BAWACHA kuichelewesha CHADEMA kuingia IKULU? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAWACHA kuichelewesha CHADEMA kuingia IKULU?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Feb 27, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  WanaJF
  Ni jambo la kawaida kwa sasa kukuta watu mbalimbali majumbani,vijiweni,makazini,mashuleni na sehemu mbalimbali wakijadili siasa za Taifa letu.Na kote huko ni lazima katika kujadili siasa hizo CHADEMA itajwe.Hapo ndipo tulipofika watanzania.CHADEMA inaweza kuzungumzwa kwa njia yeyote iwe ni kwa mazuri au mabaya.Lakini jibu hapa tunapata kwamba hakuna asiyeijua CHADEMA.Nikiri tu kama makala zangu mbalimbali za huko nyuma nilivyosema CHADEMA kimefikishwa hapa kutokana na viongozi madhubuti wa chama hicho,Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.Bila kuwasahau wabunge wote machachari wa chama hicho na viongozi wengine wa Kamati kuu na Baraza kuu la uongozi.

  Dhumuni la bandiko hili ninataka kuzungumzia Baraza la Wanawake la CHADEMA-BAWACHA.Kwa hakika ukiniuliza hata kiongozi mmoja wa baraza hili ni nani simjui.Niwe muwazi kabisa siridhishwi na ukimya wa BAWACHA.Tukirudi nyuma kwenye chaguzi mbalimbali katika nchi yetu ni wazi wanawake ndio wapiga kura wakuu na tuseme ndio nguzo kuu ya CCM.Wanaume wanaweza kuwa wapiganaji wazuri na wasemaji sana lakini siku ya uchaguzi hawajitokezi kupiga kura.

  Kwanini nawalaumu BAWACHA?
  Ni ukweli ulio wazi kwamba ngome kuu ya CHADEMA kwa sasa ni vijana chini ya baraza lao BAVICHA.Na binafsi nimefurahishwa na jitihada zinazofanywa na viongozi wa vijana chini ya Mwenyekiti wao John Heche na katibu wake Deogratius Munisi.Ni juzi tu BAVICHA wamezindua jengo lao na hakika wanastahili pongezi za dhati.Sasa nikiangalia jitihada za vijana hawa kwanini jumuiya kubwa kama Baraza la wanawake wa chama liwe kimya hivyo? Tunafahamu kupitia Baraza hili CHADEMA imeteua wabunge wa viti maalum 25.Sasa hapa najiuliza idadi hii kubwa ya wabunge wa viti maalum si ndio inapaswa kuwa chachu ya kuunganisha nguvu ya kina mama mikoani? Mbona sijawahi kusikia hata mkutano mmoja umeandaliwa na BAWACHA? Ninadhani wakati mwingine unaweza kuiga mazuri kutoka kwa mtani wako.Sasa ni wakati wa BAWACHA kuangalia jinsi UWT ya CCM ilivyo imara na jinsi ilivyo chachu ya kuipa CCM ushindi wa kishindo hasa vijijini.BAWACHA wanapaswa kujua kwamba kinamama wa vijijini hawana uhuru wa kifikra na wakati mwingine wamekuwa wakibebwa na viongozi wa jumuiya ya UWT kwenda kumpigia kura hata mtu wasiyemtaka.BAWACHA wanapaswa kujua kwamba mageuzi katika mataifa mbalimbali kama ya Afrika Magharibi na kwingineko kama Zambia na Malawi yalichochewa sana na wanawake.Ilifika mahali katika kupigania demokrasia wanawake katika mataifa haya wamekuwa hata wakivua nguo na kuandamana ili dunia isikie kilio chao.BAWACHA mpo wapi?

  BAWACHA wanapaswa kufanya nini?
  · Wanapaswa kuunganisha nguvu ya kinamama kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa
  · Wanapaswa kuwa mstari wa mbele kulaani na kukemea maovu mbalimbali kwenye jamii hasa madhila dhidi ya kinamama na watoto..mf wamtazame mama Ananilea Nkya
  · Wanapaswa kujitambulisha kama nguzo kuu ya kinamama kote nchini
  · Wanapaswa kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara na ya ndani kuhamasisha kinamama kutokuogopa mageuzi
  · Wanapaswa kujitambulisha kama nguzo kuu ya CHADEMA
  · Wanapaswa kuwa na viongozi machachari wasiotishwa na wapinzani wao.
  · Wanapaswa kuepuka kuwa Baraza la kufanya mkutano siku tu wanapoteua wabunge wa viti maalum.
  · Wanapaswa kuandaa program ya kuwaimarisha vijana wakike walio masekondari na vyuoni ili kuwa wakakamavu na kuwaondolea hofu ya kuwa viongozi miaka ijayo
  · Wanapaswa kujua kazi ya BAWACHA sio kupigania ubunge wa viti maalum tu.

  Wito wangu.
  Ninatoa wito kwa viongozi wakuu wa CHADEMA hasa Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa kwamba hakika jumuiya hii inapaswa kuangaliwa upya na ni vema ikawa na mvuto kama wa BAVICHA.Si dhambi kama viongozi wa BAWACHA wameshindwa majukumu yao wakakaa pembeni wakawapisha wengine watakaoifanya BAWACHA ionekane kweli ni moto kama chama kilivyo. Nionavyo mimi BAWACHA inaweza kuichelewesha CHADEMA kuingia madarakani

  WanaJF karibuni kwa mjadala!
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  good analysis.:poa
   
 3. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nikupongeze kwa kuliona hilo,Mimi ni mmoja wa watu ambao nimekuwa nikijiuliza hivi kweli BAWACHA
  wanaeelewa kwa nini wapo? ilivyo ni kwamba akina mama wengi wamechoshwa na hali ngumu ya
  maisha,na hawana tumaini tena, nani wa kuwapa matumaini mapya? ndio maana huwa wanaishia kuvalishwa
  kanga na tisheti za CCM,si kwamba wanapenda ila hawana mbadala! Kama hapa mjini hakuna jitihada
  zozote zinaonekana za BAWACHA huko mikoani itakuwaje? Wabunge machachri wanawake wa CHADEMA
  tunaowaona Bungeni Please mko wapi? Mama Naomi Kaihura uko wapi? PULL UP UA SOCKS PLEASE!!
  Wamama wanahitaji kuhamasishwa na kupandikiziwa vuguvugu la Mageuzi.
  Naomba uongozi wa CHADEMA ni kweli liangalieni hilo kwa upya na umakini zaidi,BAWACHA
  wasiishie kukutana ofisini na wakati wa uchaguzi tokeni mitaani,wanawake wanahitaji kuhamasishwa
  maana ndio wapiga kura na waleta mageuzi.
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu

  this is real fight for the change

  kazi nzuri sana
   
 5. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  kaka maoni mazuri sana hopely yatawafikia walengwa
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Good analysis.BAWACHA wanatia kichefuchefu sana.Amkeni jamani
   
 7. Tajy

  Tajy JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Seconded 100%!naomba hawa BAWACHA,walichukulie kwa uzito na kulifanyia kazi!
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Atakayepinga hii upembuzi huu yakinifu atakuwa ana matatizo kichwani...hata mie sijui viongozi wa hii jumuiya yetu ni akina nani...Lakini nadhani tuna nafasi ya kuinyanyua jumuiya hii,kwani tuna wabunge wanawake machachari kama Halima Mdee,Esther Matiko,Suzan Lyimo nk...nadhani ni wakati wa wao kuuanzisha moto huu kama wabunge.Vinginevyo nakubaliana na wewe kuwa hii jumuiya haina maana kuwepo kama haina uwezo wa kuimarisha chama.
   
 9. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #9
  Feb 27, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  WanaJF,
  Concern and advice noted. Action already taken, naomba kwa kuanzia mfuatilie matukio ya BAWACHA katika jiji la Dar-Salaam. Feedback will be appreciated.
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Thanks Dr.We salute you.
   
 11. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Je ni Dar es salaam tu? mikoani je?
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Huu ushauri mzuri, mimi ndio nimejua leo kuwa kuna BAWACHA..
   
 13. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimependa uchambuzi huu na naona wenye mamlaka wameshauchukua, Asante sana kwa mchambuzi wetu.
   
 14. kiagata

  kiagata Senior Member

  #14
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35


  Wadau wamesikia,watafanyia kazi ushauri wako.
   
 15. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Nilishasahau kama kuna BAWACHA sijui hata uongozi wao mbaya zaidi sijawahi hatakusikia wametoa tamko ususani kipindi hiki hali ya wanawake na watoto wanapata shida sana kutokana na mfumko wa bei, Mgomo wa Madaktari na Nk.

  Napendekeza nguvu ya ziada itumike kujenga hili baraza kwani ni muhimu sana kwa kwa changamoto zilizopo mbele ya safari.
   
 16. mwanawao

  mwanawao JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 1,982
  Likes Received: 1,639
  Trophy Points: 280
  Mkuu congrats, nimeipenda sana analysis yako, natamani sana walengwa wachukue mawazo yako na kuanza kuyafanyia kazi, hawa BAWACHA hawafahamiki kabisa, mimi mwenyewe ndo nimewafahamu hapa saa hivi, wanatakiwa kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji sahivi. Watanzania tunatamani sana kuona mabadiliko kwenye nchi yetu. Please BAWACHA wake up!!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Analysis nzuri sana mkuu. Safi sana.
   
 18. M

  Molemo JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Bawacha kama mpo angalieni hili bandiko mlitafakari vizuri
   
 19. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I salute you my President.
   
 20. M

  Malova JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ni maoni mazuri. Ukizingatia Wabunge wa viti maalum wanafanyan kazi popote. Hivi wakizunguka na BAWACHA nchi nzima ukombozi utakuwa mkubwa zaidi
   
Loading...