Batilda Buriani aleta balaa Ngorongoro

Batilda Buriani aleta balaa Ngorongoro

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,729
Reaction score
5,637
Ubishi mkubwa umezuka,Batilda Buriani anagombania ardhi na wanakijiji Ngorongoro.

Kwa hiyo wananchi wamefanya mkutano,amefika mwakilishi kutoka ofisi ya DC.

Yule afisa anawaambia,ok tuanze mkutano, lakini kabla hatujaanza mkutano lazima tujue kama akidi imetimia. Kwa hiyo kila mtu aandike jina lake. Isije ikawa tukafanya mkutano bila akidi kutimia.

Kwa hiyo umetokea ubishi pale na wanakijiji. Wanakijiji wanasema,nani aandike jina lake.

Last time ndivyo matatizo yalivyotokea matatizo. Mmetuorodhesha majina hapa,baadaye mkasema,tazama,Hawa wanakijiji wameridhia kumuuzia shamba Batilda Buriani.

Wanaambiwa,kama hamtaki kuorodhesha wote,basi angalau watu wawili au watu waandike majina yao.

Pia wanakijiji wamekataa. Wamesema ,tumeshakwambia Batilda Buriani hatumjui na asije hapa kutupora ardhi.

Kwa hiyo wale wazee wa kimila,wanaitwa nani wale,Lwaigatan? wamesema watavunja chungu pale kwa muda wa siku saba. Hawatagombana, watafanya kila kitu kwa amani,watavunja chungu kwa siku saba. Kuvunja chungu maana yake wanasoma "Al Badr ya Kimasai."
 
Masikini.. Wanataka wawasainishe mikataba kama ile ya kina Chief Mangungo wa Msovero
 
Chungu ni hatari ..Huyo Mama aombe msamaha na arudishe ardhi ya watu before it is too late.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom