BBC: Meli ya kivita ya Urusi yalipuliwa

Washabiki wa Putin , Watakuambia ni propaganda ...yaani ukiwa shabiki wa urusi automatically unajitahidi kuukimbia ukweli
FOjg7LLXEAEb91s.jpg
 
Yaliyomo
HabariMichezoVideoVipindi vya Redio
Mzozo Ukraine: Mji mdogo ambao ulizuia mipango mikubwa ya Urusi
23 Machi 2022
Voznesensk defenders
Ni miongoni mwa vita vikubwa vya uamuzi hadi sasa - mapambano ya siku mbili ya udhibiti wa mji wa kilimo wa Voznesensk na daraja lake muhimu.

Ushindi ungewezesha vikosi vya Urusi kusogea magharibi kando ya mwambao wa Black Sea kuelekea bandari kubwa ya Odesa na kituo kikuu cha nguvu za nyuklia.

Badala yake, wanajeshi wa Ukraine, wakiungwa mkono na jeshi la wanaojitolea, walisambaratisha mipango ya Urusi, kwanza kwa kulipua daraja na kisha kulirudisha jeshi lililovamia mpaka , hadi kilomita 100, kuelekea mashariki.

"Ni vigumu kueleza jinsi tulivyofanya. Tunashukuru kwa ari ya mapigano ya watu wetu na kwa jeshi la Ukraine," alisema meya wa Voznesensk mwenye umri wa miaka 32, Yevheni Velichko, akiwa amebeba silaha pamoja na walinzi wake wakiwa nje ya ukumbi wa jiji. .

MATANGAZO

TUNATAKA KUSIMULIA HADITHI YAKO: Je, wewe au jamaa zako muko nchini Ukraine sasa?

Lakini karibu wiki tatu baada ya vita hivyo, meya alitoa angalizo kwamba shambulio lingine la vikosi vya Urusi labda lilikuwa karibu na kwamba walinzi wa mji huo hawakuwa na silaha za kuwazuia kwa mara ya pili.

"Hili ni eneo la kimkakati sana. Hatutetei tu mji, lakini maeneo yote nyuma yake. Na hatuna silaha kubwa ambazo adui yetu anazo," alisema.

Voznesensk's strategically important bridge
Maelezo ya picha,
Daraja muhimu lililovunjwa Voznesensk ili kuzia jeshi la Urusi

Wasaidizi waliokuwa mstari wa mbele nchini Ukraine, Uingereza ilisambaza vifaru na makombora ambapo waliweza kulidhibiti jeshi la Urusi huko Voznesensk, na kuuacha mji ukiwa umejaa hadi vifaru 30, magari ya kivita na hata helikopta.

"Ni shukrani kwa silaha hizi pekee ambazo tumeweza kuwashinda adui wetu hapa. Na tunasema asante kwa washirika wetu kwa msaada wao. Lakini tunahitaji zaidi. Misafara ya adui itaendelea kuja," alisema Bw Velichko.

Umuhimu wa kimkakati wa Voznesensk ulionekana wazi punde tu baada ya vikosi vya Urusi kushindwa kulifikia daraja kubwa zaidi kuelekea kusini, kuvuka mto wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, Kusini mwa Buh.

Leo, Voznesensk sio mji uliotelekezwa, unaosumbuliwa na ving'ora au uvamizi wa anga. Lakini maelfu wameondoka katika wiki za hivi karibuni, kwa treni au kwenye barabara za mashambani zenye mashimo ambayo hupitia mashamba makubwa ya ngano

Wengi wa wale ambao wamechagua kubaki bado wanaonekana kuwa na hamu ya kuzungumza juu ya ushindi wao wa ajabu.

Voznesensk's mayor, Yevheni Velichko
Maelezo ya picha,
Meya wa Voznesensk Yevheni Velichko, akipongeza wapambanaji wa mji wake

"Ilikuwa jitihada kubwa ya mji mzima," alisema Alexander, muuza duka wa eneo hilo ambaye alijirekodi kwenye mstari wa mbele akiwa na AK47, akipiga kelele "Njooni warembo wangu wadogo!" huku mfanyakazi mwingine wa kujitolea akirusha guruneti la roketi kuelekea maeneo ya Urusi.

"Tulitumia bunduki za kuwinda, watu walirusha matofali na mitungi. Wanawake wazee walipakia mifuko mizito ya mchanga.

"Warusi hawakujua wapi pa kuangalia au wapi shambulio lingine lingetoka. Sijawahi kuona jumuiya ikikusanyika hivyo," alisema, akiwa amesimama kando ya mabaki ya daraja hilo, ambayo vikosi vya Ukraine viliharibu ndani ya saa chache katika shambulio la kwanza la Urusi.

Mizinga ya Urusi bado imeacha alama katika bustani ya Svetlana Nikolaevna, katika kijiji cha Rakove, kwenye ukingo wa kusini wa Voznesensk, ambapo mapigano makali zaidi yalifanyika.

Mzee mwenye umri wa miaka 59 alinyoosha kidole kwenye kibanda cha zana cha mumewe, akielezea kwamba askari wawili wa Ukraine waliokamatwa walikuwa wameshikiliwa hapo na Warusi na waliokolewa baada ya kuongezeka kwa mapigano.

"Angalia madoa ya damu kwenye mlango wangu," alisema, akiwaalika wageni ndani ya nyumba yake iliopo amshackle. Wakati yeye na familia yake walijificha kwenye eneo la karibu, Warusi walibadilisha nyumba yake yote kuwa hospitali kwa muda.

"Nilirudi kuchukua nguo siku ya pili. Kulikuwa na watu waliojeruhiwa wamelala kila mahali. Kumi kati yao, nadhani. Nimesafisha damu nyingi," alisema.

Svetlana Nikolaevna
"Waliondoka kwa haraka, usiku mmoja. Waliacha kila kitu nyuma - buti, soksi, silaha, helmeti - na wakapakia tu watu wao waliokufa na majeruhi wao na kukimbia."

Mkurugenzi wa mazishi wa eneo hilo, Mykhailo Sokurenko, ilimpasa kutafuta miili ya Warusi waliokufa mashambani kisha kuipakia kwenye treni.

"Siwachukulii kuwa ni binadamu [baada ya kile walichokifanya hapa]. Lakini itakuwa vibaya kuwaacha tu uwanjani, bado wanatisha watu hata baada ya vifo vyao," alisema.

"Warusi hawa wana matatizo ya akili, kwa hivyo itabidi tuwe macho. Lakini ushindi utakuja, na tutawaondoa Warusi kutoka kwa ardhi zetu zote."
Hehee hongera zao ila sisi tunapeleka moto tuuuuu!!!
 
Ukraine inaandika kwa kupewa silaha za kivita na USA na EU pamoja na askari wa msaada wa mapambano badala ya kutumia silaha zake halisi, hivi kweli ni akili zako binafsi au dishi lako limeyumba
Hata hao askari wa Russia hawapigani wenyewe. Wanasaidiwa na wapiganaji kutoka Chechnya, Belarus, nk.. na mamluki wanaokodiwa na Putin kutoka Syria na kwingineko
 
Back
Top Bottom