Batilda Buriani kurudi nchini baada ya kukwama Japan

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Batilda Buriani.jpg

Balozi aliyekuwa anayeiwakilisha Tanzania nchini Japan, Dk Batilda Buriani anatarajiwa kurudi nchini baada ya kukwama kutokana na ukosefu wa fedha.

Dk. Batilda aliteuliwa kuwa balozi wa Japan na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dr Jakaya Kikwete kumrithi balozi Salome Sijaona akitokea ubalozi wa Kenya kabla ya Rais Magufuli kuamua arudi nyumbani. Wizara ya mambo ya nje imethibitisha kupitia gazeti maarufu nchini.
 
bado mawaziri kuachia mzigo kwa wizara zao kupewa oc za mkate.
 
Uyu mama hajarudi bado nakumbuka uteuzi ulitenguliwa na serikal ya awamu ya 5
 
Huyu balozi si ubolozi wake ulitenguliwa na kuelekezwa arudi nyumbani? Ina maana alikuwa bado hajarejea?
sawa kabisa huyu Mama alisharudishwa Nchini na Rais Magufuli kutokea Kenya
sijui ni lini na nani alimpeleka Japan
 
Mkuu kwani huyu si rais magu alishatengua nafasi yake kipindi kirefu?
 
Naona unachanganya madawa vibaya sana. Jitahidi kufuatilia habari kwa umakini zaidi Mkuu. Kenya alishatoka zamani sana, na wakati uteuzi wake unatenguliwa na JPM alikuwa Japan.
Nakubaliana na wewe. Yaani akitokea mmoja akapotosha habari, atapata wafuasi lukuki na watatoka kwenye mada husika na kuhamia kwenye hoja isiyo na msingi:confused:
 
sawa kabisa huyu Mama alisharudishwa Nchini na Rais Magufuli kutokea Kenya sijui ni lini na nani alimpeleka Japan

hivi kwani lazima kuchangia hata kama kitu haukijui, ni aibu kuchangia huku ukijiamini wakati haupo informed. Una tatizo katika kufuatilia siasa za kimataifa.
 
Huyu balozi si ubolozi wake ulitenguliwa na kuelekezwa arudi nyumbani? Ina maana alikuwa bado hajarejea?

Huoni kilichokuwa kinangojewa? Pamoja na pengine kukamilisha miamala ya awamu ya nne huko china, lakini pia kuna jambo moja hapa naliona kama linafunikafunika uhalisia fulani kwamba "UKATA". Ukata huo ulianza tu Magufuli alipokuwa raisi au umekuja sasa anapoamua kurudi nyumbani? Au alikuwa anamalizia budget?

Ni vigumu kuelewa. Kikubwa ni kwamba tangu aamuriwe kurudi alikuwa akifanya nini hadi leo karibu nusu mwaka?
 
Back
Top Bottom