Basi la SHABIBU lapata ajali

Wengi wa madereva ni vijana sana mie naona its time now kuwe na age limit ya madereva naona waliokwenda umri kidogo watakuwa waangalifu ni mtazamo tu.

Poleni wote mlifikwa na ajali hii mbaya.
 
nasikia kuna makusudi fulani yanafanyika
kutokana na imani za kishirikina,
wanatoa watu kafara,
but i hope i am wrong.
but hizo tetesi zipo saana.

hapa nimekumbuka jambo.....kuna haya mabasi ya saidady...ukiangalia mabasi yote ya kampuni hiyo nyuma kabisa kwa nje kwenye body juu upande wa dereva huwa kuna kakitambaa kadogo keusi kanapepea...kile huwa ni kitu gani?
 
Ukiangalia asilimia kubwa ya hizi ajali chanzo chake ni dereva ana-overtake bila kuangalia mbele anakutana na gari lingine...overtake hufanyika mahali popote hata kwenye mlima au kona!
 
Kwanini wasiwafunge hao madereva wanaokwenda kasi na kusababisha vifo kila siku?
 
Dereva wa basi husika ndie alikuwa na makosa kwa kulazimisha overtaking na ajali hii imesababisha vifo vya watu watatu. Walale mahala pema peponi. Amen
 
Ajali Mbaya:Abiria,Madereva na Trafiki nani kati yao amesahau wajibu wake?
ICU
user_online.gif
Today, 07:59 AM

hii thread ingepata mjadala wa nguvu tungetatua tatizo najua JF kuna madereva, abiria na trafiki ingsaidia lakini naona wadau wa JF wanapenda kuchangia ajali ikishatokea na kutoa pole...haisaidii sana
 
Wengi wa madereva ni vijana sana mie naona its time now kuwe na age limit ya madereva naona waliokwenda umri kidogo watakuwa waangalifu ni mtazamo tu.

Poleni wote mlifikwa na ajali hii mbaya.
Sio kweli kuwa madereva vijana sio waangalifu. Hawa wenye umri kubwa ndio wasio waangalifu na wanaendesha wanavyotaka kwa kisingizio kuwan wana uzoefu wa barabara na magari pia.
 
Suala la ajali Barabarani linahitaji utatuzi wa muda mrefu. kinachofanyika sasa ni zima moto. ajali zikitulia hakuna anayejishughulisha na hili. kuna haja ya kuifanya sekta hii kama ajira rasmi kuliko sasa kuonekana ni ajira ya watu walioshindwa kuendelea na shule.
 
Basi la Shabibu la lifanyalo safari zake kati ya DODOMA na DAR limepata ajali likishindana na lori kuna maeruhi na inasemekana kuna at least watu 2 wamekufa. more news to come. Mungu aepushe vifo zaidi na poleni walioumia

hawa matajiri wa hizi kampuni za mabasi ndio wanapashwa kulaumiwa maana wana ajiri madereva vichwa maji wasiojua madhara ya ajali wala sheria za uendeshaji magari ya abiria au kama sivyo hawa matajiri wanafanya makusudi kuuwa watu kwa malengo yao binafsi.
kampuni chache sana za mabasi utakuta madereva wao wanaendesha kwa tahadhari kubwa, nitazitaja chache nazozifahamu, dar express, mtei, ibariki tanzania,scandinavia,hood,sumry.
na utakuta haya mabasi hayapati ajali kabisa labda iwe bahati mbaya sana tena majeruhi wanakuwa wachache sana.
 
Ningeshauri apart from drivers, bus owners pia washughulikiwe, hapo ndipo wangeweza kuwadhibiti drivers wao. To me, sababu kubwa ya kutokea ajali ni uzembe wa drivers. Wanaovertake kwenye vilima, kona, mwendo kasi nk nk.
 
Watunga, wasimamizi wa sheria na taratibu katika nchi yetu wengi wamezeeka akili zao hawana uwezo wa kubuni mbinu mpya n a kisasa za kuzuia/kupunguza ajali...
Woote kina Saidi Mwema na wengineo wanachojua ni ubabe tu lakini vichwa vyao havina ubunifu kabisa, yaani ni ziro. yamezeeka na akili zao huku wakiwaacha vijana wengi mtaani wenye upeo hawana kazi.....
 
Kwanini wasijaribu kuweka traffic police kwnye kila basi linalo safiri kwenda mikoani kwa gharama za hizo company ? au hata kwenye mabasi ya kampuni zinazo pata hajali zaidi ,nadhani hilo litapunguza idadi ya ajali maana kama ndani ya basi kuna traffic police sidhani kama dreva anaweza endesha mwendo kasi au hata hizo overtake zao zisizo na akili haziwezi fanyika na hata itakapo tokea hiyo ajali huyo police ata wajibika kueleza ilitokeaje na yeye alikuaw api kuweza saidi hilo lisitokee, .. sidhani kama kuna njia nyingine ya kupunguz vifo vizivyo na ulazima.

Tunajau suala la rushwa lipo, so ina wezekana huyo police atahongwa na speed ikawa pale pale, nadhani pia wasafiri washirikishwe kwa kutoa taarifa kw anjia ya sms/

Ifanyike kama hivi, KIla ticket iweime andikwa number ambayo abiria anaweza sms kueleza kuhusu uendeshaji wa dreva ukoje na wa hatari kiasi gani .

Police anapo ingia kwenye basi atakiwe atangaze number yake ya utambulisho amabayo anakua amepewa na mamalaka ya usafiri kwa abiria.

Baada ya kutangaza namba anatakiwa kuwaelezea kua yeye yuko pale kuweza ku kudhibiti uendeshaji mbovu wa madereva ,kama aabiria wakiona kua kuna speed na uendeshaji mbaya wan weza ku sms mesege kwenye number fulani, mbayo hizo sms zitatumika kama kielelezo cha jinsi hali ilivyo kuwa kwa uendeshaji wabasi kwa safdari nzima, endapo ajali itatokea huo ujumbe utaweza kua ni moja ya ushahidi wa kutuhumu hyo police hakua ana fanya kazi yake vizuri.

Zoezi zima lina weza kua na gaharama ila gharama zote ziwe kwa wenye makampuni ya mabasi kwa gharama za safari na posho kwa huyo police .Sidhani kama gharama ni tatizo hasaa ukizingatia ajali zinavyo wapa watu garama za maisha na ulemavu , kuepuka yote hayo na dhani ni jamb muhimu kifanyike kuweza kupunguz ahizi ajali zisizo za lazima.
 
Kila wakati ajali ajali ajali....Inasikitisha sana...R.I.P wale wote waliokufa katika ajali hii,na wale majeruhi tuwaombee wapone haraka

Naogopa sana kusafiri na mabasi Tanania. Hata nikisikia wanaonihusu kwa karibu wanasafari kwa basi nakuwa na wasiwasi sana. Hii inatokana hali halisi ya ajali katika mabarabara yetu ambapo Tanzania itakuwa ni moja ya nchi zenye ajali nyingi za barabarani duniani.

Askari wa usalama barabarani, kutokana na rushwa kubwa wanazokusanya kila siku, wanachangia sana katika kuwepo kwa ajali nyingi kwa kuyaachia mabasi ambayo hayastahili kuwepo barabarani kutokana na ubovu kuendelea kusafiri, Mabasi kujaza sana kuliko uwezo wake, kuwaachia madreva ambao hawastahili kuendesha kwa kutokuwa na leseni au kutozijua kabisa sheria za barabarani kuendelea kuendesha na barabara zetu nyingi ambazo nazo kwa namna moja au nyingine zinachangia sana ongezeko kubwa la ajali za barabarani.

Cha kusikitisha zaidi ni hii Serikali iliyopo madarakani kutochukua hatua zozote muhimu ili kupunguza maafa makubwa yanayotokana na ajali hizi. Watatoa kauli zao za kisanii kila inapotokea ajali na hakuna hatua zozote zili zinazofuatia. Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema penoni na awape nguvu na faraja wafiwa wote~AMEN
 
thats real true kama nchi nyinginezo hakutokei ajali kila siku why tz? mi nadhani adhabu wanazopewa madereva wasababishao ajali hazitoshi vizuri. na kama ni ushirikina hebu hao matajiri wawe na mioyo ya kibinadamu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom