Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
MRAMBA AELEZEA MAISHA YA JELA NA FAIDA ZA KIFUNGO CHA NJE
Aliyekuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya tatu, Basil Mramba, ameishauri Serikali kuhakikisha inawatumia wafungwa kutumikia jamii badala ya kuwarundika magerezani kwani maisha ya gerezani si salama na si njia pekee ya kumrekebisha mhalifu aliyehukumiwa na mahakama.
Kutokana na hali hiyo, alisema kuna haja kwa Serikali kuanza kutumia sheria namba 6 ya huduma kwa jamii kuwaangalia wafungwa wenye taaluma kutumika adhabu zao katika fani au taasisi za umma ili kupunguza gharama kuwahudumia watu ambao wanaweza kuisaidia jamii.
Mramba alitoa kauli hiyo jana, wakati yeye na mwenzake aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, walipomaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza Palestina, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kutumikia adhabu ya kifungo chao cha nje baada ya wiki iliyopita Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuridhia kuwa wanastahili kutumikia jamii kwa kipindi cha miezi sita hadi Novemba 5.
“Jamii inaamini jela ni sehemu salama na mtu akishikwa na hatia kwa kosa lolote, mahala sahihi ni jela tu, kule anakutana na watu wa kila aina, wenye makosa tofauti, hali ambayo inamfanya ajifunze mambo mengine mapya.
“Unakuta mtu amefanya uhalifu wa kuiba kitu, anafungwa na kupelekwa gerezani, anakutana na majambazi sugu wanaompa mbinu zaidi, sasa akitoka jela anakuja akiwa ameiva, anarudia kwenye matukio akiwa amekamilika,” alisema Mramba.
Chanzo Dar 24