Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,231
Ile Taasisi bora ya vijana barani Africa kwa sasa, BAVICHA, imewasili nchini Zambia ambako inawajulia hali Lundo la Wafanyabiashara wa Tanzania kutoka Tunduma na maeneo mengine ambao walitafuta hifadhi ya kibiashara nchini humo baada ya kukimbia manyanyaso nchini mwao.
Bavicha imeongea na wafanyabiashara hao katika nchi jirani ambao wamekiri kupokelewa vema nchini Zambia na kwamba kodi wanayolipa katika nchi ya watu ni Rafiki mno na kwamba wanaimudu bila shaka na wanapata faida.
Wengi wao wameapa kutorudi tena kufanya biashara nchini Tanzania.
Juhudi za kuwabembeleza bado zinaendelea.