BBA 2010: Big Brother Africa All Stars

Status
Not open for further replies.
Akinyakua hizo $180,000/- itakuwa njema kwa Tz ila sijui atafanya investment gani au atanunua share pale TBL!?
 
NI usd 200,000 mkuu.Namuombea mungu huyu kijana ashinde.ameshapigika vya kutosha na sasa ni mtu mzima sidhani kama atarudia uli ujinga wa wakati ule na akina RC.
 
NI usd 200,000 mkuu.Namuombea mungu huyu kijana ashinde.ameshapigika vya kutosha na sasa ni mtu mzima sidhani kama atarudia uli ujinga wa wakati ule na akina RC.

Nadhani huyo Mkuu hapo juu ameishapiga ile factor ya 10% ambayo Big Broda aliwaambia housemates kwamba zawadi imepunguzwa kwa 10% baada ya lile sakata la chakula ambalo lilipelekea wakavunja sheria na taratibu za kuishi ndani ya jumba la Kaka Mkubwa. Lakini alisema kwamba hizo 10% zinaweza kurudi kama vijana wataonyesha nidhamu, nadhani ilikuwa ni mkwara tu ili kuhakikisha kwamba housemates hawarudii kufanya huo mchezo.
 
NI usd 200,000 mkuu.Namuombea mungu huyu kijana ashinde.ameshapigika vya kutosha na sasa ni mtu mzima sidhani kama atarudia uli ujinga wa wakati ule na akina RC.
..........anaweza kurudia ule ujinga wa wakati ule, maana anaweza kuwa hajakuwa kiakili!
 
Kati ya Sammy na Hannington mmoja wao ataondoka jumapili.. Hilo jumba bovu nahisi Mzee wa Morogoro na kijana wa Rural Swagga halitawapa tabu.. Kasheshe kwa kina Tatiana, Jen na wengine..
 
Alikuwa kwenye season iliyopia bana... Ni mmoja wa wale niliowapenda sana, bahati mbaya ALIONDOKA bila kuwa nominated (kama mna kumbukumbu)...



Jane alinivutia sana last season na mpaka leo sijajua nini hasa kilisababisha atoke BBA; kuna anayefahamu? hata sasa namfuatilia kwa karibu ingawa nahisi anazidisha sana kujitenga na nadhania anataka kutumia strategy ya upishi! Ila Mwisho amenipa matumaini mapya; Mpaka sasa nimemkubali na nitampa support!
 
Invisible Hi!

Ulipata PMs zangu? (Maana hapa ndio pekee nakupata)

Huanijibu what happend to Jane last season
 
Jane alitoka mwaka jana kutokana na shinikizo la mzee wake..ukipitia post za nyumba Invisible ameeleza hilo tena akisema kuwa mtoto jane anausuuza sana mtima wake!
 
Kilichomrudisha ni nini,hawa ndio wale wanauziba bahati za wengine bwana.hyo baba yake kama alimshinikiza kutoka kwa nini sasa karuhusu arudi?Tuendelee kumuombea Mwisho wetu awe wa mwisho kutoka kwenye hilo jumba la kaka mkubwa.
 
Inasemekana kwamba wakati Jeniffer akiondoka kwenda kushiriki BBA mwaka jana, baba yake hakuwepo nyumbani and he was kept in dark kuanzia kwenye kujaza fomu mpaka alipojulishwa kwamba ameteuliwa kuwa mshiriki wa BBA na hivyo ataiwakilisha Msumbiji. Baba mzazi alikuja kushangaa kumwona binti yuko ndani ya nyumba. Ndipo sekeseke la kutishia kumtaliki mkewe lilipoanza kwamba kwanini mama na binti walimficha hizo habari mpaka anakuja kushitukia anamuona binti yuko ndani ya Jumba?

Baba wa binti kwa kuzingatia heshima aliyo nayo huko kwao (nadhani ni mwana sheria maarufu huko kwao kama kumbukumbu yangu iko sahihi) na pia kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele kupigania haki za akina dada/mama na hasa kuhusiana na biashara za kwenye madanguro, ndipo alipoona kwamba binti yake alikuwa anashusha hadhi ya jina la baba na familia kwa ujumla. Baba akatishia kusambaratisha ndoa (kumtaliki mkewe) kwa tuhuma kwamba mama alishiriki dhambi ya kumruhusu binti aende BBA bila ridhaa ya baba mzazi.

That is why Jennifer alipokuwa anaondoka alisema anatoka for the sake of family na hasa mama yake, impliedly, hakutaka ndoa ya wazazi wake ivunjike kwa sababu ya ushiriki wake kwenye BBA. Kama watu wanakumbuka, siku binti anatoka alipokelewa na baba yake mzazi na kuishia nae kwenda kwao Maputo.

Kurudi kwa binti, inawezekana ni kutokana na ushawishi wake kwamba hatawaangusha wazazi wake kwa ku-misbehave ndani ya jumba na inawezekana pia age-factor. Mzazi ana control ya mtoto aliye under 18, lakini ukishafikisha age ya Jeniifer ya miaka 23 hakuna mzazi anamfunga binti ama kumpangia afanye nini katika maisha yake.

Nilichokiandika ni kile ambacho kilisemwa kwenye forum ya BB ya mwaka jana, na pia magazeti ya udaku kutoka Mozambique.
 
Haya kumekuchaaaa!

Its week 3 of Big Brother All Stars and below is how the housemates have nominated this week:

1. Tatiana: Lerato & Sheila

2. Uti: Munya & Tatiana

3. Paloma: Meryl & Munya

4. Lerato: Tatiana & Munya

5. Mwisho: Uti & Sheila

6. Code: Meryl & Lerato

7. Jen: Munya & Sheila

8. Yacob: Tatiana & Meryl

9. Munya: Uti & Yacob

10. Kaone: Tatiana & Meryl

11. Meryl: Munya & Tatiana

12. Sheila: Tatiana & Munya

Barnmates' nominations

1. Sammi: Munya & Sheila

2. Hannington: Tatiana & Munya

__________________________________

Highest Votes
------------------

Munya - 8

Tatiana - 7

Meryl - 4

Sheila - 4
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom