BBC NA DOUBLE STANDARD KUHUSU URUSI

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,452
Waziri wa michezo wa urusi Vitaly Mutko, anasema kuwa anaelewa kuwa huenda taifa lake likapigwa faini na shirikisho la soka la bara ulaya kutokana na tabia isiyofaa ya mashabiki wa timu ya taifa hilo.

UEFA, imeanza uchunguzi wa machafuko makali yaliyotokea baada ya mechi ya dimba la EURO kati ya Urusi na Uingereza katika mji wa Marseille nchini Ufaransa.

Baada ya mechi kati ya mataifa hayo mawili, iliwabidi polisi kutumia gesi ya kutoa machozi pamoja na kunyunyuzia maji, ili kusitisha makabiliano hayo katika eneo la bandari mjini Marseille.

160612032628_euro2016_fans_violence_640x360_pa_nocredit.jpg
Image copyrightPA
Image captionMashabiki wa Urusi na Ufaransa wakikabiliana
Kundi moja la mashabiki wa Urusi lilivuka kizingiti cha maafisa wa usalama na kuanza kuwashambulia mashabiki wa uingereza ndani ya uwanja.

Kulikuwa na makabiliano zaidi katika mji wa Nice kati ya mashabiki wa Ireland kaskazini na ufaransa ambapo watu sita walijeruhiwa.

Baadhi ya wanahabari wa uingereza wameelezea matukio hayo kwenye mitandao ya kijamii, na kunyooshea kidole cha lawama, genge la raia wa urusi waliovalia mavazi meusi, wakisema waliingia uwanjani wakiwa na nia ya kusababisha vurugu.

NB: Ukweli kuwa kila mashindano amabyo hawa waingereza wanashiriki huwa lazima vurugu na waingereza ndio wanaongoza kwa vurugu kwenye michezo,hata kwenye mechi ya jana waingereza walikuwa chanzo,
tukumbuke world cup 1998 na euro 2000 pia walifanya fujo sana mpaka walipotolewa Waziri mkuu wao wakati huo Blair alishukuru na akasema bora warudi nyumbani,
miaka ya nyuma walifanya vurugu kubwa na kuuwa mashabiki wa GALATASARY ya Uturuki kwenye mechi za EUROPA kati ya LIVERPOOL lakini kama kawaida media zao na propaganda zao
 
Galatasaray na Liverpool ni Leeds walikufa mashabiki wa Leeds wawili na wa Arsenal waliumizwa wakati na Arsenal.... England ni wachokozi fujo hawawezi, BBC wanatetea watu wao ila pia Russia wanajaribu pia kutetea ujinga, Russia na Poland au Ukraine zingekutana ungeona pia fujo, FIFA wazifungie hizo timu tu au hayo Mashindano sababu tungefanya African Nation tungeitwa Wanyama na tungefungiwa CAF kwa miaka kibao. Sad kuona hizo tabia watu na watoto kupigana wanaona ujanja.
 
Ukweli kabisa Pazi hawa jamaa jana waliokuwa wanafanya kwa hapa kwetu utayaona ndondo cup ,
World cup ya 2010 pale south afrika hawa waingereza waliikosoa sana na kuonyesha dunia kama afrika haikustahili kuandaa,mpaka sasa tazama wanavyoichafua world cup ya 2022 Qatar kuonyesha kama wao wamestaarabika sana kumbe hakuna wapuuzi kama wao vile
 
Back
Top Bottom