Beatrice Shelukindo na ya YUDA Iskariote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Beatrice Shelukindo na ya YUDA Iskariote

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ngoshwe, Nov 21, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Baada ya Kumsaliti YESU Masia kwa Vipande 30 vya fedha, Yuda Iskariote aliumia sana moyoni akafikiri ametenda dhambi kuu, akafikia uamuzi wa kurejesha vile vipande vya fedha kwa wakuu wa makuhani na mafarisayo ili damu isiyo na hatia isije ikawamwagika juu yake, baada ya kuona ameshindwa akaishia kujinyonga...

  Mhe. Beatrice Shelukindo (Mbunge wa Kilindi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alipojua yale ambayo yatamfika Mhe. William Mganga Ngeleja na Adam Malima (Wana CCM wenzake) baada ya kutoa taarifa yake, amejikuta akiumia sana moyoni na kujutia uamuzi wake wa kumlipua Jairo. Hivyo, kuamua kurejesha vipande 30 vya fedha kwa kuwataka wabunge na Serikali isimwajibishe Ngeleja kwa kuwa hausiki...

  Mhe, Betrice Shelukingo hakujua haya yote yatatokea??..
   
 2. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kaka hawa wnzetu kufanya maamuzi magumu ni jambo ambalo si rahisi kwao!
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Beatrice alitumiwa na akina Lowassa na Januari Makamba ili Ngeleja atemeshwe mzigo then Januari achukue. Sasa amekumbuka mume wake alivyodhalilishwa Bumbuli na sasa anajaribu kurudisha nyuma gurudumu alilolianzisha, akisahau kwamba hana control tena na hoja ile si yake tena. Mnafiki mkubwa huyu!
   
 4. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Mama mnafki sana pooooooooooooooooh! Mate chini
   
 5. n

  nyandaojiloleli JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Imekula kwake
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  nyie mmefanya maamuzi yapi magumu?
   
 7. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alitaka kuvua gamba alipona wanazingua akarudia kulivaa. Magamba wote vilaza
   
 8. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Alichopaswa kufanya ni kile cha Poncio Pilato (Pontius Pilatus) mbele ya wale makuani, baada ya kuridhika kuwa hakuna sababu za kutosha za kumuunganisha Ngeleja na kashfa ya fedha haramu za Jairo, angenawa mikono mapema kwa kusema kuwa damu ya Ngeleja na Nduguye Adam Malima na iwe juu yetu watanzania, kwa kuwa ametutenda dharau, angetamka wazi kuwa yeye na nyumba yake ya Shellukindo wasihusishwe..lakini alichofanya ni kujitafutia umaarufu wa bei chee (cheap popularity) kwa kujifanya ameweka historia ya kuibua ufisadi kama akina Zitto Kabwe lakini badala yake kaingiwa na hofu ya ghafla kuhusu maisha yake baada ya kujioone kumbe yeye bado ni Magamba na magambani atarejea...japo alidai kuwa "Mungu wake mlinzi yu hai"..alishindwa kumsaidia kutafakari athareio ya unafiki alioutenda kwa watanzania...atajutia maneno yake aliyotaoa kabla na wakati akinchangia mjadala wa Ripoti ya Kamati teule..
   
 9. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Alichokionyesha Beatrice ni mja kati ya zile dalili tatu za mnafiki.
   
 10. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sishangai maana amerithi Unafiki kutoka Chama Chake cha CCM
   
 11. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  She was right! hawa watu hawajui kabisa kinachendelea juu ya fedha, nenda mkoani RC hajui lolote juu ya fedha, nenda wilayani DC hali kadhalika they are just political figure lakini hawajui kinachoendelea juu ya mambo mengine yote.
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Hahahahhaaaaa hakuna kitu kibaya kama kukimbia kivuli chako mwenyewe!!!! Alinikera sana juzi alipogeuka kabisa as if sio yeye! Aliwasha moto kwenye nyumba alimolala! Kaona na yeye anaungua kaona heri ajaribu kuuzima while it is too late
   
Loading...