BBC Swahili yasema mazingira ya uwekezaji Tanzania ni Magumu, wafungua ofisi Kenya

Naunga mkono hoja Tanzania
Jumatatu ya Juni 5,2023, BBC Swahili imetangaza kuanza msimu wake mpya wa matangazo ya runinga kutokea mjini Nairobi nchini Kenya badala ya London, Uingereza.Mitandaoni mjadala umekuwa ni kwanini studio hizo zisingehamishiwa Tanzania kutokana na uasili na idadi kubwa ya wazungumzaji wa lugha ya kiswahili.

Mwanahabari mtanzania Mubelwa Bandio, anayefanya kazi zake nchini Marekani kwa upande wake anasema mazingira ya kuwekeza na kufanya kazi za uanahabari nchini Tanzania ni magumu na yaliyoandamwa na urasimu mkubwa kulinganisha na jirani zetu Kenya.
kwenye kila kitu kumejaa madude mengi sana siasa majitaka, upumbavu, uzandiki, chuki, kujuana na tutazidi kuwa masikini mpaka dunia inaisha
 
Tanzania hata innovator wa kutuma pesa kwa mitandao kimataifa ya NALA Money, Benjamin Fernandez, licha ya kujulikana mpaka na rais na kuahidiwa ushirikiano na serikali kutoka ngazi za juu kabisa, ameshindwa kufanya kazi kutoka Tanzania, ameanzisha ofisi zake Nairobi.

Namnukuu John Doe aliyenihabarisha leo katika mjadala mwingine hapa JF kuwa:-

"Changamoto alizopita mwanzilishi wa NALA kampuni ya kutuma pesa kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine ilimpelekea mpaka kupeleka makao makuu kuhamishia Kenya. Huu ni mfano halisi wa jambo ulilozungumza hapo juu.

Angalia kituko kuhusu BoT kuna vibali vya aina moja inachukua benki kuu ya Uingereza siku moja kuvipata hivyo hivyo kwa benki kuu ya Marekani, Kenya na Uganda vinachukua siku 10 za kazi pekee. Kwa upande Rwanda na Burudi ni siku 14 ila kwa Tanzania ni miezi 6."

Mwisho wa kunukuu.

Hapo kwenye BOT huwa sielewi wana shida gani, leseni inachukua miezi 6.

Same investor akiwekeza Kenya hiyo miezi 6 anakuwa ameaanza biashara na kurudisha pesa.
 
Jumatatu ya Juni 5,2023, BBC Swahili imetangaza kuanza msimu wake mpya wa matangazo ya runinga kutokea mjini Nairobi nchini Kenya badala ya London, Uingereza.Mitandaoni mjadala umekuwa ni kwanini studio hizo zisingehamishiwa Tanzania kutokana na uasili na idadi kubwa ya wazungumzaji wa lugha ya kiswahili.

Mwanahabari mtanzania Mubelwa Bandio, anayefanya kazi zake nchini Marekani kwa upande wake anasema mazingira ya kuwekeza na kufanya kazi za uanahabari nchini Tanzania ni magumu na yaliyoandamwa na urasimu mkubwa kulinganisha na jirani zetu Kenya.
Aliyesema hayo maneno ni BBC swahili au Mubelwa Bandio????? Huyo Mubelwa anafanya kazi BBC? Au alisema wakati akihojiwa na BBC????
 
Si BBC tu hata CNN, Aljazeera asilimia kubwa huongelea bara la Africa kwa matatizo ya njaa, magonjwa, ugaidi au majanga majanga tu ilihali huko Ulaya panaweza pasiwe na matatizo sawa na Africa lakini wako most obsessive.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Kwani hayapo?

Ethiopia, Sudan, Somalia hazina njaa?

Vita na mapigano yasiyo isha Congo, Sudan, Somalia, Africa ya kati,
Burkina Faso, Chadi,Mali n.k hayapo?

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Hapo kwenye BOT huwa sielewi wana shida gani, leseni inachukua miezi 6.

Same investor akiwekeza Kenya hiyo miezi 6 anakuwa ameaanza biashara na kurudisha pesa.
Tanzania pia tuna kitu naona ni a sense of false "Tanzanian exceptionalism".

Nafikiri ni matokeo ya Ujamaa. Na kiasi fulani kuwa na resources nyingi, kuwa na bahati ya kijiografia etc.

Tunaona nchi yetu ni bora zaidi ya wenzetu na hatuhitaji kushindana nao, kwamba hata tukiwa na tofauti kubwa hivyo ya ease of doing business, bado tutakuwa competitive tu.

Ukweli wa kiuchumi unatuonesha tulivyo delusional.
 
something is wrong with this country, hata kupokea pesa kwa PAYPAL haiwezekani aisee. Kuna kundi la watu wanaoshikilia hii nchi upande wa uchumi linapaswa lisafishwe lote tuanze upya.

sera zote walizojitungia tangu 77 huko zinapaswa zipitiwe upya yaani bado tunaishi maisha ya kizamani sana sababu ya hilo kundi la watu wachache walioshikilia hii nchi na uzee wao.
Mimi Huwa napokelea Kenya na naingiza bongo kwa safaricom bila fee yoyote
 
Back
Top Bottom