Chadema Sengerema: Ngeleja na Mgeja wanapongezana kwa kutapeliwa! Hila hazitainusuru CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Sengerema: Ngeleja na Mgeja wanapongezana kwa kutapeliwa! Hila hazitainusuru CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Jan 8, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]
  CHADEMA SENGEREMA; TAARIFA KWA UMMA
  [/FONT]

  [FONT=&amp]WILLIAM NGELEJA NA HAMIS MGENJA WANAPONGEZANA KWA KUTAPELIWA! HILA HAZITAINUSURU CCM INAYOUMWA NAMBULILA!
  [/FONT]

  [FONT=&amp]KWA siku mbili mfululizo kumekuwepo na propaganda na uzushi mkubwa unaonezwa kupitia njia mbalimbali kuwa Waziri William Ngeleja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema, amehamisha uongozi wote wa juu wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Kupitia taarifa hii kwa umma, CHADEMA Wilaya ya Sengerema tunapinga uzushi huo, ambao watu wazima na akili zao wameamua kukaa chini na kuupika, wakiwa na madhumuni yao ambayo kwa bahati mbaya sana yanajulikana siku nyingi sana, kwa sababu CHADEMA ni chama imara kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi ya chini kabisa inayoitwa msingi.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Tunajua kuwa uzushi huo ni sehemu tu ya mpango mkakati ambao CCM inafikiri itaweza kujinusuru, kuwasahaulisha na hatimaye kuirejesha Kanda ya Ziwa katika nchi ya Misri, baada ya watu Kanda ya Ziwa kuonesha kasi ya ajabu kuikimbia nchi hiyo ya mateso kwenda nchi ya ahadi, CHADEMA.[/FONT]

  [FONT=&amp]Tumelazimika kutozipuuza na kuamua kuzungumzia uzushi na propaganda hizi kwa sababu moja mkubwa, moja ya malengo yake makuu ni kutaka kuwavunja nguvu wananchi, Watanzania wema ambao wameamua kwa dhati kabisa kuunga mkono upinzani wa kweli unaongozwa na CHADEMA, kwa ajili ya kufikia mageuzi ya kweli ya uongozi na kupata mfumo mpya wa utawala. [/FONT]

  [FONT=&amp]Ni mwendelezo ule ule wa CCM na serikali yake kuwarubuni na kununua makapi ya uongozi ambayo yamejificha katika mwavuli wa upinzani. Mbinu hii haijaanza jana wala leo, na kwa namna ambavyo siasa za nchi hii sasa zinavyokwenda, huku CCM ikiendelea kuwadanganya……….[/FONT]

  [FONT=&amp]Lakini pia propaganda na uzushi huo ulioanzishwa na Mbunge Ngeleja na viongozi wake wa wilaya na sasa umedakwa juu kwa juu bila hata tafakuri na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgenja, pia hauwezi kuachwa hivi hivi kwani ndani yake umedhihirisha kwa kiwango cha hali ya juu namna CCM na viongozi waandamizi wa serikali yake, wanaweza kudiriki kuudanganya umma wa Watanzania mchana kweupe kwa nia ya kutimiza mchezo mchafu kwa ajili ya manufaa ya watu binafsi na chama chao. Hawaangalii taifa, wala wananchi. [/FONT]

  [FONT=&amp]Uongo na upotoshaji mkubwa katika mpango wa Ngeleja na wenzake Sengerema[/FONT]

  [FONT=&amp]Kwanza imepotoshwa kuwa mmoja wa wanaotajwa kuwa wanachama wa CHADEMA ambao wamehamia CCM, Bw. Ayub Thomas Malima, alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema, huu ni uongo na upotoshaji mkubwa, lakini ni aibu kubwa kwa CCM na serikali yake kwa sababu umefanywa kwa maelekezo na chini ya Waziri Ngeleja. [/FONT]

  [FONT=&amp]Ukweli ni kwamba, Bw. Malima alivuliwa uongozi na uanachama tangu Julai 20, 2010, katika Mkutano Mkuu ulioitishwa kujadili utovu wa nidhamu wa bwana huyo. Moja ya tuhuma zilizowasilishwa kwenye mkutano wa maamuzi ni kubainika kwa mipango yake ya kujipatia fedha kutoka kwa mgombea ubunge wa CCM, William Ngeleja ili amfanyie hujuma na kumwangusha mgombea ambaye angesimamishwa na CHADEMA. [/FONT]

  [FONT=&amp]Kila mtu anayefuatilia siasa za Sengerema tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana, mpaka sasa anafahamu hali ya Ngeleja ilivyokuwa ya hati hati kuweza kurudi bungeni, kutokana na chama chake na yeye mwenyewe kuchokwa na wananchi. [/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa hiyo moja ya mbinu kabambe ilikuwa ni kuhakikisha kila njia inatumika, kuhakikisha anapita bila kupingwa, akiogopa kubwagwa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa umakini wa CHADEMA kama tulivyosema hapo juu, chama kiliweza kujua hata mipango ya hujuma hizo ilipokuwa inafanyika. Ilikuwa ikifanyika katika moja ya hoteli mjini hapa iliyopo Barabara ya Kamanga. CHADEMA kilikuwa na ushahidi mkubwa juu ya njama hizo, ikiwemo sauti zilizorekodiwa na hata wajumbe aliowaita ili wamsaidie kufanikisha suala hilo, bahati nzuri walikuwa waaminifu na wapambanaji wa kweli, hivyo walileta taarifa zote.[/FONT]

  [FONT=&amp]Baada ya wajumbe kumvua uanachama, Kamati Tendaji ya Jimbo la Sengerema ilimteua Ndugu Said Shabaan kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema ambaye anaendelea kukaimu hadi leo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Sarah Mathayo, siyo Katibu wa BAWACHA kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari kadhaa, bali ni mke wa Katibu wa Wilaya (Kesy Misalaba) ambaye yeye pamoja na mmewe wana tuhuma ndani ya chama kuhusika kugawa fedha, tisheti na chumvi, vitu vilivyotolewa na CCM ili kuwapatia wapiga kura. Kiongozi pekee wa Wilaya wa BAWACHA ni Bi. Agnes F, ambaye ni Mratibu. CHADEMA hatuna cheo cha katibu wala mwenyekiti wa BAWACHA Wilaya kwa mujibu wa katiba yetu. Hii yote inathibitisha namna uongo huo ulivyo mkubwa![/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Sengerema ni Deus Juma, ambaye mpaka tamko hili linapotolewa yuko kazini, akitekeleza majukumu yake kama ilivyo kawaida ya CHADEMA, hivyo aliyetajwa katika vyombo vya habari, Stanslaus Pastory kuwa ni Mwenyekiti wa BAVICHA ni uongo mkubwa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Baadhi ya watu hao waliokimbia majukumu ya kutumikia umma, kwa sababu ya uroho wao na kuwasaidia wananchi kuijua rangi yao halisi, walishafukuzwa siku nyingi kwa sababu walikiuka taratibu za chama kwenda mahakamani kupinga uteuzi wa Diwani wa Viti Maalum, Bi. Sarah P. Nyanda.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kiuhalisia, waliowahi kuwa wanachama wa CHADEMA Sengerema waliovutana na akina Ngeleja kwenda safari moja ya kifo cha CCM, ni Ayub Malima na mke wake, Bi. Luci Mussa na Kesi Misalaba na mke wake, Bi. Sarah Mathayo, wengine waliotajwa katika vyombo vya habari kuwa ni wanachama wa CHADEMA wala hata hatujui uanachama wao unafanana vipi, maana hawakuwahi kuwa wanachama wa chama hiki makini.[/FONT]

  [FONT=&amp]Chama kinapanga kufanya mikutano ya hadhara wilaya nzima ili kuwafikishia ukweli wanachama na Watanzania wote wenye moyo wa dhati katika mapambano ya kweli ya awamu ya pili, kuipigania nchi yao inayomalizwa na chama kilichofikia mwisho wa kufikiri na kuongoza.[/FONT]

  [FONT=&amp]Tuwaambie Ngeleja, Mgenja na wenzao wote katika mpango huo na CCM kwa ujumla, kuwa chama chao kinaumwa ugonjwa wa Nambulila ambao watu wa Iringa wanajua. Mtu anakuwa ni mzima, lakini hajiwezi kabisa kuzungumza. Yeye anajiona kuwa ni mzima, lakini wenzake wanaona tayari ni mfu. Hivyo wanambeba kwenda kumzika akingali mzima lakini hawezi kutamka kuwa yeye ni mzima, mpaka anazikwa akingali hai. [/FONT]

  [FONT=&amp]CCM waulize ugonjwa huo huwapata watu wenye makosa gani. CCM inaugua ugonjwa huo kwa makosa hayo hayo ambayo imefanya kwa Watanzania. Isubiri kuzikwa ikijiona! [/FONT]

  [FONT=&amp]Imetolewa leo, Januari 7, 2012[/FONT]

  [FONT=&amp]Said Shaaban[/FONT]

  [FONT=&amp]Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, Sengerema [/FONT]
   
 2. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hii sasa ni hatari. Kule Sumbawanga nako CCM ilifanya hivyo hivyo kwa kuwalaghai wanacahama wake kuhusu Shayo ambaye kumbe alishafukuzwa CHADEMA siku nyingi. Sasa Tena na huku Sengerema na inamhuusisha Waziri!
  Jamani viongozi wetu wa CCM, kwa haya mnayotufanyia hamtutendei haki kamwe sisi ambao tumeendelea kuwa wanachama waaminifu kwa Viongozi wetu wa Chama na Serikali. Tunahitaji kusikia kutoka CCM wilaya wanasemaje kuhusu haya yanayoendelea.
   
 3. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama jk alidanganywa kule mbeya, basi wote waliobaki wataendelea kudanganya kuwa wameibomoa CDM ili kunufaisha roho zao. Lakini wajue mwisho wasiku tutawadai pesa za walipa kodi walizokuwa wanahonga. HONGERENI CMD
   
 4. h

  hans79 JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  misifa ya kizembe ndo raha ya ccm,kwan so kosa lao wasema maskini akipata ****** hulia mwata. Yaelekea ccm ushamba u tele chamani
   
 5. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu kama ni kweli mbona mmechukua muda mrefu kukanusha?inaonyesha wazi hampo makini kabisa
   
 6. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  CCM wameshikwa pabaya,uongo ndo jadi yao
   
 7. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 667
  Trophy Points: 280
  Kumbeee.. Afadhali mmejibu mapema tumeujua ukweli.
  Ngeleja bro si usepe tu mkuu kwani lazima siasa? Wizarani umeboronga kabisa kabisa, huko jimboni ndio unadanganya kabisa .
   
 8. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa! Inaonyesha wako makini lakini walisubiria.
   
 9. mwanapolo

  mwanapolo Senior Member

  #9
  Jan 8, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Na kama hii ripoti ya CDM sengerema ni ya kweli nashindwa kushangaa hawa CCM wanamdanganya nani, maana % kubwa ya watz wameamka. Labda na kibaya zaidi wanajidanganya wenyewe.
  Imenisikitisha sana kwa mtu mzima kama waziri kufanya mambo ya kijinga kama hayo. Hii inaonyesha jinsi viongozi wetu walivyo wajinga.
  Lakini kiongozi mjinga kachaguliwa na nani? Ni aibu tu hata kuwasema kwani wote tunaonekana wajinga.
   
 10. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kaazi kweli kweli, Ngeleja na mahela yake yote anatapeliwa...
   
 11. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  HEEEEE!! CCM bhana kama vitoto vichanga, hivi wnawaza nini pale wanapodanganya wananchi kuhusu masuala ya msingi kama haya ya kusomba wanachama wa chama pinzani chenye nguvu ???? Kweli sikio la kufa halisikii dawa.......!!!
   
 12. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa nacheki taarifa ya habari ya saa 2, Star TV walikuwa wana report hii habari tena kwa mbwembwe kumbe, ni Changa la macho Magamba wamepigwa? dah..
   
 13. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #13
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Hii report nilivyoanza kuisoma juu mtiririko wake pamoja na ushahidi uliowekwa. Nilifikiri mwisho nitaona jina la mtu kama Dr. Slaa ama John Mnyika kwa maana majina makubwa tuliyoyazoea CDM.Kweli CDM ina vifaa vya kutosha na wamejipanga vyema .NGELEJA NI KILAAZA SIKU ZOTE SIO WA KUMJADILI KABISA
   
 14. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #14
  Jan 8, 2012
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mpaka 2015 tutaona na kusikia vioja vingi
   
 15. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hahahahahahahaha Magamba mishuzi+uharo vinamiminika,tunaendelea kuchimba kaburi lenu
   
 16. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  CCM pumbavu sana......mijitu mizima ina akili za nguruwe...
  Shenzi kabisa!!!!
   
 17. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,183
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Nilkwisha sema hapo awali ya kwamba ngeleja anatapatapa na jinamizi la jairo na luhanjo ,ambao wao wamekwisha anza safari ya kwenda nyumbani kumsaidia mama kutunza familia.
   
 18. t

  true JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  kweli ccm ni vilaza! Wanakuwa wambea kiac hicho?! Ni bora angekuwa Nape! Coz ndo kazi yake hiyo!! Lkn WAZIRI mzima?! Shame on him...,
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Brilliant counter-attack,

  hivi kuna nini huko CCM mbona hawajiamini kiasi hiki?
   
 20. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Very interesting

  .
   
Loading...