BAVICHA kuwatimua baadhi ya viongozi wake

BAVICHA kuwatimua baadhi ya viongozi wake

T2015CCM

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Posts
7,930
Reaction score
991
[h=2] BAVICHA kuwatimua viongozi wake[/h] MTANZANIA, Alhamisi, Desemba 27, 2012 04:24 Na Benjamin Masese, Dar es Salaam


BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), limesema limewagundua wanachama na baadhi ya viongozi ambao ni ‘virusi’ na litaanza operesheni nchi nzima ya kuwachukulia hatua za kinidhamu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratus Munishi, alisema hawapo tayari kulea kirusi ndani ya chama ambacho kipo kwa maslahi ya chama kingine na kuongeza kuwa, wameagiza kwa viongozi kuanzia ngazi ya mkoa na wilaya kuwadhibiti.

“Kuna uvumi umekuwa ukienezwa kwamba ndani ya Bavicha Taifa kuna mgogoro, hili si kweli kwani viongozi wote wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na tupo tayari kumfukuza mtu yeyote yule anayekwenda kinyume na malengo, dhima na dira yetu.

“Kama tunavyofahamu Bavicha ndio nguzo kubwa ndani ya Chadema, kwani vijana wengi Tanzania ni wanachama wetu, hii inatokana na sera yetu ya kupigania ajira, mfumo wa elimu na matatizo yanayowakabili wananchi wote.

“Kuendeleza Bavicha tunataka kuisafisha kwa kuwachukulia hatua za kinidhamu ila hatua zetu hatuzichukui katika majukwaa tutafanya vikao vya kisheria dhidi yao, tunaomba kama mtu anajijua ni kirusi ajiondokee mapema kabla ya kukumbwa na fagio linalokuja..

chanzo; mtanzania la leo tar 27/12.
MY TAKE: kwanini Katibu anasema hakuna mgogoro huku anasema kuna kirusi??? sasa wanaoenda kuwachukulia hatua za kinidhamu wana kosa gani??? inabidi tukubali kuwa kuna tatizo ili tulitibu.
 
MY TAKE: kwanini Katibu anasema hakuna mgogoro huku anasema kuna kirusi??? sasa wanaoenda kuwachukulia hatua za kinidhamu wana kosa gani??? inabidi tukubali kuwa kuna tatizo ili tulitibu.

Kuwapo kirusi Bavicha hakumaanishi kwamba kuna mgogoro, vinginevyo uniambie hujui hata tafsiri ya neno mgogoro.
Tatizo kweli lipo, si mgogoro. Tatizo lenyewe ni kwenu masalia a.k.a PM7 kuanzisha ushirika wa uasi ndani ya chama, na hicho ndio kirusi chenyewe ambacho lazima kiondolewe.
 
Ni Mchange, Juliana, Mwampamba, Nyakarungu, Saanane, Chagulani na Gwanchele.
 
Virusi ndio vinavyoenda kuleta mgogoro! Kwa sasa kuna virusi ambavyo ndio deo anataka awascan na kuwa delete!! No Apology
 
wewe unaombea CDM kuwe na mgogoro personally itasaidia nini katika maisha yako

halafu you have a very low reasoning, kuwa na kirusi inamaanisha ndiyo kuwa na mgogoro, ungetumia maneno yako mwenyewe ungeeleweka, tatizo wewe akili yako ni vivu ukashindwa kutumia maneno ya Munishi ambayo ujumbe wake wala haujauelewa

haya ndiyo matatizo yenu wachumia tumbo, kukurupuka na akili fupi fupi
 
BAVICHA kuwatimua viongozi wake

MTANZANIA, Alhamisi, Desemba 27, 2012 04:24 Na Benjamin Masese, Dar es Salaam


BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), limesema limewagundua wanachama na baadhi ya viongozi ambao ni ‘virusi' na litaanza operesheni nchi nzima ya kuwachukulia hatua za kinidhamu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratus Munishi, alisema hawapo tayari kulea kirusi ndani ya chama ambacho kipo kwa maslahi ya chama kingine na kuongeza kuwa, wameagiza kwa viongozi kuanzia ngazi ya mkoa na wilaya kuwadhibiti.

"Kuna uvumi umekuwa ukienezwa kwamba ndani ya Bavicha Taifa kuna mgogoro, hili si kweli kwani viongozi wote wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na tupo tayari kumfukuza mtu yeyote yule anayekwenda kinyume na malengo, dhima na dira yetu.

"Kama tunavyofahamu Bavicha ndio nguzo kubwa ndani ya Chadema, kwani vijana wengi Tanzania ni wanachama wetu, hii inatokana na sera yetu ya kupigania ajira, mfumo wa elimu na matatizo yanayowakabili wananchi wote.

"Kuendeleza Bavicha tunataka kuisafisha kwa kuwachukulia hatua za kinidhamu ila hatua zetu hatuzichukui katika majukwaa tutafanya vikao vya kisheria dhidi yao, tunaomba kama mtu anajijua ni kirusi ajiondokee mapema kabla ya kukumbwa na fagio linalokuja..

chanzo; mtanzania la leo tar 27/12.
MY TAKE: kwanini Katibu anasema hakuna mgogoro huku anasema kuna kirusi??? sasa wanaoenda kuwachukulia hatua za kinidhamu wana kosa gani??? inabidi tukubali kuwa kuna tatizo ili tulitibu.
hivi huyo jamaa mwenye bold ya bluu hapo juu anatoka tabora eee! sijawahi kumsikia sikia.
 
hata reli inakona.... chadema mwendo mdundo:A S 100:
 
Na umbea ndiyo fani yenu inayowaweka hapa mjini masalia nyie.
na waliomtuma slaa akamhujuma Halima mdee ili jimbo la kage aligawe kwa mchumba wake naye ni masalia? kazi kweli kweli.hebu ngoja nikapande zangu dala dala sahizi.
 
Chadema isipowafukuza virus wote itasambaratika
 
Waanze na huyu jamaa wa Tanga,sijui Kisandu!ndo waendelee na wengine.
 
Ni Mchange, Juliana, Mwampamba, Nyakarungu, Saanane, Chagulani na Gwanchele.
Saanane anaiingiaje hapo katika wasaliti wakati ndiye aliyewaibua na kurekodi mipango yao na ushahidi kauwasilisha ndani ya ungozi wa chama.Naamini wewe ni great thinker, refer post zote kuanzia Mamuaya,Ben,j shonza,Prezzo aka Dogo(Zitto),Machange na utaelewa what I mean
 
Back
Top Bottom