[HASHTAG]#TZA[/HASHTAG] “Beef kati yangu na Rais Putin imesababisha nikose Urais” – Hillary Clinton.......>>>"Beef kati yangu na Rais Putin imesababisha nikose Urais" - Hillary Clinton - millardayo.comduh hio source!
ndo maana putin huwa anaongoza kuwa the world most influential person...sometime wao wenyewe wanampa kick kijinga kabisa...how come putin yuko kwao huko tena nchi yake ilikuwa busy na syria halafu wanamlaumu eti anaingilia uchaguzi wao....Huyu bibi kachanganyikiwa baada ya kushindwa sasa anatafuta mchawi.
Hataki kukubali kuwa alikuwa ha connect na watu wa kwenye majimbo yaliyokuwa ya muhimu ili kumwezesha kupata ushindi.
Sasa anamlaumu Putin kwani huyo Putin alimwongezea kura Trump kwenye hizo mashine za kupigia kura?
Such a sore loser....blaming everybody else but herself when in fact she was a terrible candidate herself.
2008 Democrats wenzie walimkataa na 2016 Wamarekani wamemkataa.
Aende zake huko akalee wajukuu zake sasa.
ndo maana putin huwa anaongoza kuwa the world most influential person...sometime wao wenyewe wanampa kick kijinga kabisa...how come putin yuko kwao huko tena nchi yake ilikuwa busy na syria halafu wanamlaumu eti anaingilia uchaguzi wao....
CIA, FBI bila aibu eti ni kweli urusi ilihusika....kama ilihusika haya mashirika yalikuwa wapi?...kazi yao ni nini mpaka taifa adui kama urusi linawachagulia kiongozi....kama hawana lengo jingine na wanachoongelea ni kweli bassi ni aibu kubwa kwa marekani.....matokeo yake hata nchi za ulaya zilizokuwa zinafikiri kuwa marekani ndiko usalama wao ulipo zitaanza kusita kuamini hivyo tena
Nilimuangalia Obama alipokua anahutubia taifa juzi kuhusiana na hili suala la udukuzi. Nilichokigundua ni kwamba jamaa wamesambaratika vibaya sana. Obama huyu wa sasa si yule aliyekua akiongea hapo kabla. Hakuonyesha kabisa ile sifa yake ya orator, zaidi ni kama anaendelea kushangazwa na namna Trump anavyoipangilia serikali yake, Obama anaonyeshwa kuduwazwa sana na Trump.Yaani wanampa kiki na kumpandisha chati bure tu.
Utadhani Putin alienda kujaza kura za Trump hizo mashine za kupigia kura.
Hahahaaaaa.
Yalaaaaaaaa mkuu hapo kwenye red ndo umenivunja mbavu kabisa. hahahahahhahhahhah hadi conte jaman?Kwa maana hiyo RUSSIA ndilo taifa kubwa... Marekani na wafuasi wenu kimya ni zamu ya putin kufanya yake ni hatari.
Putin
|
Kim
|
Durtete
|
magufuli
|
Paul kagame
|
Antonio conte
|
Costa
|
Trump
Dunia hii si sehemu salama tena.
tunajifunza we cheusiWengi tumekuwa mashabiki wa siasa za Ulaya na Marekani bila kuzifahamu kiundani. Tunaendeshwa kwa mihemuko na matukio yatokeao huko Ulaya na marekani. Kwa wenzetu Exhibition katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijeshi ni kawaida sana bila kusababisha migongano miongoni mwao, ila sisi huku ndio tunaoreact as if mambo yao yanatugusa kwanjia ya moja kwa moja.
Kwa haya tunayofanya tunaonesha kuwa wamefanikiwa kututawala katika nyanja zote mpaka kiakili.
Kilicho sababisha ashindwe urais pamoja na sabab zote na zingine lkn kikubwa ni jinsia yake...Beef kati yangu na Rais Putin imesababisha nikose Urais" - Hillary Clinton
Baada ya kimya kirefu tangu ashindwe kupata nafasi ya Urais nchini Marekani, hatimaye aliyekuwa mgombea nafasi hiyo Hillary Clinton amejitokeza na kudai kwamba ugomvi binafsi uliokuwepo kati yake na Rais Vladmir Putin wa Urusi umechangia sana kumkosesha nafasi hiyo muhimu.
Clinton ameeleza hayo wakati huu kukiwa na mzozo mpya kati ya serikali ya Marekani na Urusi juu ya kuwepo taarifa za kiintelijensia kwamba Rais Putin alidhamini kitengo cha udukuzi ili kiingilie na kuvuruga uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, na tayari Rais Obama ametoa agizo la kufanyika uchunguzi na kusema kuwa serikali yake itachukua hatua kali dhidi ya Urusi.
Katika mahajiano aliyofanya siku ya Alhamisi usiku, Clinton amesema kuwa Rais Putin alikuwa akijaribu hata kuzivuruga kampeni zake ilimradi tu kumharibia njia yake kutokana na “Ugomvi Binafsi.”
“Putin alikuwa akinilaumu kwa kuwaambia ukweli raia wa Urusi kuwa walidhulumiwa haki yao, vitu ambavyo vinafanana na kile alichoamua kukifanya yeye kwa kuingia uchaguzi wetu na kuharibu kila kitu kama njia ya kulipa kisasi,” amesema Hillary.
Clinton amefananisha kilichotokea kwake ni kile kilichowapata Warusi kwenye uchaguzi uliovurugwa na usio wa kidemokrasia kwenye bunge la Urusi mwaka 2011.
Mgombea huyo amesema ana uhakika angeshinda uchaguzi kama tu Putin asingeingilia na kuvuruga pia aliendeleza lawama zake kwa Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la nchi hiyo FBI, James Comey kwa kushupalia taarifa za uchunguzi wa email zake binafsi kuwa zilipunguza kura zake.
Chanzo Millard Ayo.