Beating the Drum on One Side: Confusing the People on Both Sides

Inferiority complex at work, Nyerere alikuwa na nia njema kutokuruhusu hayo mnayoyataka.. Kwanini waislamu kote duniani ndio wanahangaika, eti 'holy war'..kama dini yenu inaweka wazi kwamba asiyekubaliana na uislamu auwawe, sasa huo si udikteta..
 
Wanajamvi,
Mimi haikunipitikia wakati ule kama iko siku ilm ile nilosoma
chuoni yaani madrasa itakuja kunifaa mimi na jamaa zangu.

Hivi sasa kuna watu wamerudi na matusi...

Maalim Haruna alikuwa akisema, "Mtu hatukani ila pale anapokuwa
kahamaki.

Ukiona hivyo basi muache hadi ghadhabu zake zimepoa ndipo
ikiwa unaona ipo haja ukaendelea na mnakasha."

Nimemueleza Lusungo historia ya 1947 - 1954 kilipitika nini katika
maisha ya Abdul kuja kuunda TANU 1954.

Katika kisa hiki nikawaleta wazalendo wawili muhimu katika
kuwaelewa wanasiasa waliokuwapo baada ya WW2 - Chief Kidaha
Makwaia na Julius Nyerere na vipi waliingiliana na Abdul Sykes
katika kutafuta uongozi wa kuwavusha Waafrika kuelekea kuunda
TANU na kudai uhuru.

Sikutegemea matusi na kejeli.
Nilitegemea mnakasha utanoga kwa maswali zaidi...
 
'islam' means 'peace'.where is that peace..penye nia pana njia na penye mwislam asiyejielewa kuna vita..wakristu, wabudha, wapagani n.k ndio wanahubiri na kutenda 'amani'..
 

Mie nimekuuliza swali linakuwa gumu sana kwako kujibu? Kwanza jibu swali langu halafu ulete hayo yako, ndiyo raha ya mnakasha, au unaonaje?

Jee, Mau Mau walipigana na Mjerumani?
 
'islam' means 'peace'.where is that peace..penye nia pana njia na penye mwislam asiyejielewa kuna vita..wakristu, wabudha, wapagani n.k ndio wanahubiri na kutenda 'amani'..

OK tumekusoma.

Jee, Mau Mau walipigana na Wajerumani?
 


Ahsante MS

Ninachokupendea ni kwamba huna jazba na unaelewa nini unafanya...

Unaelewa takwa la MTU na unajitahidi kutimiliza...

Sisi wengine humu hatuingii kwaajili ya Kejeli au matusi tunataka elimu na fafanuzi zitakazoondoa contradictions ktk mind set zetu.

Ahsante kwa muda wako.
 
Lusungo,
Hili jina linanikumbusha marehemu mdogo wangu Ibrahim.

Alikuwa na rafiki yake anaitwa Joseph Lusungo akipiga trumpet
NUTA Jazz miaka ya 1970.

Urafiki wao ulikuwa katika kucheza draft na walikuwa na barza
yao.

Ibrahim alichukua 1st prize best student in Chemistry miaka 3
mfululizo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Lusungo nae pia kesha tangulia mbele ya haki.

Ahsante kwa yote kaka.
 
Tehe! tehe! tehe!
Du! sina mbavu!!!!!
 
OK tuekusoma.

Jee, Mau Mau walipigana na Wajerumani?

Tatizo lililokutokea hivi punde la kuandika tuekusoma badala ya tumekusoma, naam linaweza kua limemtokea Prof Hirji badala ya kuandika Maji Maji akaandika Mau Mau.

Hata Mohamed Said hajishupalia hilo, kwa nini sasa usiende kwenye swali langu
 
Last edited by a moderator:
Mie nimekuuliza swali linakuwa gumu sana kwako kujibu? Kwanza jibu swali langu halafu ulete hayo yako, ndiyo raha ya mnakasha, au unaonaje?

Jee, Mau Mau walipigana na Mjerumani?

Hapana alipigana na Muingereza, sasa zamu yako
 
Mkuu turudi zetu kwa Matola huku hupawezi

Mkuu nafahamu sipawezi ila nahitaji kupaweza ili nijue...

Kutopaweza dawa yake si kukimbia ila kutujitahidi kupaweza...

Sikuingia hapa kukejeli laa... Nimeingia ili nijue na kwa bahati nzuri ndugu MS anaweza mjuvya MTU.
 
Last edited by a moderator:
Kama mwathirika mmojawapo wa hii lugha nimejitahidi kulisoma hili andiko na limenipa mwanga zaidi.
Ubabaishaji umekuwa mwingi Tanzania mpaka wanaibuka waandishi na analysts wababaishaji kati masuala nyeti kabisa ya kitaifa. Na kibaya zaidi wapo waliojipenyeza mpaka kwenye nafasi za kufanya maamuzi wanaowasujudia hawa watafiti wababaishaji na wenye malengo yao maalumu.
Asante sana Prof. Hirji kwa kujariju kurudisha mambo katika mstari.
 
Prof. Karim Hirji ameandika kisomi sana,hajabeba jazba za kidini. Hivi ndivyo namna wasomi wanavyotakiwa kujitofautisha na walalamishi.

As the author of the article being discussed, I would like to make a few important corrections and points:

1. There was an unfortunate typographic error; in haste I wrote Mau Mau instead of Maji Maji. I apologize
for this error on my part.
2. The version of my article on this website is an INCOMPLETE VERSION. THE FINAL SECTION INCLUDING
THE CONCLUSION HAS BEEN CUT OFF. SO THE FORUM MEMBERS HAVE NOT GOT THE FULL STORY. I
HAVE SENT THE FULL VERSION TO THE MODERATOR. PLEASE READ IT.
3. My main aim is not to contest historic details but to expose an erroneous way of thinking.
4. I am not pro-Christian, pro-Muslim, pro-Hindu etc. but simply pro-Tanzania who wishes to see
mutual harmony and tolerance between all religions, creeds, races, ethnicities, etc.
5. As I write in my conclusion, I regard Mohamed Said as a key intellectual voice in our society
who needs to be heard.
6. But if anyone including him promotes flawed views, we should be free to criticize them.
7. Let us discuss important issue affecting our nation in a brotherly sisterly spirit. Otherwise, if we
fight among ourselves on narrow grounds, only the enemies of the nation and exploiters of the
common person will benefit.

Prof. Karim Hirji
 

Mash'kuura yaa ukh'y FF.

Hata mimi naingia wasi wasi na huo U-Profesa wake isije kuwa kama ule wa Maji Marefu.

Mwenye CV yake jamani naomba tafadhwali aiweke hapa. Tusije pata dhunuub kwa dhan'na.

 
Tatizo lililokutokea hivi punde la kuandika tuekusoma badala ya tumekusoma, naam linaweza kua limemtokea Prof Hirji badala ya kuandika Maji Maji akaandika Mau Mau.

Hata Mohamed Said hajishupalia hilo, kwa nini sasa usiende kwenye swali langu

Mau Mau na maji maji na typo ya kukosa kuchapa herufi moja wapi na wapi?

Nataka ujibu wewe, achana na Hirji, hana jipya. Mau Mau walipigana na Mjerumani?
 

Mau Mau walipigana na Mjerumani?
 
mie nimekuuliza swali linakuwa gumu sana kwako kujibu? Kwanza jibu swali langu halafu ulete hayo yako, ndiyo raha ya mnakasha, au unaonaje?

Jee, mau mau walipigana na mjerumani?

na omba msamaha wenu. Haata profesa anaweza kufanya kosa la kitoto. Maana yangu ilikuwa
maji maji lakini kwa haraka niliandika mau mau.
Lakini kosa dogo kimoja kama hilo haliwezi kupindua logic na ukweli wa makala mzima.
Ni wale ambao hawataki kufikiria mambo kwa kiundani ndiyo watayanganganyia makosa madogo
madogo.

Prof. Karim hiri
 
Nani alipigana na Muingereza? hivi hata kuandika sentensi kamili mnashindwa? hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Hahaha we mama nachelea kusema uwezo wako wa kuargue mambo ni mdogo,

kfhirji ameshaomba radhi kwa alichoandika Mau Mau badala ya Maji Maji, ambao hatujashikwa na Dini tukakuambia ni makosa madogo madogo,

Sasa punde tu wewe mwenyewe umekosea badala ya kuandika Tumekusoma, ukaandika tuekusoma.

Mbona Banzi lililopo jichoni kwako inakua ngumu kuliona?

Bado hujajibu Swali langu, nmekuuliza hivi

Mohamed Said anaamini Uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa na Waislamu, Je unakubaliana na hilo.

Nimejibanza Hapa mtaa wa Uhuru karibu na duka la mshihiri huku nikila kashata baada ya kuchoma mahindi kwa muda sasa
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…