Hii ni moja ya mbinu inayotumiwa na watu kutaka kuficha sehemu aliyokwenda.

Kwahiyo kutokana na kwanza kukaa muda mrefu huko alikoenda tofauti na muda halisi wa Hijja, na pia kuficha passport yake kwa makusudi.. Inaaminika kuwa Mohammed Atta alienda kwenye kambi za Al Qaida nchini Afghanistan.


View attachment 473327
Muonekano wa Mtaa a Marienstrasse mjini Hamburg, mtaa ambao kulikuwa na apartment ya "Humbarg Cell"



Kijiwe cha Hamburg kinazidi kupata ushawishi

Baada ya Atta, Ramzi na Shehhi kuwa marafiki walioshibana, hatimaye siku ya November 1 mwaka 1998 wote watatu wakapanga 'apartment' moja katika mtaa wa MarienstraBe jijini Hamburg.

Apartment yao ikaja kujipatia umaarufu sana kwa wanafunzi wengi wa kiarabu wenye misimamo mikali waliokuwa Hamburg.
Ilifikia kipindi mpaka karibia wanafunzi 21 wa kiarabu walikuwa wameandikisha apartment hiyo kama "address" yao rasmi kwenye nyaraka mbali mbali.

Kulikuwa na ratiba ya mijadala kwa wiki mara tatu au nne na mijadala hii yote ilihusu Marekani na Israel na jinsi wanavyogandamiza waislamu.

Kadiri muda ulivyoenda, kijiwe hiki kilianza kuwavutia hata "magaidi" halisi.

Inaelezwa kwamba hata Khalid Sheikh Mohammed aliwahi kukitembekea kijiwe hiki mara kadhaa kufanya "vetting" kwa ajili ya mpango wa shambulio la kiihistoria,alio uwasilisha kwa Osama, ingawa hawa vijana wenyewe hawakujua nia ya KSM kuwatembelea.



SEHEMU YA NNE JUMAMOSI..



The Bold
 
Umeanza tabia ya SHIGONGO na magazeti yake ya ijumaa...humalizi stori...ili uendeleee kula muda wetu..kwani ni TAMTHILIA HII?. Licha ya kutusaidia kwa kuyakusanya matukio pamoja..ila sasa umeanza kula muda wetu..au tupe link /translation source tusome wenyewe...Au sasa tutanza kuona kama unaboa....pia hii inaonyesha umeanza kuishiwa matukio...unaanza kuketa series. Hii mbinu hiache itakupunguzia wafuasi. Maliza stori ..ulete ingine maana ziko nyingi duniani...HATA HIVYO NAKUSHUKURU kwa kutenga muda wako !.


The bold na Shigongo wapi na wapi Conductor.

Mi naona usiwasemee watu wengine coz naamini wapo wanaosoma hivyo hivyo nusu nusu na wanaelewa(mimi nikiwa mmoja wapo) so ni vizuri tu kama ni ngumu kwako na wengine (kama wapo) m/usubiri iishe then m/utaisoma kwa uzuri.

Hizi kauli za kusema kama ameishiwa sijui nini na atapoteza wafuasi labda wewe tu. Kuhusu link ingia Google au You tube kule nadhan itakuwepo (kama ni rahis kiasi hicho).
 
Wadau wengine acheni mambo ya kiseng*

Bonge la post alaf una quote kuandika vijimaneno viwili vitatu... Mnatukera tuaotumia simu.

Wengine acheni u hater, kama unaona stori hazikufai sio lazima usome, pia kama una haraka lipia ada kajiunge kwenye group, ukishindwa kabisa komaa na GOOGLE,

msimkatishe tamaa mtu anayepoteza muda wake kukonaa kuandika post ndeefu na zenye mtiririko mzuri kwa mambo yenu ya kiduwanzi..

Big up The bold
 
Wadau wengine acheni mambo ya kiseng*

Bonge la post alaf una quote kuandika vijimaneno viwili vitatu... Mnatukera tuaotumia simu.

Wengine acheni u hater, kama unaona stori hazikufai sio lazima usome, pia kama una haraka lipia ada kajiunge kwenye group, ukishindwa kabisa komaa na GOOGLE,

msimkatishe tamaa mtu anayepoteza muda wake kukonaa kuandika post ndeefu na zenye mtiririko mzuri kwa mambo yenu ya kiduwanzi..

Big up The bold
Umenena mkuu,watu wanaponda huku wanasoma,wanajazba ya kusubilia

Kuwa mvumilivu kama buku huna au unasababu zako binafsi za kuto kwenda whatsapp


Tukomae tuu kibishi bishi humu humu

By the way hv the bold anaumwa nn??

Kapepeluka kwenye vipepeo
 
uko wapi the bold...mwenzio haka kaseries natongozea demu,na anajua mimi ndiye mtunzi,sasa mkuu nilimuambia leo nakutetea sehemu ya nne,tangu asubuhi ananikumbusha najifanya niko bize na kikao,sasa siku inaisha mkuu the bold tafadhali nifanyie wepesi tafadhali kaka.
 
uko wapi the bold...mwenzio haka kaseries natongozea demu,na anajua mimi ndiye mtunzi,sasa mkuu nilimuambia leo nakutetea sehemu ya nne,tangu asubuhi ananikumbusha najifanya niko bize na kikao,sasa siku inaisha mkuu the bold tafadhali nifanyie wepesi tafadhali kaka.
Hahahahhhaaaa kaka zima simu kwanza, the bold atafanya utoswe
 
Mkuu The Bold hapo juu umesema sheikh Salim swedan alikodi chumba nairobi mwaka 1988.nadhani utakuwa umekosea mwaka.itakuwa unamaanisha 1998 mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom