Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,504
- 51,099
Huyu ni mfungwa wa Zamani, aliyekaa Jela kwa miaka 9 kuanzaia miaka ya 1980,s mpaka miaka ya 1990 alipoachiwa kutokana na purukushani za kuvunjika kwa Umoja wa Kisoviet.
----------------------------------------------------------------------------------------------------
Bwana Prigozhin alizaliwa mwaka 1961, na baba wa Kiyahudi katika mji wa St Petersberg. Miaka miwili baadae baba yake akafariki. Prigozhin akaasiliwa (adopted) na baba mwingine wa Kiyahudi. Kwa hiyo Prigozhin akakulia katika familia ya kiyahudi.
Kundi la Wagne lilianzishwa Mwaka 2014 na askari wake wa mwanzo walikuwa ni askari wa zamani wa jeshi la Urusi. Na operseheni zake za awali, zilikuwa katika mikoa ya mashariki mwa Ukraine kwa wakati huo.
Baadae Kundi hilo lilipanua shughuli zake hadi huko Syria na Afrika ikiwemo Libya na Afrika ya kati.
Mwaka 2018 waandishi wa habari waliokuwa wakifanya uchunguzi wa kundi hilo walivamiwa na kuuawa. Kutokana na matendo yake kundi hili limewekwa katika kundi la magaidi na serikali ya Marekani na Prigozhin ni mtafutwa na mamlaka ya Marekani kama Gaidi.
Baada ya kutoka Jela, Prigozhin alifungua mgahawa katika mji wa St Petersberg, mgahawa uliokuwa maarufu sana kwa watu maarufu wa Urusi enzi hizo. Na hata Vladmir Putin mwenyewe alikuwa mhudhuriaji mzuri katika mgahawa huo.
Baadae Prigozhin aliweza kujipenyeza karibu na wakubwa ndani ya serikali ya Urusi na kufanikiwa kuwa anapata tenda kubwa za kusupply vyakula kwa majeshi ya Urusi. Kutokana na business zake hizi ameweza kupata hela ndefu sana.
Pamoja na kuendesha na kusimamia kundi la Wagner , Prigozhin anaendesha kampuni ya Internet Research Agency, kampuni inayolalamikiwa na serikali ya Marekani kuendsha operation zilizovuruga uchaguzi wa marekani mwaka 2014 na kumsaidia Donald Trump kuingia madarakani kwa kumzidi Hillary Clinton.
Sehemu ya taarifa hii imechukuliwa katika mtandao maarufu wa ynetnews.com wa Israel
Unaweza kuisoma kirefu hapa:

Who are you, Yevgeny Prigozhin? Wagner Group's powerful Jewish leader
The former felon-turned-restauranteur-turned-militia chief gained notoriety as 'Putin's chef', responsible not only for keeping the bellies of the Russian president's troops full but also for assisting in the execution of his global military and imperial ambitions
www.ynetnews.com