BAVICHA kuandaa maandamano nchi nzima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAVICHA kuandaa maandamano nchi nzima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ritz, Jun 8, 2011.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), John Heche amesema ataandaa mikutano itakayofanyanyika nchi nzima kulaani kitendo cha kukamatwa na kuwekwa ndani mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

  Akizungumza na gazeti la Mwananchi jana kwa njia ya simu akiwa Mwanza, Heche alisema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo lilitolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa la kuruhusu vijana wa chama hicho kuandamana nchi nzima.

  "Katibu ameishatoa tamko la kuruhusu maandamano nchi nzima mimi naunga mkono tamko hilo natarajia kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mikutano hiyo kwa baadhi ya mikoa." alisema

  Heche na kuongeza maandamano yanatarajia kufanyika wakati wowote.

  SOURCE: MWANANCHI JUNI 8, 2011
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CDM wasipochukua hatua za kusimamia maendeleo ya majimbo yao huenda wakaongoza hayo majimbo kwa kipindi kimoja tuu. Wengi wao wamejikita katika kukitangaza chama kitaifa (ushiriki wao kwenye maandamano sehemu mbali mbali nchini) badala ya kusimamia maendeleo sehemu walizopigiwa kura.

  Madhalani tuchukulie Jimbo la Arusha mjini, moja ya wafuasi wakubwa wa CDM ni Wamachinga na ahadi kubwa aliyotoa Mh. Mbunge ni kujenga Machinga Complex mbili. Leo hii, ambapo imebaki takribani miaka minne na miezi mitatu kabla ya kampeni za uchaguzi wa 2015 hakuna lolote (tangible) liliofanyika.

  Mvuto alioanza na Mh. Mbunge wa Arusha mjini kama hataweka mbele utekelezaji wa yale aliyoahidi, huenda mvuto wake kwa wapiga kura ukafifia kwa stahili ile ile ya Raisi wetu wa sasa.
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Watanzania wenye uchungu na nchi yetu, pesa yetu walipa kodi (Ruzuku) inakwenda tena kwenye maandamano wanakwenda kugawana posho za maandamano. Chadema wamefanya maandamano kama Sekta yao ya kugawania pesa zetu Watanzania.

  Takwimu zinaonyesha kila maandamano yanatumia zaidi ya milioni 40, na nchi hii ilivyokua kubwa mpaka waimalize kwa maandamano sijui watatumia kiasi gani cha pesa zetu Watanzania.

  Si bora hizo pesa wangechimba visima kila jimbo walioshinda uchaguzi au wangenunua madawati watoto wetu wapate pakusomea wananchi wangewapongeza.
   
 4. M

  MPG JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umetumwa na NAPE naona unawza kwa kutumia makamasi wewe,haya wasalimu masaki huko,na mdogo wako anayesoma Marekani
   
 5. z

  zamlock JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Haina haja ya maandamano kama Mbowe ametoka wapambane Bungeni saizi kupigania maendeleo.
   
 6. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Kwa nini yawe ya kulaani kukamatwa kwa Mbowe na sio wabunge wa upinzani kwa ujumla wake? Tuondokane na fikra za mwenyekiti kwani hata kukamatwa kwa Zitto na Esterina Kilasa ni mbinu chafu za kudhoofisha upinzani.

  Yakiisha hayo, yaandaliwe mengine ya kulaani uonevu wa serikali ya CCM kutumia vyombo vya serikali kwa kuwatesa wananchi (TRA na Polisi).
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu, mambo ya ajabu kabisa kila kukicha wabunge wa Chadema wao na maandamano nchi aijengwe na maandamano
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Angalia mimi nimejiunga lini JF na huyo Nape kachaguliwa lini, jenga hoja usilete porojo
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Heche mwenyewe kachaguliwa kwa rushwa, zengwe, (Bavicha) leo na yeye anataka kuwaingiza watu barabarani hii kweli ni Deceit kabisa
   
 10. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Hapo umenena kweli,na kwa muhutasari wabunge wengi wa CDM uchaguzi ujao hawatoweza kupita, pia viti maalum vitaondoshwa kitu ambacho kitakuwa ni pigo kubwa sana kwa chadema, kwani itakuwa imetengeneza wingi wa wabunge waliong'atuliwa na kuwafanya washinde kijiweni pale kinondoni kama slaa, na mbaya zaidi watakuwa hawewezi kulipwa kama Dr anavyokula kwa mlija.
   
 11. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Nia ya dhati haiwezi letwa na Mhuni, aliyehuni mafundisho ya Mungu na kuikumbatia dunia.
   
 12. L

  LAT JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  wameanzisha thread halafu wanachangia wao wenyewe .... teh teh teh

  napita tuu kwa kupotezea

  kazi njema
   
 13. m

  mkulimamwema Senior Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Time will tell whether is CHADEMA or ccm
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Endeleeni na thread yenu, maana ninyi wenyewe mlioanzisha mnatosha, bado Faiza Foxy anakuja.
   
 15. t

  tufikiri Senior Member

  #15
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO. wajinga wameshaliwa. watu wanajifanya mabalozi wa kukijibia Chama humu, kumbe hawakijui chama wala hakiwajui wao. Unacheza wewe! Mtu ameshindwa kwenye dini ndo aje aweze kwenye siasa?
   
 16. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Niliwaambia kwenye nyuzi nyingine kule watumie "scientific approach" kwenye siasa. Hawajui kuwa ngoma ikivuma sana hupasuka. Hawana jipya na hao wanaoandaa maamndamo wamejipatia njia moja ya kujipatia posho kiulaini.
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Halafu rushwa zenyewe walizianika humu JF mpaka za shillingi 1,500/= Wananchekeshaa!
   
 18. K

  Kaseko Senior Member

  #18
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  yatawashinda ya bavicha mmeshindwa kuzi allocate raslimali za uvccm kwa vijana wenu wamechoka kama matambala ya deki, bavicha ni zaidi ya Nape na uvccm na vitega uchumi vyenu vya kipumbafu mmeshindwa hata kuisaidia bodi ya mikopo itoe huduma bora kwa vijana tz.
   
 19. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kaka, Unalipa kodi wewe? in person
   
 20. K

  Kaseko Senior Member

  #20
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nape kawatuma eti, atachemka tu! Kama mvua ya masika imeshindwa umande utaweza? Dr. Slaa ni mtu makini ya mungu anayajua na hata ya dunia sasa ndie kiongozi bora na kiongoz bora ni yule anaechukia maovu na ufisadi wa viongoz wa ccm wasiomuogopa mungu.
   
Loading...