Beef kati yangu na Rais Putin imesababisha nikose Urais" - Hillary Clinton

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
1,333
Beef kati yangu na Rais Putin imesababisha nikose Urais" - Hillary Clinton

Baada ya kimya kirefu tangu ashindwe kupata nafasi ya Urais nchini Marekani, hatimaye aliyekuwa mgombea nafasi hiyo Hillary Clinton amejitokeza na kudai kwamba ugomvi binafsi uliokuwepo kati yake na Rais Vladmir Putin wa Urusi umechangia sana kumkosesha nafasi hiyo muhimu.

Clinton ameeleza hayo wakati huu kukiwa na mzozo mpya kati ya serikali ya Marekani na Urusi juu ya kuwepo taarifa za kiintelijensia kwamba Rais Putin alidhamini kitengo cha udukuzi ili kiingilie na kuvuruga uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, na tayari Rais Obama ametoa agizo la kufanyika uchunguzi na kusema kuwa serikali yake itachukua hatua kali dhidi ya Urusi.

Katika mahajiano aliyofanya siku ya Alhamisi usiku, Clinton amesema kuwa Rais Putin alikuwa akijaribu hata kuzivuruga kampeni zake ilimradi tu kumharibia njia yake kutokana na “Ugomvi Binafsi.”

“Putin alikuwa akinilaumu kwa kuwaambia ukweli raia wa Urusi kuwa walidhulumiwa haki yao, vitu ambavyo vinafanana na kile alichoamua kukifanya yeye kwa kuingia uchaguzi wetu na kuharibu kila kitu kama njia ya kulipa kisasi,” amesema Hillary.

Clinton amefananisha kilichotokea kwake ni kile kilichowapata Warusi kwenye uchaguzi uliovurugwa na usio wa kidemokrasia kwenye bunge la Urusi mwaka 2011.

Mgombea huyo amesema ana uhakika angeshinda uchaguzi kama tu Putin asingeingilia na kuvuruga pia aliendeleza lawama zake kwa Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la nchi hiyo FBI, James Comey kwa kushupalia taarifa za uchunguzi wa email zake binafsi kuwa zilipunguza kura zake.
Chanzo Millard Ayo.
 
Huyu bibi kachanganyikiwa baada ya kushindwa sasa anatafuta mchawi.

Hataki kukubali kuwa alikuwa ha connect na watu wa kwenye majimbo yaliyokuwa ya muhimu ili kumwezesha kupata ushindi.

Sasa anamlaumu Putin kwani huyo Putin alimwongezea kura Trump kwenye hizo mashine za kupigia kura?

Such a sore loser....blaming everybody else but herself when in fact she was a terrible candidate herself.

2008 Democrats wenzie walimkataa na 2016 Wamarekani wamemkataa.

Aende zake huko akalee wajukuu zake sasa.
 
ndo maana putin huwa anaongoza kuwa the world most influential person...sometime wao wenyewe wanampa kick kijinga kabisa...how come putin yuko kwao huko tena nchi yake ilikuwa busy na syria halafu wanamlaumu eti anaingilia uchaguzi wao....
CIA, FBI bila aibu eti ni kweli urusi ilihusika....kama ilihusika haya mashirika yalikuwa wapi?...kazi yao ni nini mpaka taifa adui kama urusi linawachagulia kiongozi....kama hawana lengo jingine na wanachoongelea ni kweli bassi ni aibu kubwa kwa marekani.....matokeo yake hata nchi za ulaya zilizokuwa zinafikiri kuwa marekani ndiko usalama wao ulipo zitaanza kusita kuamini hivyo tena
 
Yaani wanampa kiki na kumpandisha chati bure tu.

Utadhani Putin alienda kujaza kura za Trump hizo mashine za kupigia kura.

Hahahaaaaa.
 
Aache ujinga mbona cc wengine tupo huku kijijin maisha yanatuchapa bt hatujamlaumu Magu japo ndio chanzo. AKAE KIMYA ALE MAISHA ALIYOJALIWA
 
Yaani wanampa kiki na kumpandisha chati bure tu.

Utadhani Putin alienda kujaza kura za Trump hizo mashine za kupigia kura.

Hahahaaaaa.
Nilimuangalia Obama alipokua anahutubia taifa juzi kuhusiana na hili suala la udukuzi. Nilichokigundua ni kwamba jamaa wamesambaratika vibaya sana. Obama huyu wa sasa si yule aliyekua akiongea hapo kabla. Hakuonyesha kabisa ile sifa yake ya orator, zaidi ni kama anaendelea kushangazwa na namna Trump anavyoipangilia serikali yake, Obama anaonyeshwa kuduwazwa sana na Trump.
Nadhani kuna mambo mengi sana yataibuka soon or later. Demos bado hawajajua jamaa wamkabili namna gani, maana kadri siku zinavyosonga, waliokua na machungu wengi wanaonekana wameshakunywa maji na sasa ni kama wanabadirika na kuwa mashabiki wa Trump. Demos wana kibarua kigumu cha kubadili aina za siasa kwa hivi sasa, maana wameshaamini kwamba wanayemkabili si mwanasiasa.
 
Kama Obama na serikali yaake wameshindwa kumdhibiti Putin ni wazi angeingia madarakani Putin angemuendesha vibaya mno ila pia hasemi mbinu zake chafu alizokuwa anawafanyia wagombea wenzake kupitia chama chake na jinsi alivyotumia media kumhujumu Putin ikiwemo kupewa maswali kabla naa jinsi alivyokuaa akimpandikizzia kashifa kama zile za kudhalilisha wanawake
 
azilaumu wafanyaji wa tafiti kwa kumwaminisha ya kuwa atashinda tena kwa ushindi mnono
 
Wengi tumekuwa mashabiki wa siasa za Ulaya na Marekani bila kuzifahamu kiundani. Tunaendeshwa kwa mihemuko na matukio yatokeao huko Ulaya na marekani. Kwa wenzetu Exhibition katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijeshi ni kawaida sana bila kusababisha migongano miongoni mwao, ila sisi huku ndio tunaoreact as if mambo yao yanatugusa kwanjia ya moja kwa moja.
Kwa haya tunayofanya tunaonesha kuwa wamefanikiwa kututawala katika nyanja zote mpaka kiakili.
 
Kwa maana hiyo RUSSIA ndilo taifa kubwa... Marekani na wafuasi wenu kimya ni zamu ya putin kufanya yake ni hatari.

Putin
|
Kim
|
Durtete
|
magufuli
|
Paul kagame
|
Antonio conte
|

Costa
|
Trump

Dunia hii si sehemu salama tena.
Yalaaaaaaaa mkuu hapo kwenye red ndo umenivunja mbavu kabisa. hahahahahhahhahhah hadi conte jaman?
 
Wengi tumekuwa mashabiki wa siasa za Ulaya na Marekani bila kuzifahamu kiundani. Tunaendeshwa kwa mihemuko na matukio yatokeao huko Ulaya na marekani. Kwa wenzetu Exhibition katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijeshi ni kawaida sana bila kusababisha migongano miongoni mwao, ila sisi huku ndio tunaoreact as if mambo yao yanatugusa kwanjia ya moja kwa moja.
Kwa haya tunayofanya tunaonesha kuwa wamefanikiwa kututawala katika nyanja zote mpaka kiakili.
tunajifunza we cheusi
 
Beef kati yangu na Rais Putin imesababisha nikose Urais" - Hillary Clinton

Baada ya kimya kirefu tangu ashindwe kupata nafasi ya Urais nchini Marekani, hatimaye aliyekuwa mgombea nafasi hiyo Hillary Clinton amejitokeza na kudai kwamba ugomvi binafsi uliokuwepo kati yake na Rais Vladmir Putin wa Urusi umechangia sana kumkosesha nafasi hiyo muhimu.

Clinton ameeleza hayo wakati huu kukiwa na mzozo mpya kati ya serikali ya Marekani na Urusi juu ya kuwepo taarifa za kiintelijensia kwamba Rais Putin alidhamini kitengo cha udukuzi ili kiingilie na kuvuruga uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, na tayari Rais Obama ametoa agizo la kufanyika uchunguzi na kusema kuwa serikali yake itachukua hatua kali dhidi ya Urusi.

Katika mahajiano aliyofanya siku ya Alhamisi usiku, Clinton amesema kuwa Rais Putin alikuwa akijaribu hata kuzivuruga kampeni zake ilimradi tu kumharibia njia yake kutokana na “Ugomvi Binafsi.”

“Putin alikuwa akinilaumu kwa kuwaambia ukweli raia wa Urusi kuwa walidhulumiwa haki yao, vitu ambavyo vinafanana na kile alichoamua kukifanya yeye kwa kuingia uchaguzi wetu na kuharibu kila kitu kama njia ya kulipa kisasi,” amesema Hillary.

Clinton amefananisha kilichotokea kwake ni kile kilichowapata Warusi kwenye uchaguzi uliovurugwa na usio wa kidemokrasia kwenye bunge la Urusi mwaka 2011.

Mgombea huyo amesema ana uhakika angeshinda uchaguzi kama tu Putin asingeingilia na kuvuruga pia aliendeleza lawama zake kwa Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la nchi hiyo FBI, James Comey kwa kushupalia taarifa za uchunguzi wa email zake binafsi kuwa zilipunguza kura zake.
Chanzo Millard Ayo.
Kilicho sababisha ashindwe urais pamoja na sabab zote na zingine lkn kikubwa ni jinsia yake...

Pole yake, ila amejitahidi, USA hawanaga hizo nafasi za majaribio kwenye nafasi kubwa...

Nawaza kwa sauti,
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom