MUSUMIFYCOM
Member
- Nov 28, 2012
- 55
- 28
*CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)* *OFISI YA BAVICHA MKOA- MARA*
*S.L.P 1537 - MARA TANZANIA*
*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*
Ndugu waandishi wa habari, kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uzima na mpaka sasa tuko pamoja nanyi, vile vile ninawashukuru kwa kufika kwenu hapa kwani si jambo rahisi kama wengi wanavyodhani. Baraza la Vijana CHADEMA MKOA WA MARA tunaamini kupitia ninyi sauti hii itasikika kwa kuwafikia wana mkoa wa Mara na Watanzania kwa ujumla.
Kwa maana hiyo basi Baraza la Vijana MKOA wa Mara kupitia kikao cha jana tarehe 06/07/2016 kilichofanyika Wilayani Butiama tumekubaliana kwa kauli moja kuunga mkono Tamko la Makamu Mwenyekiti BAVICHA TAIFA Mhe *PATRICK SOSOPI* alilolitoa tarehe 02/07/2016 juu ya *kukutana Dodoma na kulisaidia jeshi la Polisi dhidi ya wenzetu CCM kutii sheria bila shukrani.*
Aidha ifahamike sasa kuwa kupitia kikao cha vijana kilichofanyika jana Wilayani Butiama ambapo kikao hicho pia kilihudhuriwa na *Mwenyekiti wa vijana Taifa Mhe (PATROBAS KATAMBI)*, *KATIBU MKUU WA BAVICHA TAIFA Mh Julius Mwita na Mh (EDWIN SEMBEYI)* Mwenezi wa Vijana Taifa, Vijana wapatao Mia Tatu (300) walijiandikisha tayari kwa safari ya kuelekea Dodoma, Aidha hatiwazuii vijana kuendelea kujiandikisha ili kuongeza nguvu zaidi mwisho wa kujiandikisha ni tarehe *16/07/2016* tayari kwa kuanza safari ya kuelekea Dodoma bila mkusanyiko isipokuwa mmoja baada ya mwingine.
Ndugu wanahabari naomba ifahamike kuwa *BAVICHA Mkoa wa Mara* wanapenda *Amani* na hivyo hatuko tayari kuona Kauli ya Mtukufu Rais wa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR. JOHN. MAGUFURI ya kuzuia mikusanyiko haramu ya siasa mpaka ifikapo mwaka 2020 inakiukwa na Chama chochote cha Siasa hata kwa wenzetu CCM.
Hivyo basi tunakwenda Dodoma *kulisaidia jeshi la Polisi kuzuia mkusanyiko haramu unaotegemewa kuwepo tarehe 23/07/2016* kwa kutambua uchache wa polisi wetu, hatutahitaji posho wala silaha isipokuwa tutajua tunafikaje, tunakulaje na tunatumia silaha gani ama mbinu ipi kuzuia na kutawanya mkusanyiko huo haramu mnamo *tarehe, 23 /07/2016 mjini Dodoma*
Ndugu wanahabari, wengi wenu wanadhani tunaigiza lakini endapo itafika tarehe *23/07/2016*na Kauli iliyotolewa na Mtukufu Rais haijatenguliwa hapo ndipo mtaamini yakuwa tuko siliasi na tukio husika kwani hatutakuwa tayari kuona Kauli ya Mtukufu Rais wa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA inakiukwa.
Aidha nitoe Rai kwa, *Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma* kuwa sisi BAVICHA mkoa wa Mara tunajitosheleza kimafunzo na hakuna haja ya kutuelekeza kazi ya kufanya isipokuwa ni kutuweka jirani na wale watakaokaidi *Agizo la Rais* ili tushughulike nao kwa namna yoyote tutakayoona inafanana. Tutaanza safari yetu tarehe ambayo itapangwa rasmi kati ya *tarehe 20-21/07/2016* tayari kwa kuelekea Dodoma hivyo atupokee kwa moyo mmoja.
Mwisho nirudie kwa kusema sisi BAVICHA Mkoa wa Mara tunafahamika kwa misimamo na hasa pale tunapoonewa/kudharauliwa misimamo huongezeka zaidi. Hivyo hatutakuwa tayari *kuona Agizo la Rais wetu Mtukufu likivunjwa ama kukiukwa kwa namna yeyote Ile.*
*Ahsante kwa kunisikiliza*
*Imetolewa leo tarehe 07/07/2016*
*Kaunya Yohana*
*Katibu BAVICHA Mkoa Mara*
*Simu _0768-912 - 077_*
_*0756-319-206*_
*TUKUTANE DODOMA*.