Bavicha Kuhamia Ofisi zake Mpya

Bavicha Kuhamia Ofisi zake Mpya

majibu yake huwa yanamletea matatizo sana. kuna siku dr.slaa alimpa dakika3 asalimie wananchi mpale mwembe yanga. yaani stasahau, alilala selo siku hiyo na akaambiwa awe anareport baada ya kuachiwa. mara ooh..polisi wananionea sababu nipo CDM. inabidi CDM wamfundishe lugha ya kisiasa.

Siasa ni wito!! Waganga njaa wengi siku hizi wanaharibu harakati za kupinga dhulma wanazotendewa watanzania; mwansiasa wa kweli huwa msikivu na mwenye kujibu kwa unyenyekevu hata kama hakubaliani na linalosemwa, kuhusu huyu Ng`hily hili ni tatizo kubwa hajui namna ya kujieleza na inashangaza zaidi anapojihusisha na majibizano yeye kama mwanasiasa na mwenye ndoto ya kuwa mbunge nilitegemea ajibu kwa unyenyekevu zaidi kwani hao ndio atakaowaomba kura "EVERY VOTE COUNT" sasa inachekesha sana anapotoa kauli kama teh teh sijui zinamjenga ama kumbomoa kisiasa!

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
una majibu machafu sana,ndugu yangu hatuendi hivyo,kama kiongozi lazina uwasikilize wanachama wako na kupokea maoni yao hata kama huyataki mana bili wao wewe si kitu.

Mkuu, sikukusudia kutoa majibu machafu na kwa unyenyekevu kabisa na kwa wote waliokwazwa na jibu hilo naomba mnisamehe...
 
majibu yake huwa yanamletea matatizo sana. kuna siku dr.slaa alimpa dakika3 asalimie wananchi mpale mwembe yanga. yaani stasahau, alilala selo siku hiyo na akaambiwa awe anareport baada ya kuachiwa. mara ooh..polisi wananionea sababu nipo CDM. inabidi CDM wamfundishe lugha ya kisiasa.

Mkuu, sikukusudia kutoa majibu machafu na kwa unyenyekevu kabisa na kwa wote waliokwazwa na jibu hilo naomba mnisamehe...
 
Fanya kazi watu waone. Jenga chama fungua matawi tandika, mikoroshini, nzasa, mbagala kuu, kijichi, charambe nk.

Mkuu nina operation ya siku tisini ambapo nazunguka kata zote na ikiwezekana na mitaa yote ya Temeke kwa maana ya jimbo na kwa week karibia tatu hivi niko Mtoni. Kazi ninazozifanya huko ni pamoja na kuwashukuru wanainchi kwa kutuunga mkono katika chaguzi. Lakini vile vile ni kukiimalisha chama kwa kuhakikisha tunaingiza wanachama wengi na vile vile kufungua matawi mapya..Ni ukweli inawezekana sisikiki kwa vyombo vya habari na hili ni swali ambalo nimekuwa nikiulizwa na wengi na ukizingatia kitaaluma mimi ni mwanahabari, hata hivyo hiyo ndo style ninayoitumia kufanya kazi zangu...

Mwisho nirejee kukuombeni radhi kwa majibu yangu ya awali...SAMAHANI SANA...Ukweli sikujua kama nitaeleweka tofauti na nilivyokuwa nimekusudia kueleweka.I AM DEEPLY SORRY
 
Ndugu Wapenzi, Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na watanzania kwa ujumla. Japo mimi sio msemaji wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Taifa, nimeagizwa na Katibu wa BAVICHA Taifa Mh. Deogratias Siale, kukujulisheni kuwa siku ya Jumatano 22nd Feb 2012, BAVICHA watahamia katika ofisi zao mpya pale mtaa wa Togo Opp na Kinondoni Police Station...

...

Taarifa imeandikwa vizuri. Lakini bado CDM mnatakiwa kuongeza bidii kwenye swala la kutumia lugha ya kiuenezi. Kuna taarifa moja iliandikwa na Said Shaban wa CDM Sengerema wakati wa sakata la Ngeleja kuvua uongozi wote wa Jimbo. Taarifa yenyewe nimeipaste hapo. Kwa hakika, lugha aliyoitumia ilikuwa ya kimapinduzi zaidi. Mtumieni mara kwa mara kuongeza nguvu.

CHADEMA SENGEREMA; TAARIFA KWA UMMA

​

WILLIAM NGELEJA NA HAMIS MGENJA WANAPONGEZANA KWA KUTAPELIWA! HILA HAZITAINUSURU CCM INAYOUMWA NAMBULILA!

​
KWA siku mbili mfululizo kumekuwepo na propaganda na uzushi mkubwa unaonezwa kupitia njia mbalimbali kuwa Waziri William Ngeleja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema, amehamisha uongozi wote wa juu wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema.

Kupitia taarifa hii kwa umma, CHADEMA Wilaya ya Sengerema tunapinga uzushi huo, ambao watu wazima na akili zao wameamua kukaa chini na kuupika, wakiwa na madhumuni yao ambayo kwa bahati mbaya sana yanajulikana siku nyingi sana, kwa sababu CHADEMA ni chama imara kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi ya chini kabisa inayoitwa msingi.

Tunajua kuwa uzushi huo ni sehemu tu ya mpango mkakati ambao CCM inafikiri itaweza kujinusuru, kuwasahaulisha na hatimaye kuirejesha Kanda ya Ziwa katika nchi ya Misri, baada ya watu Kanda ya Ziwa kuonesha kasi ya ajabu kuikimbia nchi hiyo ya mateso kwenda nchi ya ahadi, CHADEMA.

Tumelazimika kutozipuuza na kuamua kuzungumzia uzushi na propaganda hizi kwa sababu moja mkubwa, moja ya malengo yake makuu ni kutaka kuwavunja nguvu wananchi, Watanzania wema ambao wameamua kwa dhati kabisa kuunga mkono upinzani wa kweli unaongozwa na CHADEMA, kwa ajili ya kufikia mageuzi ya kweli ya uongozi na kupata mfumo mpya wa utawala.

Ni mwendelezo ule ule wa CCM na serikali yake kuwarubuni na kununua makapi ya uongozi ambayo yamejificha katika mwavuli wa upinzani. Mbinu hii haijaanza jana wala leo, na kwa namna ambavyo siasa za nchi hii sasa zinavyokwenda, huku CCM ikiendelea kuwadanganya……….

Lakini pia propaganda na uzushi huo ulioanzishwa na Mbunge Ngeleja na viongozi wake wa wilaya na sasa umedakwa juu kwa juu bila hata tafakuri na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgenja, pia hauwezi kuachwa hivi hivi kwani ndani yake umedhihirisha kwa kiwango cha hali ya juu namna CCM na viongozi waandamizi wa serikali yake, wanaweza kudiriki kuudanganya umma wa Watanzania mchana kweupe kwa nia ya kutimiza mchezo mchafu kwa ajili ya manufaa ya watu binafsi na chama chao. Hawaangalii taifa, wala wananchi.

Uongo na upotoshaji mkubwa katika mpango wa Ngeleja na wenzake Sengerema

Kwanza imepotoshwa kuwa mmoja wa wanaotajwa kuwa wanachama wa CHADEMA ambao wamehamia CCM, Bw. Ayub Thomas Malima, alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema, huu ni uongo na upotoshaji mkubwa, lakini ni aibu kubwa kwa CCM na serikali yake kwa sababu umefanywa kwa maelekezo na chini ya Waziri Ngeleja.

Ukweli ni kwamba, Bw. Malima alivuliwa uongozi na uanachama tangu Julai 20, 2010, katika Mkutano Mkuu ulioitishwa kujadili utovu wa nidhamu wa bwana huyo. Moja ya tuhuma zilizowasilishwa kwenye mkutano wa maamuzi ni kubainika kwa mipango yake ya kujipatia fedha kutoka kwa mgombea ubunge wa CCM, William Ngeleja ili amfanyie hujuma na kumwangusha mgombea ambaye angesimamishwa na CHADEMA.

Kila mtu anayefuatilia siasa za Sengerema tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana, mpaka sasa anafahamu hali ya Ngeleja ilivyokuwa ya hati hati kuweza kurudi bungeni, kutokana na chama chake na yeye mwenyewe kuchokwa na wananchi.

Kwa hiyo moja ya mbinu kabambe ilikuwa ni kuhakikisha kila njia inatumika, kuhakikisha anapita bila kupingwa, akiogopa kubwagwa.

Kwa umakini wa CHADEMA kama tulivyosema hapo juu, chama kiliweza kujua hata mipango ya hujuma hizo ilipokuwa inafanyika. Ilikuwa ikifanyika katika moja ya hoteli mjini hapa iliyopo Barabara ya Kamanga. CHADEMA kilikuwa na ushahidi mkubwa juu ya njama hizo, ikiwemo sauti zilizorekodiwa na hata wajumbe aliowaita ili wamsaidie kufanikisha suala hilo, bahati nzuri walikuwa waaminifu na wapambanaji wa kweli, hivyo walileta taarifa zote.

Baada ya wajumbe kumvua uanachama, Kamati Tendaji ya Jimbo la Sengerema ilimteua Ndugu Said Shabaan kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema ambaye anaendelea kukaimu hadi leo.

Sarah Mathayo, siyo Katibu wa BAWACHA kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari kadhaa, bali ni mke wa Katibu wa Wilaya (Kesy Misalaba) ambaye yeye pamoja na mmewe wana tuhuma ndani ya chama kuhusika kugawa fedha, tisheti na chumvi, vitu vilivyotolewa na CCM ili kuwapatia wapiga kura. Kiongozi pekee wa Wilaya wa BAWACHA ni Bi. Agnes F, ambaye ni Mratibu. CHADEMA hatuna cheo cha katibu wala mwenyekiti wa BAWACHA Wilaya kwa mujibu wa katiba yetu. Hii yote inathibitisha namna uongo huo ulivyo mkubwa!

Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Sengerema ni Deus Juma, ambaye mpaka tamko hili linapotolewa yuko kazini, akitekeleza majukumu yake kama ilivyo kawaida ya CHADEMA, hivyo aliyetajwa katika vyombo vya habari, Stanslaus Pastory kuwa ni Mwenyekiti wa BAVICHA ni uongo mkubwa.

Baadhi ya watu hao waliokimbia majukumu ya kutumikia umma, kwa sababu ya uroho wao na kuwasaidia wananchi kuijua rangi yao halisi, walishafukuzwa siku nyingi kwa sababu walikiuka taratibu za chama kwenda mahakamani kupinga uteuzi wa Diwani wa Viti Maalum, Bi. Sarah P. Nyanda.

Kiuhalisia, waliowahi kuwa wanachama wa CHADEMA Sengerema waliovutana na akina Ngeleja kwenda safari moja ya kifo cha CCM, ni Ayub Malima na mke wake, Bi. Luci Mussa na Kesi Misalaba na mke wake, Bi. Sarah Mathayo, wengine waliotajwa katika vyombo vya habari kuwa ni wanachama wa CHADEMA wala hata hatujui uanachama wao unafanana vipi, maana hawakuwahi kuwa wanachama wa chama hiki makini.

Chama kinapanga kufanya mikutano ya hadhara wilaya nzima ili kuwafikishia ukweli wanachama na Watanzania wote wenye moyo wa dhati katika mapambano ya kweli ya awamu ya pili, kuipigania nchi yao inayomalizwa na chama kilichofikia mwisho wa kufikiri na kuongoza.

Tuwaambie Ngeleja, Mgenja na wenzao wote katika mpango huo na CCM kwa ujumla, kuwa chama chao kinaumwa ugonjwa wa Nambulila ambao watu wa Iringa wanajua. Mtu anakuwa ni mzima, lakini hajiwezi kabisa kuzungumza. Yeye anajiona kuwa ni mzima, lakini wenzake wanaona tayari ni mfu. Hivyo wanambeba kwenda kumzika akingali mzima lakini hawezi kutamka kuwa yeye ni mzima, mpaka anazikwa akingali hai.

CCM waulize ugonjwa huo huwapata watu wenye makosa gani. CCM inaugua ugonjwa huo kwa makosa hayo hayo ambayo imefanya kwa Watanzania. Isubiri kuzikwa ikijiona!

Imetolewa leo, Januari 7, 2012

Said Shaaban

Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, Sengerema
 
Ndugu Wapenzi, Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na watanzania kwa ujumla. Japo mimi sio msemaji wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Taifa, nimeagizwa na Katibu wa BAVICHA Taifa Mh. Deogratias Siale, kukujulisheni kuwa siku ya Jumatano 22nd Feb 2012, BAVICHA watahamia katika ofisi zao mpya pale mtaa wa Togo Opp na Kinondoni Police Station...

Nyote mnakaribishwa sana kuzitembelea ofisi hizi na kupata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa BAVICHA mambo kadha wa kadha yatakayo saidia katika kuleta mabadiliko katika taifa letu. Hili linawezekana kwa kuwa sote kwa pamoja tunaamini kuwa Sababu ya kujiletea Mabadiliko Tunayo, Nia Tunayo na Uwezo pia Tunao. Hebu kwa pamoja tushikamane, na kwa hakika INAWEZEKANA...

INAWEZEKANA...Inawezekana tukajiondoa katika utawala huu dharimu usiojali na usiokuwa na suruhuisho la matatizo ya Watanzania...Inawezekana tukasimama kwa pamoja na kusema IMETOSHA...IMETOSHA kuonewa, IMETOSHA kutosikilizwa, IMETOSHA kupuuzwa na Imetosha kudhalauliwa tena katika aridhi yetu wenyewe na mbaya zaidi na watanzania wenzetu...

Hebu na tuilejeshe ila ndoto ya waasisi wetu, na hili linawezekana...Linawezekana kwa kuwa tumeishaonyesha nia yetu. Kinachotakiwa ni kusimama kidete na kwa pamoja tuupinge huu uonevu, kwa pamoja tuupinge huu unyanyasaji, kwa pamoja tuupinge huu udhalilishaji unaofanywa na watawala wetu....Ndugu zangu inawezekana, nakumbuka kuna wakati nimekuwa nikimnukuu mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake na hasa ile ya Mei Mosi kule Mbeya, alisema;

"Moja ya sifa za kiongozi au yule anayetaka kuchaguliwa kuwa diwani, mbunge ama rais; ni lazima kwanza ayajue matatizo ya watanzania ama wale watu anaotaka kuwaongoza. Lakini si kuyajua tu ila pia aumie kama watu wake wanavyoumia juu ya matatizo hayo lakini pia awe na suluhisho la matatizo hayo"....CDM tunayajua matatizo ya Watanzania, CDM tunauchungu na tunaumwa kama wananchi wanavyouma na CDM tuna mbinu na suluhisho la matatizo hayo, tunamba mtuunge mkono....

Narudia tena kusema mnakaribishwa sana kutembelea ofisi hizi mpya za bavicha na kuonana na watendaji wake...ALUTA CONTINUA ..............Tunatanguliza Shukrani Zetu za Dhati na Mwenyezi Mungu Awabariki Sana.

Mungu Ibariki Bavicha..
Mungu Ibariki CDM...
Mungu Ibariki Tanzania...

Tunashukuru kwa tarifa inatia matumaini sana, ushauri wangu kidogo kabla ya kutuma post fanya uhakiki wa ulichokiandika hasa kwa taarifa muhimu kama hii, taarifa yako inamapungufu mengi ya kiuandishi si vema kwa kiongozi kushindwa kutofautisha matumizi ya R na L.
Nakutia moyo fanya mazoezi ya lugha,
Sifa ya kiongozi bora ni yule anayekubali kukosolewa na kujirekebisha.

Natumaini utalifanyia kazi hili.
Zaidi naipongeza BAVICHA chini ya uongozi uliopo.
 
Ndugu Wapenzi, Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na watanzania kwa ujumla. Japo mimi sio msemaji wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Taifa, nimeagizwa na Katibu wa BAVICHA Taifa Mh. Deogratias Siale, kukujulisheni kuwa siku ya Jumatano 22nd Feb 2012, BAVICHA watahamia katika ofisi zao mpya pale mtaa wa Togo Opp na Kinondoni Police Station...

Nyote mnakaribishwa sana kuzitembelea ofisi hizi na kupata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa BAVICHA mambo kadha wa kadha yatakayo saidia katika kuleta mabadiliko katika taifa letu. Hili linawezekana kwa kuwa sote kwa pamoja tunaamini kuwa Sababu ya kujiletea Mabadiliko Tunayo, Nia Tunayo na Uwezo pia Tunao. Hebu kwa pamoja tushikamane, na kwa hakika INAWEZEKANA...

INAWEZEKANA...Inawezekana tukajiondoa katika utawala huu
dharimu usiojali na usiokuwa na suruhuisho la matatizo ya Watanzania...Inawezekana tukasimama kwa pamoja na kusema IMETOSHA...IMETOSHA kuonewa, IMETOSHA kutosikilizwa, IMETOSHA kupuuzwa na Imetosha kudhalauliwa tena katika aridhi yetu wenyewe na mbaya zaidi na watanzania wenzetu...

Hebu na
tuilejeshe ila ndoto ya waasisi wetu, na hili linawezekana...Linawezekana kwa kuwa tumeishaonyesha nia yetu. Kinachotakiwa ni kusimama kidete na kwa pamoja tuupinge huu uonevu, kwa pamoja tuupinge huu unyanyasaji, kwa pamoja tuupinge huu udhalilishaji unaofanywa na watawala wetu....Ndugu zangu inawezekana, nakumbuka kuna wakati nimekuwa nikimnukuu mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake na hasa ile ya Mei Mosi kule Mbeya, alisema;

"Moja ya sifa za kiongozi au yule anayetaka kuchaguliwa kuwa diwani, mbunge ama rais; ni lazima kwanza ayajue matatizo ya watanzania ama wale watu anaotaka kuwaongoza. Lakini si kuyajua tu ila pia aumie kama watu wake wanavyoumia juu ya matatizo hayo lakini pia awe na suluhisho la matatizo hayo"....CDM tunayajua matatizo ya Watanzania, CDM tunauchungu na tunaumwa kama wananchi wanavyouma na CDM tuna mbinu na suluhisho la matatizo hayo, tunamba mtuunge mkono....

Narudia tena kusema mnakaribishwa sana kutembelea ofisi hizi mpya za bavicha na kuonana na watendaji wake...ALUTA CONTINUA ..............Tunatanguliza Shukrani Zetu za Dhati na Mwenyezi Mungu Awabariki Sana.

Mungu Ibariki Bavicha..
Mungu Ibariki CDM...
Mungu Ibariki Tanzania...

Wewe ni Mtanzania?
 
Kinondoni kama mateja? Jipanueni sake mahala m bali

Mkuu,

Sijui ni sehemu gani ndani ya mipaka ya Tanzania hii chini ya serikali ya CCM na sera zake ambayo ina nafuu kuliko sehemu nyingine.Unaongelea kinondoni kwa mateja bila kuhoji imekuaje kukawa na mateja na ni nnani hasa au chama gani chenye sera zinazozalisha mateja kila kukicha.

Chadema ni chama ambacho kiko karibu na wananchi,chadema ni chama kinachopigania kupitia sera na falsafa yake kuhakikisha hao mateja unaowaongelea wanapata maisha bora na kufanya shughuli za maana ili wasiwe mateja tena kwa kupigania raslimali za taifa hili na kuhakikisha mgawanyo sawa wa raslimali.

Sidhani kama unategemea BAVICHA ijitenge na mateja na vijana wengine waliopoteza tumaini la maisha.BAVICHA ni chombo cha kuwasemea vijana wa aina hii,bavicha ni chombo cha kuwatetea vijana wanaofanywa watumwa ndani ya nchi yao,Bavicha ni chombo kinachotoa msukumo na ushawishi kwa vijana katika kusukuma mbele harakati za mabadiliko.

Inaonekana unataka BAVICHA ifananne na UVCCM iliyobakia kuwa kijiwe cha watoto wa vigogo wasiojua hali ya maisha ya vijana.Nakushauri mkuu wangu na wengine muishinikize UVCCM kama jumuiya ya chama tawala,ikishinikize chama na serikali yake kuhakikisha matatizo ya vijana yanamalizwa na kutunga sera itakayopunguza au kumaliza uzalishaji wa mateja mtaani.

Hongera BAVICHA,Ofisi ni kitendea kazi, ni miundombinu ya kutuwezesha kufikia malengo yetu.Naamini tunahitaji zaidi kujenga ofisi mioyoni mwa vijana wapenda mabadiliko ili kurahisisha harakati hizi.Tutumie ofisi hii kufanikisha malengo yetu.Nipo geita kwa sasa (Ogun-Niger Delta ya Tanzania).Hivi punde tutakoleza harakati za kudai haki,vijana huku wamefanywa watumwa maisha yao ni magumu,wamesalitiwa na watanzania wenzao,wanauawa,wanateswa,wanafukuzwa na kufanyiwa unyama kwa msaada wa polisi wanaolipwa kwa kodi ya watanzania.Tunashirikiana na BAVICHA Geita na uongozi kwa ujumla kuamsha wananchi wa Geita katika kuamua hatima yao.Hatima ya mtanzania iko mikononi mwake mwenyewe,sio kwa wageni na sio kwa wasaliti wa Tanzania
 
Kila kitu ni mipango sisi kama vijana tunahitaji kuwa na malengo jinsi ya kukijenga chama

VIVA BAVICHA
 
Mkuu, sikukusudia kutoa majibu machafu na kwa unyenyekevu kabisa na kwa wote waliokwazwa na jibu hilo naomba mnisamehe...

mimi na wewe damu damu. nmekuelewa mkuu. nakusema ili ujue mapungufu yako ujirekebishe. unakumbuka ulipoenda mti mpana nilikuletea meza usimamie na mic ya kuongelea?. siwezi kukuchukia ndugu yangu. nakutakia kazi njema mkuu. Mungu akubariki sana.
 
Mkuu nina operation ya siku tisini ambapo nazunguka kata zote na ikiwezekana na mitaa yote ya Temeke kwa maana ya jimbo na kwa week karibia tatu hivi niko Mtoni. Kazi ninazozifanya huko ni pamoja na kuwashukuru wanainchi kwa kutuunga mkono katika chaguzi. Lakini vile vile ni kukiimalisha chama kwa kuhakikisha tunaingiza wanachama wengi na vile vile kufungua matawi mapya..Ni ukweli inawezekana sisikiki kwa vyombo vya habari na hili ni swali ambalo nimekuwa nikiulizwa na wengi na ukizingatia kitaaluma mimi ni mwanahabari, hata hivyo hiyo ndo style ninayoitumia kufanya kazi zangu...

Mwisho nirejee kukuombeni radhi kwa majibu yangu ya awali...SAMAHANI SANA...Ukweli sikujua kama nitaeleweka tofauti na nilivyokuwa nimekusudia kueleweka.I AM DEEPLY SORRY

Nimekuuliza wewe ni Mtanzania? kama jibu ni ndio, mbona hujui hata kuandika lugha yako ya taifa vizuri?

Halafu unatamba kuwa ni "mwanahabari". Taaluma zimeingiliwa. Kama kiongozi unatakiwa uwe makini kwa maandishi yako na lafdhi yako, wazee tulio pembeni tuna mengi tuliyokwisha yaona kutokana tu na maandishi na lafdhi yako. Huko juu umenikera kwa kuandika hovyo Kiswahili halafu umewakera wengine kwenye majibu yako ya kifedhuli.

CHADEMA ikiwa vijana wenu ni namna hii, kazi kubwa sana mnayo. Nawashauri mnapowapeleka vijana kwa wazee wa Kiswahili, hizi kanda za pwani, muwapeleke wanaojuwa Kiswahili kizuri. Huyu katika hizo hekaheka zake itakuwa anapita baadhi ya sehemu na kwingine hathubutu. Kwa lugha tu.
 
Hiki ulichoandika ni ujinga mtupu
 
Usilete ya Jusa hapa jamvini mkuu,Kinondoni sio Tz?kama mawazo yako yalivyo,basi ofisi hizo zitakuwa mkombozi wa hao vijana.
 
Back
Top Bottom