Kifungo cha maisha kwa wabakaji waliotumwa na afande siyo habari njema

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
279,995
727,391
Hii sio good news ever.

Labda huelewi.

Kifungo cha maisha/Life sentence (L.S) haitawafundisha kitu hawa vijana. Kwanini nasema hivi.

1. L.S hawafanyi adhabu nje ya ngome ambazo ndio ngumu kumrekebisha mhalifu. Wao ni watu wa ndani tu kula na kulala. Wanaohukumiwa adhabu chini ya kifungo cha maisha, mfano niliyopata hupokea adhabu kali za nje ya ngome.

2. L.S hawalalii virago vibovu, wao magodoro na blanket ni nzuri na hawalali mabweni (Cells) zilizochakaa wao ni second high class baada ya #condemned.

- Nyundo na wenzake wakutwa na hatia, wahukumiwa kifungo cha Maisha Jela

3. Kulingana na sheria zetu hawa wakikaa miaka 20 wanaachiwa like hawakufanya lolote vile, sawa wanakuwa wamepoteza lkn hiyo 4m anayopewa victim haitamsaidia kitu, nikwambie na wakitoka huyo victim atakuwa 40'yrs old na hilo kwake halitakuwa limesahaulika.

4. Mind you huku uraiani ukiwa Public servant ukafanya kosa unachukiwa na kuzomewa ILA ukiingia JELA wewe ni Top Boss siku si chache atapewa mkanda na ataheshimiwa maana kule hakuna anayedeal na ulichofanya uraiani.

Huyu anaenda kustarehe...

ISITOSHE ana rufaa huyu akienda COURT OF APPEAL tutamuona uraiani nimesoma ground za kushinda ni nyingi kwasbb ya ubovu wa sheria zetu.

Mtakuja kuniambia.

Nilitegemea wafungwe miaka 30

Ambayo hii ukiappeal kwenda Court of Appeal kulingana na makosa yao wangekaa gerezani km miaka 5 hivi ndio waitwe Mahakamani.

Kwahiyo km wangepewa sentence ya 30's wangefanya adhabu za nje zote ngumu pia wangekuwa na vigezo vya kupelekwa magereza ya adhabu km kule Songea, mpk wanakuja kuitwa Mahakama wamenyooka.

PILI, ikitokea rufaa imegoma inawapandisha kifungo cha maisha ambapo napo kutoka ni mtihani
Credit: Eng_Matarra X
 
Mkuu mshana, kosa walilofanya adhabu yake ni kifungo cha maisha. Hivyo ikiwa sheria imeainisha kosa fulani hukumu yake ni hii hakimu/judge hawezi kubadili.

N.b. kifungo cha maisha haina kutoka labda wapate msamaha.
Je hawawezi kukata rufaa? Maana mtuhumiwa mkuu ga
Yule afande aliyewatuma yuko wapi? na yeye kafungwa mingapi?
Hebu tuupe muda wakati itajulikana tuu..
 
Ni ngumu kuthibitisha pasi na shaka kwamba walitumwa, mtu mzima unatumwa kufanya uhalifu kwani we robot huna judgement ya implications zake?. Kimsingi hamna namna ya kumshtaki aliyewatuma wangekuwa watoto labda ingeleta maana
Kwenye makosa hua wanabebwa,
1. Mpanga njama
2. Mtenda tukio

Kama kuna mtu aliyewatuma huyo ndie aliyepanga hizo njama za tukio zima na waliotekeleza tukio wote ni wakosaji, hatujui mwenendo wa kesi ulikuaje kama walikiri kutumwa basi aliyewatuma atafutwe na kama ni utashi wao basi adhabu inawastahili.
 
Mkuu mshana, kosa walilofanya adhabu yake ni kifungo cha maisha. Hivyo ikiwa sheria imeainisha kosa fulani hukumu yake ni hii hakimu/judge hawezi kubadili.

N.b. kifungo cha maisha haina kutoka labda wapate msamaha.
haha! ambacho hujui mweka mada hata hao wafungwa wangefungwa miaka 30 angekuja na hoja nyengine pia ya kutetea kuwa adhabu hio haitoshi!..
kuna baadhi ya watu wao saikolojia yao ni kupinga tu haijalishi umepatia ama umekosea, umefata sheria au haujafata sheria wao ni kupinga tu lkn muulize mfungwa yoyote atakuambia kifungo sio kizuri otherwise awe na matatizo yakisaikolojia!.
 
Kwenye makosa hua wanabebwa,
1. Mpanga njama
2. Mtenda tukio

Kama kuna mtu aliyewatuma huyo ndie aliyepanga hizo njama za tukio zima na waliotekeleza tukio wote ni wakosaji, hatujui mwenendo wa kesi ulikuaje kama walikiri kutumwa basi aliyewatuma atafutwe na kama ni utashi wao basi adhabu inawastahili.
Lazima kuwe na ushahidi usio na mashaka wa kumhusisha aliyewatuma. Mfano maandishi ya kuwa mkambake fulani, miamala ya fedha kutoka kwa mtumaji, watu walioshuhudia maagizo yakitolewa na fedha ikipokewa.

Tuhuma tu za kuwa alitutuma siyo sufficient kuwa evidence
 
Back
Top Bottom