BAVICHA kuwatimua baadhi ya viongozi wake

[h=2] BAVICHA kuwatimua viongozi wake[/h] MTANZANIA, Alhamisi, Desemba 27, 2012 04:24 Na Benjamin Masese, Dar es Salaam

BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), limesema limewagundua wanachama na baadhi ya viongozi ambao ni ‘virusi’ na litaanza operesheni nchi nzima ya kuwachukulia hatua za kinidhamu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratus Munishi, alisema hawapo tayari kulea kirusi ndani ya chama ambacho kipo kwa maslahi ya chama kingine na kuongeza kuwa, wameagiza kwa viongozi kuanzia ngazi ya mkoa na wilaya kuwadhibiti.

“Kuna uvumi umekuwa ukienezwa kwamba ndani ya Bavicha Taifa kuna mgogoro, hili si kweli kwani viongozi wote wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na tupo tayari kumfukuza mtu yeyote yule anayekwenda kinyume na malengo, dhima na dira yetu.

“Kama tunavyofahamu Bavicha ndio nguzo kubwa ndani ya Chadema, kwani vijana wengi Tanzania ni wanachama wetu, hii inatokana na sera yetu ya kupigania ajira, mfumo wa elimu na matatizo yanayowakabili wananchi wote.

“Kuendeleza Bavicha tunataka kuisafisha kwa kuwachukulia hatua za kinidhamu ila hatua zetu hatuzichukui katika majukwaa tutafanya vikao vya kisheria dhidi yao, tunaomba kama mtu anajijua ni kirusi ajiondokee mapema kabla ya kukumbwa na fagio linalokuja..

chanzo; mtanzania la leo tar 27/12.
MY TAKE: kwanini Katibu anasema hakuna mgogoro huku anasema kuna kirusi??? sasa wanaoenda kuwachukulia hatua za kinidhamu wana kosa gani??? inabidi tukubali kuwa kuna tatizo ili tulitibu.

Mkuu kuna tofauti kati ya mgogoro na kuwepo kwa wasaliti.

Mgogoro ni kwamba watu wameshindwa kuelewana na hata vikao Na juhudi za kusuluhisha zimeshindikana
 
Hatuwezi kusema kuna mgogoro mahala ambapo wachache wameamua kutumikia Magamba (Masalia) wakiwa ndani ya chama chetu.Bavicha Msimwonee aibu mtu. Tunataka kuwa na chama chenye viongozi waadilifu na watiifu kwa chama chetu.
[h=2] BAVICHA kuwatimua viongozi wake[/h] MTANZANIA, Alhamisi, Desemba 27, 2012 04:24 Na Benjamin Masese, Dar es Salaam

BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), limesema limewagundua wanachama na baadhi ya viongozi ambao ni ‘virusi’ na litaanza operesheni nchi nzima ya kuwachukulia hatua za kinidhamu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratus Munishi, alisema hawapo tayari kulea kirusi ndani ya chama ambacho kipo kwa maslahi ya chama kingine na kuongeza kuwa, wameagiza kwa viongozi kuanzia ngazi ya mkoa na wilaya kuwadhibiti.

“Kuna uvumi umekuwa ukienezwa kwamba ndani ya Bavicha Taifa kuna mgogoro, hili si kweli kwani viongozi wote wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na tupo tayari kumfukuza mtu yeyote yule anayekwenda kinyume na malengo, dhima na dira yetu.

“Kama tunavyofahamu Bavicha ndio nguzo kubwa ndani ya Chadema, kwani vijana wengi Tanzania ni wanachama wetu, hii inatokana na sera yetu ya kupigania ajira, mfumo wa elimu na matatizo yanayowakabili wananchi wote.

“Kuendeleza Bavicha tunataka kuisafisha kwa kuwachukulia hatua za kinidhamu ila hatua zetu hatuzichukui katika majukwaa tutafanya vikao vya kisheria dhidi yao, tunaomba kama mtu anajijua ni kirusi ajiondokee mapema kabla ya kukumbwa na fagio linalokuja..

chanzo; mtanzania la leo tar 27/12.
MY TAKE: kwanini Katibu anasema hakuna mgogoro huku anasema kuna kirusi??? sasa wanaoenda kuwachukulia hatua za kinidhamu wana kosa gani??? inabidi tukubali kuwa kuna tatizo ili tulitibu.
 
Thanks ! ni vema kuwaondoa wote wale maamluki wa ccm, Mimi naomba viongozi wa juu mje LUSHOTO TANGA, kupata ushaidi zaidi ya baadhi ya viongozi ambao wanaishi kwa njia ya CCM.
Sisi lushoto, Kwa maoni ama uhakika wa mambo niyasemayo nipigie kwa no hii +255 785 83 96 69, philip lulinda, Katibu wa vijana CHADEMA wilaya Lushoto Tanga
 
Nyoka nyoka tu ni kupiga mpaka kuua hakuna cha saanane wa SAAtisa wote ni wale wale tu.
Saa Nane amekwishatubu na kuachana na usaliti. natumaini hata kwenye vikao vya chama ataomba msamaha
 
Last edited by a moderator:
na waliomtuma slaa akamhujuma Halima mdee ili jimbo la kage aligawe kwa mchumba wake naye ni masalia? kazi kweli kweli.hebu ngoja nikapande zangu dala dala sahizi.

Akiwa wa Moshi shida iko wapi? Mbona Mwinyi, Mkapa, Jk ambao hawakuwa watu wa moshi na ndio waliouza raslimali za hii nchi, nchi imejaa rushwa na ufisadi. Kwa hayo mambo yanayofanywa na ccm, watanzania hatudanganyiki tena kwa hoja za ukabila wala udini. Watanzania tunasubiri 2015 waipe CHADEMA nchi ili tuone nao wataifanyia nini hii nchi. Ccm miaka 50 ya kutawala imetosha. Watanzania tumewachoka. Hamna jipya
 
na waliomtuma slaa akamhujuma Halima mdee ili jimbo la kage aligawe kwa mchumba wake naye ni masalia? kazi kweli kweli.hebu ngoja nikapande zangu dala dala sahizi.

Huu si ndiyo umbea wenyewe unaotengeneza, mwanaume kuwa mbea haipendezi, haya kagombee dala dala uwahi matapu tapu.Halafu hapo kwenye red bold ndiyo wapi tena huko?
 
CHADEMA ondoa uchafu kabisa tunajua hao mamluki hawawezi kabisa kuivuruga Chadema tunajua wameshalambishwa za EPA na RICHMOND wasitubabaishe kabisa MBOWE, SLAA MAFAGIO YA CHUMBA HEBU FAGIENI HUO UCHAFU
 
Back
Top Bottom