Basi Sawa Tumeona Tayari Sasa Ibinafsishwe tu

Basi Sawa Tumeona Tayari Sasa Ibinafsishwe tu

Naendelea kuamini nchi imeharibika.

Tupo hapa SGR Head Office Station. Tukiwa ndani ya lounge ina kiyoyozi lakini tumelowa jasho.

Ilikuwa tuondoke saa 12 jioni kuelekea Dodoma mara bin vuu tunambiwa treni ya Dodoma hamna.

Mara mvua inanyesha Dodoma hivyo haiwezi kwenda, mara abilia wachache, mara jazeni fomu ili mrudishiwe pesa zenu mwakani, yaani mambo ni mengi hadi namkumbuka Magufuri 😢!.

Nakumbuka sijui waziri gani alisema, hata ije mvua haina gani hakutakuwa na changamoto ila tumbili alipotest kidogo mara wooooz, no safari.

Gafla treni ya kuishia Morogoro inaondoka alafu tunaambiwa pandemi humo mkaunganishe safari mbele huko 😭!.

Daaa, mimi nachoka nageuka kumuangalia mtu wa kumpiga kofi hamna natokwa jasho.

Nimewaambia ongeeni na kampuni yoyote ya mabasi walete hapa buses hapa tuondoke matokeo yake kila mtu anashangaa na wengine wanaanza kubadirika rangi.

Nchi ishakuwa ngumu hii.
Basi sawa, akabiziwe muwekezaji.
Magufuri hamka uone wanachofanya.
Nilishawahi kusema serikali ya CCM hakuna kitu hata kimoja imewahi / itawahi kufanya vizuri yaani hakuna hata kimoja. Wakitaka wafanye vizuri Kuna mambo mengi mno ya kubadilishwa na wao hawataki reforms Kwa sababu ya ulaji wao. NARUDIA HAKUNA KITU KITAFANIKIWA NA KULETA MATOKEO MAZURI CHINI YA SERIKALI HII YA CCM YAANI HAKUNA.
 
Kiongozi alikua magufuli wa ayo mambo. Kwa sasa kuna kiongozi wa nywanywanywa
 
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kusitisha safari za treni ya mwendokasi (SGR) kwa ruti ya Dar es salaam - Morogoro kwa muda kwanzia hii leo Disemba 31, 2025 kwa kile kilichotajwa uharibifi wa miundombinu uliosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli imeeleza "Shirika la Reli Tanzania (TRC) linapenda kuutarifu Umma kusitishwa kwa safari za treni ya SGR kwa muda kuanzia tarehe 31 Disemba 2025 kati ya Morogoro - Dodoma na Dodoma - Morogoro kutokana na athari za mvua zilizopelekea uharibifu wa miundombinu katika eneo la Kidete (Kilosa, Morogoro) na Godegode (Mpwapwa, Dodoma)."

"Kufuatia athari hiyo, safari zote za SGR zitakuwa kati ya Dar es Salaam - Morogoro na Morogoro - Dar es salaam hadi pale marekebisho yatakapokamilika na usalama kuthibitishwa. Hivyo abiria wanashauriwa kubadili ratiba za safari zao kuendana na mabadiliko yaliyotokea."
#MillardAyoUPDATES
 
Guys guys tulieni jamani hii sio habari ya kutangaza kama tunasherekea kukwama kwa treni. Fanyeni responsible journalism
 
GT mrangi Nakumbuka comment yako flani ukiwaonya watu humu siku za mwanzo mwanzo SGR.
Mkuu sahv tuko jirani in 2 weeks time ntakuja dental tena,aise kumbe christiania pale pamefungwa nliona hkupo kama zamani
Kuhusu sgr serikali haiwezi kuendesha maana hakuna kitu wanachoweza

Ova
 
Hii nchi haina viongozi wenye maono ya mda mrefu ina viongozi sifuri ,mambwa kabisa yaani treni mwaka mmoja tu ulimi nje,mvua kidogo tu chalii,na mvua za Dodoma zilivo ,kama ndio zitapiga zenyewe zile mpk April ,tukutane July kwenye treni
 
Mkuu! Kuhusu nauli umejaza fomu ya kurudishiwa?
 
Huu mradi wa sgr unahujumiwa na wenye biashara za mabasi na malori ya mizigo. Mnadhani mikopo ya benki watairejeshaje kama mabasi Yao hayapati abiria? Alisika mlevi mmoja huko stesheni akiropoka!
 
Ilibidi nitembee kwa miguu baada ya kuona hakueleweki.
 
Back
Top Bottom